Wakimuenzi ni haki yao.Hata jambazi muuaji na katili sana,kama anajali familia yake(au hata asipojali sana), mabaya yakimkuta, lazima hatakosa wapendwa wa kumlilia na hata kusema 'jinsi alivyokuwa mzuri na mwema kwa walio karibu naye'.
Hakuna tatizo na mema yake.Ila mema na mazuri yake,hayakuahalalisha kutenda aliyoyatenda dhidi ya Tz.Akachapwa kisawa sawa kabisa.Pia propaganda kabla,wakati na baada ya vita yaweza kuwa na kamchango na kwenye vita ni jambo la kawaida,ila,ukweli alivamia Tz.
Cha msingi, alifanya kosa kuivamia Tanzania na kuchukua ardhi ya Tz na askari wake kufanya ukatili ndani ya waTz.Hatimae akakipata kilichomstahili na alistahili.
Ni dhahiri hakosi mema aliyofanya nchini mwake, japo hata kwa wachache. Na si ajabu ni kweli kabisa baadhi ya watu walifanya uovu na kuishia kumchafulia yeye kama kiongozi.Mfano kina Malyamungu,Bob Astles,na makamu wake Idris.Lakini,yeye kama kiongozi alipaswa kusimamia anaowaongoza na 'kuashiria' toka awali kuwa,vitendo vya kikatili hawezi kuvikubali wala kuvivumilia.Waliokuwa chini yake,ama wasingetenda kabisa au vingekuwa vichache sana,tena kwa kificho.
Yakitokea mabaya chini ya uongozi wa anayeongoza,kuwajibika (ama kuwajibishwa kwa namna fulani) ni kawaida.
Tunae Rais mstaafu aliyekuwa mwungwana sana na kuamua kuwajibika alipokuwa waziri kwa makosa yaliyotendwa na waliokuwa chini yake.Huu ni mfano tu.
Idi Amin with only a handful of his children