Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

unknown, confusing & difficult contents.
& bichwa langu lipo wazi, maana nazisikia sikia izi habari adi naziota live kabisa.

dunia ina mengi sana, even if u have a big soap u cant make it clean.
 
Dah mkuu hebu nitoe tongo tongo,kuna miungu wawili??hao kina Eloim sijui
Mkuu maishapopote Lilith hakuzaliwa bali alitolewa mavumbini siku moja na Adamu na wote walipewa mamlaka sawa ila baada ya uumbaji ule ndipo mungu akatambua Samael(Lucifer)alikuwa na nia ovu na kinyongo kwa Elohim ambae ndie alieumba Mbingu na nchi na kisha akamshauri mungu waumbe wanadamu kwa mifano yao (mw.1:28,Zab.8)

Kuumbwa pamoja soma (Mwa.1:27na waebrania 2:6-8)hapo utaona mke wa kwanza wa Adamu
Kisha soma (mwa.2:22)inatanabaisha Hawa kama mke wa pili wa Adamu

Somo hili ni refu jamani na ili uelewe inabidi usiwe mfia dini pekee ila uwe mfia dini wa kumjua mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba hiko kitabu mkuu
Niko tayari kutoka nje kama utanishawishi kwa hoja...na angalau evidence kidogo maana mambo ya imani ya limited evidence mi nataka kukuuliza ulishawahi kusoma the book of enoch? Kama hujasoma nikutumie kitakusaidia sana hicho kitabu hakijawekwa kwenye biblia ila kinatumika na wakristu jitahidi ukisome utaelewa haya mambo unayoyasema kwa undani sana
Enoch ni babu yake na nuhu, aliishi miaka 300 na akapaa mbinguni, alikuwepo kipindi wale malaika wanashuka kuja kutoka mbinguni na kulala na binti za binadamu...kumbuka adamu alikua babu yake enoch kwa vizazi vichache mno na Enoch ameandika kwa undani mambo hayo mnayoyazungumzia bila uhakika...kipo kisome naamini na ww utatoka nje ya box la iman yako unayoiamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii impya. Fafanua tafadhali. Mtu wa Kwanza ni Nani Kama si Adam?
Hiyo ni hoja nyingine. hoja hpa ni kwamba Adamu si mtu wa kwanza bali ni Nabii wa kwanza

Sent using LEAGOO M12
 
Hiyo ni hoja nyingine. hoja hpa ni kwamba Adamu si mtu wa kwanza bali ni Nabii wa kwanza

Aisee.... ADAMU SI MTU WAKWANZA!!!!!!!!!!! Wakwanza ni nani sasa kama si yeye? Ungesema si Binadamu wakwanza ungekuwa sahihi kabisaaaaaaa, lakin unaposema si mtu wakwanza, unazingua kabisaaaa.
 
Hii impya. Fafanua tafadhali. Mtu wa Kwanza ni Nani Kama si Adam?


Sent using LEAGOO M12
Aisee.... ADAMU SI MTU WAKWANZA!!!!!!!!!!! Wakwanza ni nani sasa kama si yeye? Ungesema si Binadamu wakwanza ungekuwa sahihi kabisaaaaaaa, lakin unaposema si mtu wakwanza, unazingua kabisaaaa.
Kapotea

Jr[emoji769]
 
Habari za Lilith hazijaandikwa popote kwenye Biblia takatifu, na huko zilikoandikwa si kwa wema bali kwa ubaya ukiachilia satanism na atheism.
Lilith atakua ni shetani lakini hakua mwana wa adam,atakua ni mmoja wa malaika walio hasi kwa molah wao.katika uumbaji alioufanya mungu akuumba kiumbe chochote chenye utashi na akili kama adam,hata hao malaika mwanzo wa biblia haijataja uumbaji wao,lakini wakati mungu anaumba mbingu na ardhi na kila kitu alikua na malaika na ndo maana mungu alipowaambia malaika wamsujudie adam ndo wakaasi na kuitwa ibilis,hata mm naweza kuungana kua ibilisi ni shetani mwanamke,lkn mara nyingi shetan anatambulishwa sana kwa jinsi ya kike zaidi ya mwanaume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba ufafanuzi kwenye hili tafadhali kama hutojali

