Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
- Thread starter
-
- #61
Dah ni kweli,lakini sijakupata vizuri.Ninachotaka nipe idea angalau jinsi ya kupunguza huu ufisadi ,because we are kooking for solutions.Do you mean I must start with myself first? Ninachoona hapo hakuna anayeweza kumuwajibisha mwenzie. bosi atamuonea haya Mfagizi kumwambia usitoroke kazini,sababu huwa anamtuma wakati mwingine sokoni kununua vitu vya nyumbani.Hebu nielezee vizuri tafadhali.
Binti Sayuni,
Kanisani kuna ule wimbo "Toa kwanza boriti, kwenye jicho lako, ndipo utaona kibanzi, kwenye jicho la mwenzako...."
As a nation tumepoteza mwelekeo, hakuna moral wala ethics zozote. Hatueshimiana wenyewe kwa wenyewe, mfano utakuta mmepanga mstari benki kwa masaa na mtu mwingine bila aibu anakuja na anaingia mbele ya mstari bila hata aibu.Na mara nyingine raia au wateja wengine hatakusema lolote hawasemi.....its a shame.
Mkandara
Miafrika ndivyo Ukiwemo wewe? na Rev. Kishoka?? huko ni kukata tamaa. kuna watu wengi tu wanajitahidi kujikwamua kwenye makucha ya manyang'au na mafisadi...afadhali uwatafute uungane nao kuliko kukata tamaa.
mkuu unauliza kitu ambacho ni wazi kabisa?.. hivi ukisikia Miafrika ndivyo TULIVYO, wewe unaelewa vipi?Mkandara
Miafrika ndivyo Ukiwemo wewe? na Rev. Kishoka?? huko ni kukata tamaa. kuna watu wengi tu wanajitahidi kujikwamua kwenye makucha ya manyang'au na mafisadi...afadhali uwatafute uungane nao kuliko kukata tamaa.
MSOME HUYU;Shida ya Umeme, Uhaba wa Maji, Foleni za Magari, Takataka na Mazingira Machafu.
Takataka ni kila kona, na kila mtu anajitupia takataka anapopenda. Kila baada ya mita 500, kuna kijilima cha matakataka yaliyozagaa, iwe ni Masaki, Chang'ombe, Manzese au Kariakoo.
je Upinzani Tanzania una kazi gani na manufaa gani?
Yote ni kweli. Lakini tatizo kubwa ni toka ngazi za juu kama viongozi kazi zao hawajui wajibu wala hawaoni haya hali kama uchafu ni kawaida kwao, mwananchi atajitahidi kadri ya uwezo wake lakini kama kiongozi hajali. Ndo inabidi uwe msafi kwako nje huna hila Waafrika tunataka viongozi wenye kujituma na kuchagua wafanyakazi wanaoweza kufanya kazi bila usimamizi, kujivunia kazi tukijilinganisha na wenzetu wa majuu kazi anaiheshimu hata kama ina mshahara mdogo lajini kama unaifanya kwa usanifu boss anagawa mshahara ziada.Kila mara naisikia sauti ya Nyani Ngabu Julius ikisema Miafrika Ndivyo Tulivyo. Kisha kwa mbali Bob Mkandara hunguruma watu na mazingira. Kisha FMES humalizia kwa kusema viongozi wetu ni image yetu wenyewe.
Kwa wiki tatu, kauli hizo nimezithibitisha tena kuwa ni sahihi na kwa masikitiko makubwa nikakubali kuwa ndio hali halisi.
Kuna vitu kadhaa ambavyo nitavigusia kwa undani kuhitimisha au kuainisha maono ya Mchungaji.
- Kwanza, Watanzania wengi sana ni Mafisadi kwa namna yao.
- Pili, Watanzania wengi sana wameridhika na dhiki, kero, shida na umasikini na wanaita ni hali halisi!
- Tatu, Watanzania wengi wamenogewa na kutegemea misaada na kupewa.
