Fene
JF-Expert Member
- May 4, 2021
- 2,945
- 4,827
Mkuu wa Majeshi ya Uganda na mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amezua taharuki mpya ya Kidiplomasia baada ya kutoa maonyo makali dhidi ya Uturuki kutokana na uhusiano unaozidi kuwa mbaya kati ya nchi hizo mbili.
Katika msururu wa machapisho yake kwenye X (zamani Twitter), Kainerugaba alidai Uganda inajiandaa kukata uhusiano wote wa
Kidiplomasia na Uturuki ndani ya siku 30, huku pia akipendekeza kuwa Shirika la Ndege la Uturuki kuzuiwa kufanya kazi Uganda.
Matamshi yake ambayo yanatajwa sana kuwa ya uchochezi, pia yamechukua msimamo mkali wa kuiunga mkono Israel, unaoambatana na matamshi ya kidini na matamko kwamba Uganda inaweza kupeleka Wanajeshi kuunga mkono Israel.
Kainerugaba amezidisha mvutano mtandaoni kupitia machapisho ya kichokozi yanayolenga Iran, akipuuzilia mbali uwezo wa Kijeshi wa nchi hiyo na kutaka ukuu wa kidini katika mashambulizi yake.
Kauli hizo zimevuta hisia katika eneo lote, na kuibua maswali mapya kuhusu mwelekeo wa sera ya kigeni ya Uganda na kama diplomasia sasa inaendeshwa kupitia mitandao ya kijamii.