Uganda kuanza kuunda magari 2018

Uganda kuanza kuunda magari 2018

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Uganda itaanza utengenezaji wa magari mwaka wa 2018, imetangaza serikali ya Uganda. Profesa Sandy Stevens, ambaye ni afisa mkuu wa mradi unaopanga kuanzisha uundaji wa magari hayo, anasema ifikap mwaka huo kila kitu kitakuwa tayari kuanza kazi hiyo.

Mhandisi mkuu wa mradi huo Isaac Musasizi anasema watahitaji dola za kimarekani milioni 350, kupanga kila kitu pamoja na kujenga kiwanda cha uundaji wa magari hayo. Anasema pia magari yakakayo kuwa yakiundwa na nchi hiyo, ni sawa na lile lililozinduliwa na rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni, mwaka wa 2011.

Waziri wa biashara na viwanda nchini humo Amelia Kyambadde, anasema kuanza kwa mradi huo wa uundaji magari ni moja wapo ya mipango ya serikali yake, ya kuipa nchi hiyo maendeleo ya kiuchumi. Hata hivyo serikali ya Uganda inasema itashirikiana na kampuni moja ya Kimataifa, ili kuhakikisha magari yao yanatambulika kimataifa pindi tu yatakapoanza kuuundwa.
 
Watutishe bana, sisi tulishatengeneza magari kibao ya nyumbu, hamyaonagi sabasaba?! kila mwaka wale jamaa wana budget yao kwa ajili ya uvumbuzi mbalimbali, Baba Ritz ondoa shaka uko mbele kaka mkubwa, achana na waganda kwanza gugari gwenyewe gubayaaa!....
kiira.gif
 
nchi ya kisanii sana hii,Kenya wanazalisha yao yanaitwa MOBIUS TRUCK yako kama landover ,Bei ni KSH 900,000/=

Sisi bado kwanza tunafanya maonesho! mpaka Rwanda watatengeneza ndege sisi bado tunaagiza baiskei!
mobius-2-876.jpg
 
Sisi bado kwanza tunafanya maonesho! mpaka Rwanda watatengeneza ndege sisi bado tunaagiza baiskei!
View attachment 171272

Kagari nimekapenda haka ila comments zilivyokaa zimenifanya nishindwe kuelewa hii gari ni imetengenezwa Kenya, Tanzania au Rwanda? Kwa hisani yako tu ndugu, hii ni gari gani na imetengenezwa wapi?
 
Kagari nimekapenda haka ila comments zilivyokaa zimenifanya nishindwe kuelewa hii gari ni imetengenezwa Kenya, Tanzania au Rwanda? Kwa hisani yako tu ndugu, hii ni gari gani na imetengenezwa wapi?
mkuu hii gari imetengenezwa Kenya,na ni purposely kwa rough terrain,Usishangae kampuni za kitalii hata za Tanzania wakakimbilia kununua hizi,maana bei ni cheap tofauti na landcruser,na hizi ni mpya kabisa unanunua ni sawa na 0 millage,Ksh 900,000/= ni kama Tsh Mil 18hivi kwa gari mpya na spear ni guaranteed zipo,kwanini wasiuze?
 
iv nyumbu tulitengeneza au tuliasembo vitu mana kuliunda gari from scratch cdhan na nahisi ata majiran zetu ni ivo ivo tu engine wanaagiza gearbox wanaagiza piston afu wana tengeza bodi,sasa apo umetengeza gari,umeunda au umeuganisha vfaa upate gari??

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kagari nimekapenda haka ila comments zilivyokaa zimenifanya nishindwe kuelewa hii gari ni imetengenezwa Kenya, Tanzania au Rwanda? Kwa hisani yako tu ndugu, hii ni gari gani na imetengenezwa wapi?

MOBIUS hiyo ya wakenya.
 
Waganda wanaunda mkuu, wanatengeneza from scratch!
 
Kagari nimekapenda haka ila comments zilivyokaa zimenifanya nishindwe kuelewa hii gari ni imetengenezwa Kenya, Tanzania au Rwanda? Kwa hisani yako tu ndugu, hii ni gari gani na imetengenezwa wapi?
Mobius, ni ya Kenya hii...
 
Back
Top Bottom