- Nne, Rushwa na Takrima si uhalifu tena, bali ni haki na halali ili mtu apate haki yake au atimiliziwwe mahitaji.
- Tano, Sheria, Kanuni na Taratibu zipo, tena nyingi sana, lakini kila mtu anajifanyia analotaka bila kujali matokeo ya yeye kukiuka Sheria au kanuni na wale walio na majukumu na wajibu wa kuhakikisha kuwa Sheria zinafuatwa na zinafanya kazi inavyopaswa, hawafanyi kazi zao na wanafumbia macho kwa makusudi ukiukwaji na kuvunjwa kwa sheria.
- Sita, hakuna Uongozi na Viongozi. Kila mtu na lwake na Serikali iko Likizo.
Shida ya Umeme, Uhaba wa Maji, Foleni za Magari, Takataka na Mazingira Machafu.
Hivi vitu nilivyovitaja hapo juu, ni vitu tosha kabisa kuelewa Tanzania ni Taifa la namna gani na Watanzania ni watu wa namna gani.
Jiji la Dar Es Salaam, kila siku kuna foleni ya magari inayoanzia saa 11 asubuhi. Ukitoka Kibaha, kwenda Pale Askari Monument, jiandae kutumia si chini ya masaa matatu, iwe ni alfajiri au hata jioni tena ile ya kuondoka mjini saa 2 usiku.
Sehemu nyingi za mji wa Dar Es Salaam, hazina maji ya kutosha au kuaminika kuwa kutakuwa na maji. Dawasco wamekata mabomba ya watu, wakidai kuna maji ya Mchina, halafu Dawasco hao hao hufuata raia na kuwauzia maji.
Umeme ni tatizo sugu, kila siku kuna shida ya umeme, iwe ni viwandani, maofisini na majumbani. Unajiuliza, kama Dar ndio kinara cha uzalishaji wa nchi yetu ina shida kubwa namna hii ya Umeme, ni lini tutapata maendeleo?
Takataka ni kila kona, na kila mtu anajitupia takataka anapopenda. Kila baada ya mita 500, kuna kijilima cha matakataka yaliyozagaa, iwe ni Masaki, Chang'ombe, Manzese au Kariakoo.
Sasa kilichonishangaza na kuniudhi ni ile tabia ya Watu wa Dar Es Salaam, kuonekana kuwa ama wameridhika na hali hiyo ya kukosa Umeme, Maji, Foleni na Takataka au basi wamekubali kuwa hawana jinsi yoyote ile bali kuikubali hali halisi.
Wananchi wanasema "what's a big deal about it" na Serikali nayo inasema "what's the big deal about it"!
Sasa kutokana na tabia hizi, kinachotokea Dar ni vurugu tupu-Chaos, Disorder and Disorganization.
Watu wa Dar ambao ndipo mtu ungetegemea pangekuwa ndio chimbuko la kuiwajibisha Serikali kwa kutaka Serikali itumikie wananchi, wamekaa kana kwamba wao wanamilikiwa na Serikali (very passive and submissive) na hawana sauti.
Matokeo yake, kila mtu anafanya analotaka na thubutu umuulize.
Mfano kwenye foleni za magari, kila mtu anavunja sheria na kanuni za uendeshaji magari ili kuhakikisha anawahi anakotaka kwenda. Lakini ukimuuliza haraka hii ya nini au ina manufaa gani hakupi jibu kama vile anachelewa kazini, anatumia mafuta mengi kwa umbali mdogo au kuwa ni ameudhika kutokana na matuta yaliyojazwa barabarani au udogo wa barabara.
Hali kadhalika kila mtu mwenye pesa yake anajijengea anavyotaka, bila hati, bila kufuata mipango miji tena mbaya zaidi ni Wasomi ndio wanaoongoza kwa hili.
