Ugali wa na Vanilla? Serikali Yataka Kampuni za Unga Kufikiria Ubunifu Mpya

Ugali wa na Vanilla? Serikali Yataka Kampuni za Unga Kufikiria Ubunifu Mpya

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
3983.jpeg


Je, unaweza kula ugali wenye ladha ya strawberry au vanilla? Huenda wazo hilo likasikika geni kwa wengi, lakini Serikali ya Kenya sasa inazitaka kampuni za kusaga mahindi kufikiria uwezekano wa kubuni aina mpya za ugali ili kupanua soko la bidhaa hiyo nje ya nchi.

Katibu Mkuu katika Wizara ya Viwanda, Juma Mukwana, ametoa changamoto kwa kampuni za kusaga mahindi kuangalia uwezekano wa kutengeneza unga wa ugali wenye ladha mbalimbali, ikiwemo strawberry na vanilla, kama sehemu ya kukuza ubunifu katika sekta ya chakula.

Mukwana alitoa pendekezo hilo Oktoba 31, 2026, wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Kenya Millers Fortification Index Awards. Alieleza umuhimu wa wazalishaji kubuni bidhaa zinazoweza kuvutia masoko mapya, ikiwemo soko la kimataifa, huku wakizingatia mabadiliko ya mahitaji ya walaji.

Elewe pendekezo hilo halimaanishi kuwa Serikali tayari imeamuru uzalishaji wa ugali wa strawberry na vanilla. Hapana! Ni wito tu kwa kampuni za unga kuchunguza uwezekano wa kuboresha na kuongeza aina za bidhaa zinazotokana na mahindi.

Hata hivyo, ubunifu huo unakuja wakati sekta ya usagaji mahindi ikikabiliwa na changamoto nyingine. Beju Shah, mwenyekiti wa Chama cha Wasagaji wa Nafaka nchini (Cereals Millers Association), alikaribisha wito huo wa ubunifu lakini pia akazungumzia wasiwasi kuhusu upatikanaji wa akiba ya mahindi katika Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB), ambayo wasagaji hutegemea wakati wa upungufu wa mahindi.

Hali hiyo inaibua mjadala kuhusu vipaumbele vya sekta ya mahindi nchini: kwa upande mmoja, kuna haja ya kubuni bidhaa zitakazoweza kushindana katika masoko mapya; kwa upande mwingine, upatikanaji wa mahindi ya kutosha na uthabiti wa uzalishaji wa unga ni masuala yanayohitaji kupewa kipaumbele.

Je, ugali wa strawberry na vanilla unaweza kuwa bidhaa yenye soko nje ya Kenya na hata nyumbani au ni ubunifu ambao huenda ukawa mgumu kukubalika kwa walaji waliozoea ugali wa kawaida? Wewe ungependa kujaribu ugali wa ladha hizo?
 
Back
Top Bottom