Mwanagenzi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2006
- 738
- 273
Hapo mwanzo niliona mtu mwenye cheo aketiye barazani, aliyeamuru nani aongee na nani aketi chini. Nikaambiwa mtu huyu hatendi kama ilivyopaswa. Nikapewa ujumbe nimuonye mtu huyu kabla ya anguko lake, naye hakunisikia akajiendea na shauri lake. Baada ya miaka mitatu ya utawala wake, na baada ya utawala uliotoka kwenye nchi yenye maziwa mengi na asali iliyolambwa na wengi na siyo wachache kuanguka, basi yule mtu mkuu aketiye barazani akapewa amri asiseme tena neno liwalo lolote. Naam mkuu yule akatii. Akawa mpole kama hua.
Hatimaye nikaona kiongozi mmoja, kijana, wa mkoa wenye madini na mifugo mingi nao watu weupe kutoka mbali hupenda kuutembelea, akipambana nami. Akapata misukosuko lakini hatimaye akanishinda. Kijana yule akatawala eneo hilo licha ya maneno mengi mabaya kuhusu yeye.
Nikaona kiongozi mwingine kijana, wa wilaya moja jirani na mkoa nilioutaja hapo juu, akipambana na wanasiasa na matajiri wa kaskazini. Nikamwonya aache njia zake naye hakunisikiliza. Hatimaye baada ya siku kadhaa kupita yule kiongozi kijana akawa na huzuni kubwa,nikaambiwa alipata msiba mkubwa sana. Na tazama punde si punde nikaona yule kijana akifikishwa kwa pilato, naye akajitetea, lakini akatupwa mahali pa giza. Watu wengine wakashangilia ila wengine wakahuzunika wakisema kijana yule hakufanya yale aliyofanya kwa faida yake bali kwa manufaa ya waliompeleka na wengi pia.
Yule kiongozi kijana baada ya muda kupita, akajitetea kwa pilato mkubwa zaidi ya yule wa awali, naam, mawakili wake waitwao wasomi, wakamsaidia, yule kijana akashinda daawa lililokuwa mbele yake, akawabwaga watesi wake.
Lakini haukupita usiku hata mmoja, yule kijana akatiwa mbaroni na kutupwa tena kwenye giza kwa makosa mengine mengi. Kijana akapatwa na fadhaa, akaugua, akafanyiwa upasuaji kwenye kichwa, akalia na akasaga meno, lakini haikusaidia kitu. Haya yote yalitokea katika kipindi cha kutawala kwake malkia mwenye binamu zake kule Ghuba za Ajemi, na nchi za jangwa, na hari kwa wingi, na tende na ngamia.
Mambo haya yote nilifunuliwa nikiwa kwenye nchi yenye baridi, na barafu na theluji. Naam, kuanguka kwa watawala na kuinuka kwa utawala mpya wa malkia kulitokea nikiwa ughaibuni. Na hata lile anguko kuu, lililoleta simanzi, nilipata kusikia sauti yake nikiwa huko kwenye theluji, na nilipata ujumbe mapema kutoka kwa watawala waliokuwepo kabla, kuwa mwamba umeanguka.
Kwa vile sikupenda sana kukaa kwenye baridi, na barafu na theluji, nikawauliza watawala waliokuwepo kabla kama ningeweza kurudi kwenye nchi yenye joto, na wale waendeshao magari ya moto yenye magurudumu mawili, wanaokula unga uliotiwa maji ya moto na kisha kukorogwa na kukaushwa.
Basi wale watawala waliokuwepo kabla, ambao walisafiri pande zote za dunia wakati walipokuwa wakitawala, wakasema watamrai malkia ili niweze kurudi kwenye mji wa wazee wangu. Naam, haukupita muda mrefu nikapokea ujumbe kutoka kwa malkia kuwa naweza kurejea kwenye nchi ya maziwa na asali, isiyo na baridi kama kule nilikokuwa. Na kwamba hakuna shauri litakalosimama tena mbele yangu, maana yote ni ubatili mtupu. Na kwamba tuko kwenye zama za masikilizano; zama za kulamba asali na mbuzi kula kwa urefu wa kamba zao.
Naam, zama za mbuzi na mwanakondoo kulala kwenye zizi moja na mtoto wa chui, mwanapunda na jike la simba.
Baada ya kurudi kwenye mji ule wa wazee wangu, watu wengi wakaja kunilaki, na mitende na masale, na tazama, nikaona vijana wengi wanapata ajali na wengi kufariki kutokana na kufanya kazi ya laana; kazi ya kukimbiza upepo barabarani si kwa farasi bali kwa magari ya moto yenye magurudumu mawili, na wengi katika mji ule wanakula chakula kisichofaa, kinachodumaza akili. Nikapata ujumbe wa kuwaonya, baadhi wakanisikia, na baadhi wakanipuuzia.
Siku zikapita, na wakati yule malkia aliyetawala kipindi kile akifanya sherehe, kushangilia utawala wake, baadhi ya watu wakalalamika, kuwa maisha ni magumu sana ikilinganishwa na wakati wa utawala uliotangulia. Watu wengine nao wakasema si vema kugawana madaraka na maadui.
Kule kwenye umoja wa watawala wanaosubiri nafasi ya kutawala, nako kukatokea uasi, na umoja ukagawanyika. Wengine wakiwalaumu wenzao kuwa eti wanalamba asali peke yao. Na kwamba na wao waliumizwa na kupoteza mali na hadhi zao wakati wakipigania maslahi ya umoja wa wote.
Kukawa na vurugu na malumbano na mnyukano, watu wengi wakasema wanataka kutungwe sheria mpya za kugawana maziwa na asali na mikate na nyama kwenye nchi hii iliyobarikiwa. Na tazama, nikapitiwa na usingizi.