Jr[emoji769]
wote waislam na wakristo tunaamini Adam alikuwa Nabii kutoka kwa mwenyezimungu, Na kanuni ya mtu kuwa nabii au mtume ni kutumwa kufikisha ujumbe wa mwenyezimungu kwa binadamu.kwa maana hiyo kabla ya Adamu kutumwa kulikuwa na binaadam na ndio maana yeye akatumwa kufikisha ujumbe wa mwenyezimungu kwa wale watu.
Isingewezekana mwenyezimungu amtume Nabii wake pasipokuwapo na binadaam
Kwa hiyo Adamu hakuwa mtu/binadamu wa kwanza bali alikuwa nabii wa kwanza kutumwa hapa duniani
 
Duh kumbe shetani ni demu
Lilith anayesemekana ni mke wa kwanza wa Adam. Hatajwi popote kwenye Biblia takatifu zaidi ya kwenye kitabu cha Isaya 34 : 14, na ambapo hata hivyo kutajwa kwake hakuna mahusiano kabisa na Adam.

Kuna simulizi nyingi nje ya Biblia zinazokinzana na nyingine kushabihiana kumhusu mwanamama huyu Lakini zote zinakubaliana katika jambo moja kuwa Lilith alimwacha Adam kwakuwa hakutaka kuwa chini ya amri za mwanaume. Hakutaka kuongozwa wala kutawaliwa na mwanaume kwa utetezi kwamba, wote waliumbwa siku moja na kwa malighafi zinazofanana. Hivyo hakuna mkubwa kuliko mwingine.

Sasa asili ya Lilith ni nini!? ni wapi?

Lilith anaonekana mara nyingi kwenye Biblia ya Kiebrania na huko anajulikana kama malkia wa usiku, pepo katili la usiku lenye tamaa kubwa ya ngono... Huku kazi yake kubwa ikiwa ni kuiba watoto gizani usiku. Lilith sio jina jema popote zaidi ya kwenye imani za kipagani na kishetani.

Asili ya Lilith inatajwa sana kwenye simulizi za Wayahudi (c 700-1000). Hapa anatajwa kama mke wa kwanza wa Adam waliyeumbwa pamoja (mwanzo 1:27, kisha akafuatia mke wa pili wa Adam baada ya Lilith kuondoka (mwanzo 2:22). Hapa inasemekana Lilith alimuacha Adam kwenye bustani ya Eden na hakutaka kurudi huko na kwenda kugawa kipochi manyoya kwa malaika muasi aliyeitwa Samael. Lakini pia simulizi nyingine zinasema aliondoka na kwenda kungonoka na shetani ili kuendeleza kizazi na uzao wa shetani.

Hii inaweza kuleta uhalisia kidogo kutokana na vile satanism wanavyomchukulia Lilith, kumuamini na kumwabudu kama mungu mwanamke, mke wa baba yao shetani.

Hizi zote ni simulizi nje ya Biblia takatifu lakini kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba kuna hicho kiumbe chenye jinsia ya kike kiitwacho Lilith ambacho hakuna popote kinatajwa kwq wema. Kuna mahali anaelezewa kama mchawi, pepo aliyengonoka na shetani kwa makusudi mazima ya kuendeleza kizazi chao kama tulivyoona hapo juu.


Ibada za kutoa kafara katika satanism

Tunaterejea tena kutazama yale mambo yaliyoacha utata na pengine hayajawahi kujadiliwa na wengi.

Tumeshajadiliana sana kuhudu Eden, Hawa, tunda la mti wa kati(mti wa ujuzi wa mema na mabaya), nyoka na Adam. Katika vyote hivi kuna mtu pia tumemjadili kwa kiasi, mtu huyu hata maandiko hayamtaji wala kumjadili sana. Mtu huyo ni Lilith, mwanamke anayesemekana kuwa mke wa kwanza wa Adam.

Jambo hili la Adam kuwa na mke aliyeitwa Lilith halitajwi kwenye misahafu yetu hii tunayoijua bali kwenye maandiko mengine lakini ya kiimani pia.

Lilith anayetajwa kwenye maandiko hayo kama mwanamke kiburi na mwenye nguvu, na ambaye pia inasemekana alizaliwa sawa na Adam, aliasi na kutengana na Adam baada ya kushindana tabia. Lilith alitaka kuwa na mamlaka makubwa kwa Adam.

Habari za Lilith zinaishia pale alipoachana na Adam, kisha Adam alirejea Eden kuanza maisha ya upweke akiwa kama mtalikiwa na tunaambiwa Lilith alikuja kugeuka kuwa kiumbe cha kuzimu.