Tabia ya kuombaomba na kutegemea imekuwa sana. Zaidi inakera kuwa watu wanaomba hongo bila woga na si ili wakusaidie upate kitu, bali wanakuambia tupatie chakula. Ukimkatalia anakubeza! Watu kutegemea kupewa pesa au misaada ni uonjwa sugu na donda dugu, na hili si la Dar pekee, nenda mpaka vijijini, watu wanasuiri mfadhili.
Nguvu ziliniishia siku moja nilipoona kwenye gazeti picha ya shule fulani na tamko la uongozi wa shule lililosema kuwa linaomba wafadhili wawajengee Waalimu choo. Sasa mfadili awe ni Mzungu au Mchungaji Kishoka, ni vipi mpaka choo kitushinde kuchimba tusubiri ufadhili?
Serikali ipo, lakini imelala usingizi mzito kabisa na kukoroma. Haijigusi wala kujiuliza kuwa huu mfukuto wa kero , mwisho wake ni mlipuko mkubwa kuliko yale mabumo ya Mbagala.
Hakuna Sauti yenye kutoa agizo wala amri. Hakuna nahodha wa kuonyesha dira au kuongoza Merikebu inavyopaswa.
Lakini Serikali yetu, jamani inajua kuzichuma, ukiangalia nyumba za wakubwa na magari wanayotumia yale ya kifahari, unajiuliza, je hawa ni watumishi wa umma au umma unawatumikia?
Sasa kwa kuwa Ufisadi ni mfumo ulioshamiri na kukubalika kirahisi na kila mtu kama ndio njia sahihi ya kujipatia mahitaji ili kuondokana na kero, basi vita ya kumkaba koo Jeetu Patel, Chenge na Rostam itakuwa ngumu mno na hata zile kauli za Sitta na Mwakyembe nilizozilaani waliposema wapiga kura wakihongwa wachukue hizo pesa na kuzila, inaonyesha kuwa Rushwa, Takrima na Hongo ni kitu cha ulazima na cha kawaida katika maisha ya Mtanzania.
Nikirudi kwenye uongozi, nilichobakiwa nacho ni masononeko. Mfumo mzima wa Uongozi na Kiutawala unabidi kubadilika na kubadilishwa, lakini kazi hiyo ni ngumu kwa kuwa ni wananchi wenyewe ndio wanapaswa kubadilika kwanza.
Kama watu wa Dar wameridhika na dhiki, kero na shida za kila siku na wala Serikali na chama tawala wala havisumbuki au kuhofia kupoteza japo kiti cha Udiwani au Ubunge, je Upinzani Tanzania una kazi gani na manufaa gani?
Waliojitahidi kuonyesha kukerwa ni wale Wanafunzi wa Kibasila na pale Kimara kwa Msuguri ambao walizuia magari yasipite, wenzao walipogongwa na magari na kupoteza maisha.
Kwa unyonge tena mkubwa nakubali, Ndivyo Tulivyo!
Rev.Kishoka,
Usinichekehse miye weee! yaani hatan wewe ulipita ukakiona ukakiacha kama wengine kisha unauliza jibu wakati mwenyewe unalo mkuu..duh! ama kweli nasikia raha tupu na vundo la Bongo!
Nitazidi kuuliza hao wananchi wataukusanya huo uchafu waulpeleke wapi?..Hivi kweli unategemea mtu wa kawaida achukue hata mkokoteni hadi tabaka Dampo, hana kazi nyingine jamani. Uchafu umeshakusanywa, umetupwa sehemu moja ni kazi ya Halmashauri ya mji kushughulikia kazi nyingine. Mimi hadi sasa hivi sikubaliani na usemi kwamba wananchi ni wachafu hata kidogo, pamoja na umaskini wao wanafagia nyumba zao za vumbi na wengi sana wanajitahidi hata kupanda michongoma na kuweka bustani katika maeneo yao..Lakini tazma amaeneo yote yanayomilikiwa na hizo halmashauri ni mashauri kweli!..
