Uganda: Askofu aitaka serikali kukata fungu la kumi katika mishahara ya waumini wao

Uganda: Askofu aitaka serikali kukata fungu la kumi katika mishahara ya waumini wao

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Askofu wa kanisa katoliki Uganda amewataka waumini kukatwa fungu la kumi kabla kulipwa mishahara.

Alilalamika kuwa wengi wa waumini hawalipi fungu la kumi kanisani Sawa na serikali ambayo inamtoza kila mmoja ushuru, viongozi wa kanisa katoliki nchini Uganda wameitaka serikali kukata fungu la kumi kwa mishahara ya waumini wao.

Askofu wa dayosisi ya kampala Dr. Cyprian Kizito ametoa pendekezo akitaka serikali ikate 10% kwa mshahara wa kila muumini na kuilekeza kwa kanisa.

Askofu Kizito amelalamika kuwa waumini si waaminifu katika kulipa mishahara.

Akizungumza Jumapili kanisani, askofu huyo ameleeza kuwa njia hiyo itafaa zaidi maana baadhi huweka sadaka zisizofaa kwenye makapu ya sadaka.

‘’ Mniunge mkono kwa pendekezo hili maana itatufaa. Je si mmechoka kuweka sadaka katika vikapu kila wakati?'' Aliuliza.

Kulingana naye, baadhi ya waumini wake wana mazoea ya kukwepa kila sadaka zinapokusanywa na hivyo kusitisha shughuli za kanisa kwa kukosa hela za kutosha.

''Kila tunapotaka kila mmoja kutoa fungu la kumu, watoa hutoa kile wanacho. Bibilia husema kuhusu kutoa 10% ya mali yako,''aliongezea.

Dr. Kizito ameitaka serikali kukata 10% ya mishahara kuepukana na tatizo la kuwaomba waumini kulipa fungu lakumi kila wiki.

Kwa upande mwingine, wengi wa viongozi wa makanisa wamekashifiwa vikali kwa kuwafilisisha waumini huku wao wakiishi maisha ya kifahari kwa sadaka zao.
 
Fungu la kumi ilikuwa sawa na income tax ya leo (na waliostahili kuipokea walikuwa ni Walawi - de facto political rulers of the Israelites). Kanisa la leo halina na halifanyi kazi za Walawi; kwa mantiki hiyo fungu la kumi hali-apply wakati na mazingira ya leo.
 
Nabadilisha dini embu waache huo upuuzi, kwani kanisa linawalipa hao waumini? Au wauumini wote wa hilo kanisa wana kazi?
 
Ujinga kweli fungu la kumi haijawahi kuwa sadaka ya kidini it was a national tax to israelites na ilikuwa lazima sasa kama wewe ni muisraeli haya toa fungu la kumi
NB sadaka yoyote ina elements 2
. -hiari
-moyo wa kupenda
Fungu la 10 linakosa sifa hizo
 
Heri wewe umeijua kweli hongera bro dini zinadanganya watu
Fungu la kumi ilikuwa sawa na income tax ya leo (na waliostahili kuipokea walikuwa ni Walawi - de facto political rulers of the Israelites). Kanisa la leo halina na halifanyi kazi za Walawi; kwa mantiki hiyo fungu la kumi hali-apply wakati na mazingira ya leo.
 
Fungu la kumi ilikuwa sawa na income tax ya leo (na waliostahili kuipokea walikuwa ni Walawi - de facto political rulers of the Israelites). Kanisa la leo halina na halifanyi kazi za Walawi; kwa mantiki hiyo fungu la kumi hali-apply wakati na mazingira ya leo.
Eehhh?
Mlawi wa leo ni nani?
 
Halafu alipomaliza akasema "tumsifu yesu kristu" waumini wakaitikia "amina". Huu utaratibu wa kutoruhusu maswali kwenye misa unawalinda sana hawa watu, wanatamba tu wanavyojisikia.
Ni kweli mkuu utaratibu ubadilike. Kanisani maswali yaulizwe. Kama mikutano ya serikali ya vyama taasisi n.k.
 
Uyo Askofu ana mapepo sio bure.
HAELEWI HATA MAANA YA SADAKA
 
Ujinga kweli fungu la kumi haijawahi kuwa sadaka ya kidini it was a national tax to israelites na ilikuwa lazima sasa kama wewe ni muisraeli haya toa fungu la kumi
NB sadaka yoyote ina elements 2
. -hiari
-moyo wa kupenda
Fungu la 10 linakosa sifa hizo
Elimu nzuri.
 
Back
Top Bottom