Uganda: Askofu avuliwa nafasi za kuhudumia Kanisa kutokana na kashfa ya kutoka kimapenzi na mke wa mtu

Uganda: Askofu avuliwa nafasi za kuhudumia Kanisa kutokana na kashfa ya kutoka kimapenzi na mke wa mtu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kanisa la Kianglikana nchini Uganda limemvua cheo aliyekuwa askofu mkuu wa kanisa hilo, Stanley Ntagali, na kusitisha utendaji wa majukumu ya uaskofu pamoja na kuzuiwa kuwakilisha kanisa hilo kabisa kwasababu ya madai ya uzinzi. Bwana Ntagali alistaafu mwaka jana Machi baada ya kuhudumu kwa miaka 43 kama askofu.

Katika taarifa ya Januari 13 kwenye tovuti ya kanisa la Kianglikana mrithi wake Dkt. Stephen Samuel Kaziimba, amesema Bwana Ntagali alijihusisha na mahusiano na mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye ndoa na hilo alilifahamu.

"Alisaliti ofisi ya Askofu, kiapo alichokula wakati wa kuapishwa, na maadili mema aliyotekeleza kwa kujitolea," Dkt. Kaziimba ameongeza.

Dkt. Kaziimba amesema kanisa la Uganda limejitolea kuwa na uwazi pamoja na kutoa uangalinzi wa uchungaji kwa wale ambao wameathirika na hali hiyo na kutoa wito wa maombi kwa wanandoa wote, kuomba msahama na maridhiano.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Amerika Kaskazini, Foley Beach, pia naye alitoa taarifa yake akionesha kusikitishwa na tukio hilo.

"Stanley ni ndugu katika Yesu ambaye nimekuwa nikifurahia kufanya kazi naye kwa miaka mingi na inanisikitisha sana kusikia mambo hayo. Ni maombi yangu mbele ya Mungu kuwa ataendelea na njia ya kuomba msamaha na kwamba Mungu atafariji wote walioathirika na dhambi hii."

Stanley Ntagali, aliyekuwa Askofu hakupatikana kutoa maoni yake kuhusiana na kusimamishwa uaskofu.

Lakini raia wengi wa Uganda watamkumbuka kwa kuzungumzia kile ambacho alikiona kama maadili mabaya nchini humo, 2019 aliyenukuliwa na gazeti la eneo akishauri watu “kudhibiti matamanio yao ya kingono”.

Kanisa la Kianglikana nchini Uganda limekadiriwa kuwa na wafuasi milioni 13.
 
Hii kitu hii
Uvumulivu umeishinda nafsi askofu akaona yanini kula kwa macho mtoto mzuri hivi, akaamua kuruka kwa reverse engineering amri ya 6
 

Attachments

  • IMG_20210120_231239_284.jpg
    IMG_20210120_231239_284.jpg
    65 KB · Views: 1
Si ndio hili kanisa walaiohalalisha ndoa Za Mashoga kama walishapoteza muelekeo.
 
Mke wa mtu!
Kwanini lakini?
Mbona wapo wengi
Unamaanisha wapo wengi wake za watu sio? Mi ndo nashangaa roho mbaya ya kanisa letu. Yaani kuna wake za watu wengi tu, lakini Baba Askofu kajisevia mmoja tu ndo imekuwa nongwa.
 
Unamaanisha wapo wengi wake za watu sio? Mi ndo nashangaa roho mbaya ya kanisa letu. Yaani kuna wake za watu wengi tu, lakini Baba Askofu kajisevia mmoja tu ndo imekuwa nongwa.
Wewe mchache wa lugha
 
Back
Top Bottom