Rai ya Jenerali
Kitoto Chetu, Ovyo Toka Mbelekoni
KAMA nilivyoahidi, sasa napenda kujielekeza, na kumwelekeza msomaji wa safu hii, katika suala la familia ambako ndiko inaelekea tunataka kutafuta 'wokovu' wetu kila tunapokumbana na suala la kumpata kiongozi, hasa baada ya Bwana Mkubwa kufariki, au yanapotokea matatizo na malumbano katika mchakato wa kurithisha utawala.
Ni muhimu kuiangalia familia kama kituo cha msingi, selo, katika ujenzi wa jamii, jumuiya na taifa kwa ujumla, kwani wananchi walio wengi katika jamii yo yote ile wametokana na familia ya aina moja au nyingine. Inawezekana huko tuendako wakazuka 'wahandisi wa kijamii' watakaobuni aina nyingine ya selo itakayochukua nafasi ya familia, lakini kwa sasa hatuna budi kuenenda kwa kuijali familia, na kuisaili vile vile.
Malezi na makuzi ndani ya familia aghalabu huzaa matunda yanayofanana na malezi na makuzi hayo. Ingawaje hutokea watoto wa familia moja wakawa na hulka tofauti sana, lakini mara nyingi ajabu familia huzaa watoto wanaofanana na mazingira ya familia hiyo, angalau kwa mambo makuu na ya msingi. Sehemu inayobaki ya hulka hujaziwa na makuzi nje ya familia: kijijini, mtaani, shuleni, kazini na kwingineko.
Inaaminika kwamba iko hatua ya uundwaji wa hulka ya binadamu (formative stage) ambayo ni ile miaka ya mwanzo kabisa ya maisha ya binadamu ambayo ikiisha kupita, hulka ya binadamu wengi inakuwa imekamilika kwa kiasi kikubwa, na baada ya hapo hakuna la msingi linalobadilika kwa mtu husika, labda tu impate dhoruba ya kumtikisa hadi ndani ya kokwa ya nafsi yake.
Bila shaka katika hili, kama ilivyo kwa masuala mengi mengine, hutokea tofauti hapa na pale, lakini kama wasemavyo wahenga, tofauti hizo ni zile zinazosaidia kuthibitisha desturi.
Binafsi naiamini nadharia hii kwa sababu kwa kuwaangalia watu niliowajua mwaka 1956, au mwaka 1960, au mwaka 1965, au mwaka 1970, au mwaka 1980, kila nikiwachunguza leo hii, natambua kwamba ni watu wale wale, hulka zao ni zile zile, hata kama wengine wana madevu yenye mvi, wengine wana vipara na wengine wamebakiza meno sita kinywani. Naamini nami pia naonekana vivyo.
Msemo kwamba mtoto umleavyo ndivyo akuavyo una mantiki ya kimsingi kabisa. Ni wachache tu huweza kuepukana na mihuri waliyobandikwa wakiwa wachanga na kujitengenezea hulka zilizo tofauti na jinsi walivyokuzwa.
Kitoto kilichozaliwa na kukuzwa katika familia ya watu katili mara nyingi kitakuwa ama na roho ya ukatili, kama njia ya kulipiza kisasi, ama na roho ya woga na utashi wakuepuka mahusiano na watu kwa kukumbuka, na kuogopa jinsi mahusiano yake na watu yalivyokuwa na mateso makubwa kiliyopata kikiwa bado kichanga.
Kitoto kilichozaliwa na kukuzwa katika familia yenye upendo aghalabu kitaonyesha upendo kwa watu wengine kitakaohusiana nao ukubwani kwa sababu kinakumbuka na kuelewa faida kilizopata katika familia kilimokulia. Na hivyo ndivyo yalivyo mazingira ya vitoto vingi vinavyozaliwa na kujaliwa kukua hadi utu uzima.
Ubishi umekuwapo kwa muda mrefu kuhusu ni kitu gani chenye athari kubwa kwa mtoto, kati ya maumbile na malezi (nature and nurture), kati ya chembechembe za asili za wazazi na mazingira ya malezi. Ubishi huo utaendelea kwa muda mrefu mwingine, kimsingi kwa sababu yote mawili yanachangia, lakini ukweli unaojulikana sasa ni kwamba maumbile yanajielekeza zaidi katika tabia ya umbo la kiwiliwili wakati malezi yanajikita katika tabia ya utu, roho, hulka, silika.
Sasa tukiangalie kitoto kilichozaliwa katika familia iliyojaa ufisadi. Kinapoanza kufumbua macho na kupata fahamu ya kwanza kinaona kimezungukwa na mazingira yasiyoeleweka, na kadri kinavyopata fahamu zaidi ndivyo kinavyojikuta hakipati uelewa wo wote juu ya mambo kinayoyaona.
Baba, mathalan, ana uwezo mkubwa wa fedha uliomwezesha kujenga kasri kama ya Mwinyi Fuad. Ana magari utadhani anaendesha tawi la International Motors. Ana watumishi wa ndani utafikiri kasri yake ni hoteli ya nyota kadhaa. Tusiseme chakula cha kumwaga, vinywaji vya kifahari kila aina, na aina zote za anasa.
Mama naye hajaachwa nyuma. Aliolewa na huyu mume wake, si kwa sababu ya mapenzi, bali kwa sababu bwana alitumia fedha 'kama fimbo' na kum-impress binti kwa mbwembwe za magari, starehe za kila aina, na binti, ambaye alikuwa kipusa kweli kweli katika ujana wake, akarubunika kumwacha mpenzi wake wa kweli na akaolewa na 'kizito'.
Sasa mama ana kila kitu: mavazi ya kifahari; vito vya dhahabu miguuni, shingoni hadi kidevuni, mikononi hadi kwenye viwiko; nywele za kubandika za gharama ya bajeti nzito, safari za Ulaya na Marekani kila akijihisi kachoka; matumizi ya fedha yasiyokuwa na mpaka….lakini kwa sababu ndoa hii si ya mapenzi bali ni ya biashara, mama atatafuta mapenzi nje ya ndoa, kama baba naye afanyavyo.
Kitoto kinaanza kukua na kwenda shule, na baada ya kujua hesabu za 'moja ongeza moja' kinaanza kujumlisha yote kinachoyaona nyumbani, lakini kila kikipiga hesabu, hesabu zinagoma. Baba ni mwajiriwa katika serikali au shirika la serikali. Kikitafutatafuta kitapata kujua ni kiasi gani analipwa kama haki yake ya mshahara na marupurupu.
Hesabu zisizokuwa na urari zinakichanganya kitoto hiki, na kutokana na utamaduni wetu, hakina ujasiri wa kumuuliza baba wala mama kuhusu utajiri huo usiokuwa na maelezo. Mwisho wa siku kinakuwa 'socialised' na kuikubali hali hiyo kuwa ndiyo ya kawaida.
Shule kinakosoma kitoto hicho ni shule teule, shule ya wana wa wakwasi watupu, na gharama zake ni kubwa kiasi kwamba baba na mama wa kawaida hawawezi kuimudu, lakini wazazi wa kitoto chetu wanaimudu kutokana na zile hesabu zetu zisizoingia akilini. Kikiwa na 'bahati' kitapelekwa ughaibuni, Kenya, Uganda au Ulaya kwa hesabu hizo hizo.
Katika shule hizo, kitoto chetu hakioni sababu ya kufanya kazi ya shule kwa bidii kwa sababu kimezoezwa kwamba 'mafanikio' katika maisha hayategemei sana kufanya kazi kwa bidii, kwa sababu wazazi wake wanayo 'mafanikio' ambayo hayakutokana na kazi bali ni matunda ya hesabu zile zile.
Ukifika wakati wa mitihani, msimu wa kupima kiwango cha kazi iliyofanyika, kitoto chetu kitatafuta njia ya mkato, kama kawaida ya maisha yake tangu awali. Baba au mama atatoa pesa na kitoto kitanunuliwa mtihani, katika soko lililojengeka nchini la kuuza na kununua mitihani. Mwisho wa mwaka kitatangazwa kwamba 'kimeshinda mitihani' na kitateuliwa kwenda shule ya juu.
'Ushindi' huo utashangiliwa kwa mbwembwe kubwa katika sherehe nono na kitapewa zawadi kem kem mbele ya halaiki iliyoitwa kukishangilia kitoto hicho kwa 'ushindi' kiliopata katika 'mitihani' ambayo hakikufanya. Ukiangalia jinsi nyuso za baba na mama zinavyoonyesha furaha kubwa katika sherehe hizo, unaweza kabisa kuamini kwamba kulikuwa na mitihani na kitoto hicho kiliifanya na kikashinda.
Hatimaye hata chuo kikuu kitakwenda, hapana taabu. Hakina haja ya kupata mkopo kama watoto wengine, kwani wazazi hawashindwi kulipa moja kwa moja, lakini kitaomba mkopo na kitaupata, kwa sababu kuna uwezekano kwamba mikopo inayotolewa huenda isilipwe.
Kinapotoka chuoni, kitapata ajira moja kwa moja, ama katika asasi za serikali ama katika mashirika ya binafsi au ya kimataifa yanayoendeshwa na wabia wa baba au mama katika mitandao ya ufisadi. Katika asasi hizo kitapandishwa madaraja bila kufanya kazi ya maana kutokana na mitandao hiyo hiyo walimo baba na mama.
Sasa kitoto chetu kimekuwa kijitu kizima, kimo ndani ya jamii na kinatamba kutokana na 'uwezo' mkubwa uliozaa 'mafanikio' makubwa tangu kilipoanza.
Kinaweza sasa kupata tamaa ya kuingia katika 'uongozi' na ikiwa hivyo , mambo ni yale: katika soko jingine lililojengeka na kuimarika nchini, soko la kura, kitanunua kura, ama kwa fedha zake ambazo kimekwisha kuiba au kwa kutumia fedha za baba na mama.
Huu ni mradi mwingine ambao matokeo yake yatasaidia familia kuendeleza 'mafanikio' yake, kama kawaida. Hatimaye, nani ajuaye? Nchi itashitukia siku moja kitoto chetu kinakwenda hadi juu kabisa katika 'uongozi' wa taifa.
Nacho kitaoa, au kitaozeshwa kwa binti au kijana wa familia inayofanana na ile yake (na kwa utaratibu ule ule) na mchakato unaanza upya.
Rev., wow..just wow! Nina mengi ya kusema na unajua jinsi hili jambo la Ndivyo Tulivyo lilivyo near and dear to my heart. Lakini hicho nilichonukuu hapo juu kimenigusa kidogo.
Ni kweli Watanzania ni mafisadi unique. Hata wale wasio mafisadi kwa matendo ni mafisadi wa kimawazo. Nitoe mfano mmoja tu.
Kuna huyu jamaa mwizi aliyefungwa jela huko UK, Mponjoli or whatever his name is. Juzi juzi tu hapa head negro in charge aka Invisible alianzisha mada inayomhusu huyo mwizi. Kulikuwa na range of opinions kuhusu matendo na hiyo tabia yake ya wizi.
Kilichonishangaza na kunisikitisha ni kwamba kuna watu ambao bado wanaona alichokuwa anakifanya (wizi) ni sawa. Wengine walikuwa waki condone. Tuliolaani hiyo tabia yake tulionekana tuna wivu na hayo ni maisha yake kwa hiyo hata tusilaani alichokuwa anakifanya.
Tendo la baadhi ya watu kuunga mkono alichokuwa anakifanya huyo jamaa kiliniacha kuhitimisha kuwa bado tuna safari ndefu sana dhidi ya hii vita ya mafisadi. Hatutaweza kupigana effectively hii vita kama bado kuna segment kubwa ya watu wenye attitudes za kifisadi.
We have a serious attitudinal problem here. Mpaka hapo tutakapobadilisha fikra zetu hii vita dhidi ya ufisadi haitafanikiwa. Na kubadilisha fikra jumuia za watu si kid's play na si kitu kinachotokea overnight. Inasononesha kwa kweli.
Rev., wow..just wow! Nina mengi ya kusema na unajua jinsi hili jambo la Ndivyo Tulivyo lilivyo near and dear to my heart. Lakini hicho nilichonukuu hapo juu kimenigusa kidogo.
Ni kweli Watanzania ni mafisadi unique. Hata wale wasio mafisadi kwa matendo ni mafisadi wa kimawazo. Nitoe mfano mmoja tu.
Kuna huyu jamaa mwizi aliyefungwa jela huko UK, Mponjoli or whatever his name is. Juzi juzi tu hapa head negro in charge aka Invisible alianzisha mada inayomhusu huyo mwizi. Kulikuwa na range of opinions kuhusu matendo na hiyo tabia yake ya wizi.
Kilichonishangaza na kunisikitisha ni kwamba kuna watu ambao bado wanaona alichokuwa anakifanya (wizi) ni sawa. Wengine walikuwa waki condone. Tuliolaani hiyo tabia yake tulionekana tuna wivu na hayo ni maisha yake kwa hiyo hata tusilaani alichokuwa anakifanya.
Tendo la baadhi ya watu kuunga mkono alichokuwa anakifanya huyo jamaa kiliniacha kuhitimisha kuwa bado tuna safari ndefu sana dhidi ya hii vita ya mafisadi. Hatutaweza kupigana effectively hii vita kama bado kuna segment kubwa ya watu wenye attitudes za kifisadi.
We have a serious attitudinal problem here. Mpaka hapo tutakapobadilisha fikra zetu hii vita dhidi ya ufisadi haitafanikiwa. Na kubadilisha fikra jumuia za watu si kid's play na si kitu kinachotokea overnight. Inasononesha kwa kweli.
Yebo Yebo,
Kuna ukweli ktk maelezo ya Jenerali lakini hatuwezi kurekebisha malezi ya mtu mwingine hata kidogo na bahati mbaya hao hao ndio huja na kuwa viongozi wetu. Ukichunguza kwa makini hoja ya Ulimwengu haina solution kwa mlalahoi zaidi ya kukubali matokeo ama kuomba Mungu wazazi hawa wenye tamaa watakuja badilika, jambo ambalo haliwezekani.. Kwa hiyo tujiandae kwa vizazi vyetu kuwa katika wakati mgumu zaidi.
Kusema kweli kulingana na historia ya nchi yetu, viongozi wetu wote walitoka familia maskini, kwani baada ya ASzimioa la Arusha, familia nyingi tajiri walitupwa chini kiutawala, hivyo ni wachache sana waliokulia katika maisha ya fridge Open. Kisha basi viongozi wote hawa walipigwa msasa wa Ujamaa Kigamboni wakawa waumini wa imani hiyo ya malezi.
Binafsi naamini kabisa WaTanzania tumepitia malezi hayo ya Ujamaa na pengine kosa kubwa lililofanyika ni kuwa strictly ktk imani ya Ujamaa. Kama vile mzazi unapokuwa mkali sana kwa mwanao kuhusiana na zinaa au anasa za dunia, sasa siku akija funguliwa na kuona yanayotokea nje huingia kwa pupa na kasi ya ajabu. Mfano mdogo na mzuri ni Wasomali wanapoingia nchi hizi.
Kwa uhakika Tanzania tulipitia kipindi kigumu sana cha Ujamaa, Tanzania ilikuwa nyumba ya gate kali sasa tulipokuja kuingia Ubepari, mtumeee haramu zote zilikuwa halali, ndio haya tunayoyaona leo. Lakini cha ajabu na kile kinacho nisukuma mimi kuamini kwamba NDIVYO TULIVYO, nazitazama nchi kama Kenya, Zimbabwe, Zambia. wao walikuwa Mabepari toka enzi lakini leo hii hawana tofauti na sisi tena wao ndio wameathirika zaidi, leo hii Kenya wanachimba visima vya maji mijini, wanavaa mitumba na kadhalika...Kenya ambayo tulikuwa tukiisikia tu kikifananishwa na London. Zimbawe ndio usiseme kabisa yaani duh!
Kwa hiyo, kweli malezi yanachangia makuzi ya mtoto sana tu lakini sidhani kama kuna malezi bora kwa mtoto zaidi kuzingatia Utamaduni wa wahusika na mazingira wanayoishi. Wahindi, Wachina na hata hao Wazungu malezi yao wote wanafuata tamaduni zao zaidi ya kuchukua malezi ya kuiga..Mtoto wa kihindi ni lazima ajifunze kwanza tamaduni za Kihindi kuanzia lugha, chakula, mavazi, heshima, mawasiliano na kadhalika..All of them have their own culture hata kama kuna wageni toka nje, wao hawasahau culture zao. Wazungu na Wachina wote ni katika mfumo huo huo..
Ukirudi kwa MIAFRIKA na hasa nchi za kusini mwa Jangwa (maskini kuliko zote) sisi sote tumeziacha culture zetu..Mkerewe mimi sitaki hata kusikia wala kuzungumza kikerewe, kumwamkua kaka ama dada yangu shikamoo ati ni utumwa, kwa sababu tu mzungu kasema hivyo.
Hata Nyerere alipokuja na Ujamaa ulikuwa wa kuchonga zaidi ya kufuata culture zetu. Mpango wa kuitana Ndugu badala ya Mheshimiwa, kuanzisha vijiji vya Ujamaa ulowachanganya watu wa makabila kuondoa Ukabila pasipo kufahamu kwamba kiswahili lugha iliyokubalika haina historia ya Utamaduni nyuma yake. hatukuwa na mwongozo wa Utamaduni nyuma ya makundi yote haya ila siasa za Ujamaa ambao hata Wachina waliufuata lakini bado walitukuza culture zao. Leo hii kila mtu hapendi kuzungumza kiswahili maanake sii lugha yake, ni sawa na mtoto alozaliwa Marekani umwambie yeye ni Mtanzania atakubishia hadi kesho!
Kwa hiyo hitimisho langu ni pale tulipopoteza Utamaduni wetu, makabila yote yanafanya vizuri nchini ni yale yaliyolinda tamaduni zao ndani ya Ujamaa. Unaona Wahaya, Wachagga na Wanyakyusa hadi kesho wanalinda tamaduni zao za kiasili na wanalindana sana ukilinganisha na Wasukuma au wanyamwezi ambao bado wanatukuza kiasi tamaduni zao lakini mikoa yao imevamiwa na wageni kiasi kwamba tamaduni hizo hazionekani.. watoto wao wanakua pasipo kuziona, kupitia malezi yenye kutukuza tamaduni hizo na matokeo yake ndio unayaona..
Mkuu niamini tazama nchi zote maskini, watu wake hawana utamaduni wao kabisa na huwezi jenga values kwa kutumia siasa ama sheria za bunge pasipo kutukuza tamaduni zinazo identify jamii hiyo.. Utamaduni ndio chanzo cha mawasiliano, mshikamano na hata kuaminiana...Ni katika tamaduni hizo ndipo kipimo cha malezi bora huweza pimwa.