Maisha ya upweke Eden yanamfanya Mungu kumtengenezea Adam msaidizi wa kufanana naye
ndipo Adam sasa anamshukuru Mungu kwa kusema. Sasa huyu ni nyama katika nyama zangu na mfupa katika mifupa yangu? (Wanazuoni wanatafsiri kauli hii kama kwamba mwanzoni alikuwepo mwingine ambaye hakutokana na Adam! ) Je, mtu huyo ni Lilith?

Maisha mapya ya furaha upendo na mapatano ndani ya Eden kati ya Adam na Eva/Hawa yanamvuta nyoka anayetajwa kama ibilisi akijulikana kama malaika aliyeasi mbinguni (Lilith?) Huyu ndio pekee aliyejua siri ya uumbaji (ukiacha Mungu) na siri ya tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya!

Kwa hakika Lilith hakupenda kabisa kuona Adam akiwa na mwanamke mwingine na hilo liko wazi hata kwa kizazi cha leo. Ule usemi wa wanawake hawapendani asili yake ni huku. Lilith kwa uwezo alionao anavaa umbo la nyoka na kumlaghai Eva/Hawa ale tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mti ambao Adam alizuiwa kula matunda yake.

Bibie Eve/Hawa bila kujua nia ovu ya nyoka anakubali kula tunda la mti wa kati ambalo aliliona ni TAMU na linapendeza kwa macho! Kilichofuatia baada ya hapo kinajulikana wazi. Nyoka akawafitinisha Adam na mkewe Hawa kwa Mungu. Wakafumbuliwa macho yaonayo na kujiona wako uchi.

Nyoka akalaaniwa kuwa atatembea kwa tumbo. Eva akalaaniwa kuwa atazaa kwa uchungu.

Adam akalaaniwa kuwa atakula kwa jasho na wote wakafukuzwa Eden palipokuwa na kila kitu cha bure.

Lengo la Lilith la kulipa kisasi likawa limetimia na kwa mtazamo huo inawezekana kabisa Lilith ndio ibilisi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wote waislam na wakristo tunaamini Adam alikuwa Nabii kutoka kwa mwenyezimungu, Na kanuni ya mtu kuwa nabii au mtume ni kutumwa kufikisha ujumbe wa mwenyezimungu kwa binadamu.kwa maana hiyo kabla ya Adamu kutumwa kulikuwa na binaadam na ndio maana yeye akatumwa kufikisha ujumbe wa mwenyezimungu kwa wale watu.
Isingewezekana mwenyezimungu amtume Nabii wake pasipokuwapo na binadaam
Kwa hiyo Adamu hakuwa mtu/binadamu wa kwanza bali alikuwa nabii wa kwanza kutumwa hapa duniani
Ok sawa sasa tuje kwenye swali la msingi binadamu wa kwanza kuumbwa na Mwenyezi Mungu ni nani?

Jr[emoji769]
 
Baba yao hao binadamu wa Kwanza kabla ya Adam,ni Nani?
Binadamu wa Kwanza kuumbwa na Mungu ni Nani?
Msaada tafadhali.
wote waislam na wakristo tunaamini Adam alikuwa Nabii kutoka kwa mwenyezimungu, Na kanuni ya mtu kuwa nabii au mtume ni kutumwa kufikisha ujumbe wa mwenyezimungu kwa binadamu.kwa maana hiyo kabla ya Adamu kutumwa kulikuwa na binaadam na ndio maana yeye akatumwa kufikisha ujumbe wa mwenyezimungu kwa wale watu.
Isingewezekana mwenyezimungu amtume Nabii wake pasipokuwapo na binadaam
Kwa hiyo Adamu hakuwa mtu/binadamu wa kwanza bali alikuwa nabii wa kwanza kutumwa hapa duniani

Sent using LEAGOO M12
 
Baba yao hao binadamu wa Kwanza kabla ya Adam,ni Nani?
Binadamu wa Kwanza kuumbwa na Mungu ni Nani?
Msaada tafadhali.

Sent using LEAGOO M12
Mkuu kwanza tukubaliane kwanza hili kisha twende sehemu nyiningi tusichanganye
 
Naweza kushawishika kwmb Adam na Eva hawakuwa viumbe wa mwanzo pekee ktk uumbaji, nashawishika kwmb kulikuwa na viumbe waliotangulia, ht km ni hao waliozaliwa na ibilisi ila walikuwepo! Mwanzo 4:17 Kaini akamjua mkewe: nae akapata mimba akamzaa Henoko.....swali la kujiuliza, ikiwa Kaini na Habili walikuwa wazaliwa wa kwanza wa Adam na Eva, mke aliyeolewa na Kaini alitoka wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom