Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Mchezaji wa Simba na timu ya taifa ya Uganda the Cranes Emanuel Okwi ameifungia timu yake ya taifa bao pekee dhidi ya Misri kwenye mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia 2018.
Mchezo huo wa Kundi E umechezwa leo August 31, 2017 kwenye uwanja wa Mandela jijini Kampala, Uganda imepata ushindi wa goli 1-0 matokeo ambayo yanaifanya the Cranes kuongoza Kundi lao wakati mapharao wakishuka hadi nafasi ya pili huku wakisubiri mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuchezwa wiki ijayo Alexandria, Misri.
Okwi alimiliki mpira vizuri kabla ya kumtungua kwa shuti la chinichini golikipa wa Misri Essam El-Hadary mwenye miaka 44 kuipa Uganda ushindi wa goli 1-0.
Misri walikaribia kusawazisha dakika ya 63 lakini mlinda lango wa Uganda Denis Onyango aliokoa mpira wa kichwa uliopigwa na mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah.
Kikosi cha Uganda: Onyango, Wadada, Walusimbi, Isinde, Juuko, Mawanda, Aucho, Okwi (Sserunkuma 88′), Miya (Kizito 75′), Nsibambi, Ochaya (Muleme 93′).
Kikosi cha Misri: El-Hadary, Abdel-Shafi, Hegazy, Rabia, Fathi, Hamed, Elneny, El-Said (Hamed 73′), Trezeguet (Sobhi 46′), Salah, Kahraba (Gamal 67′).
Kwa hisani ya Shaffih Dauda shaffihdauda.co.tz