#COVID19 Uganda kumuenzi iddi amin je historia ilipindishwa?

Idd amin dada mla nyama za watu..
Muua mtoto wake mwenyewe.
Kawamwaga watu mto wa mamba.
Kaua ndugu zetu wa kagera na mabomu yake.

Huyu boya tulitakiwa kumdaka tukamfunga bongo hapa hapa akawa analima na kuchunga ng'ombe.
Duh anakula nyama za watu?? Hizi propaganda za Nyerere naona zilibrainwash sana akili za watanganyika.
 
Mimi Nina ndugu waganda hakuna hata mmoja anayemlaani IDD amini ni huku tu ndiyo kuna sumu.
 
Ukiwa Uganda usimseme vibaya Idd Amin Dada (aliitwa Dada kwa sababu tulipokuwa naye mafunzo ya kijeshi Kenya, alipenda sana kutoroka kambini na akirejea alikuwa lazima aje na mwanamke, akiulizwa anasema huyu Dada yangu, so jina akawa Idd Amin Dada). Pia kuna generation ya waganda hawapendi kiswahili kwa sababu majeshi ya Amin na ya Tz yalitumia kiswahili kubaka/kuiba etc,
 
Nilishangaa sana kuna kipindi nilikuwa Kampala, kuna jamaa mmoja Mganda anamsifia Idi Amin sana kwamba alikuwa anawawezesha wazalendo.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Kwenye aya ya mwisho pale "kuikanyaga kanyaga bendera ya CCM" ingekuwa imetokea miaka ya hivi karibuni hata Tanzania kungekuwa na vita (sisimua dhidi ya washangiliaji) vya wenyewe kwa wenyewe.
Kulikuwa na chama kimoja enzi hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu kubwa ya wilaya ya misenyi ni Uganda hata kule wanaongea kiganda
aMipaka iliwekwa na wakoloni.ili baki hiohio kufanana lugha sio kigezo cha kuwa was huko.

Kwa logic yako kaskazini ya msumbiji wa kuwa wanaongea kimakonde basi ni Tanzania

Au makabila za Zambia ya juu yanayoongea kinyakyusa tuseme no Tanzania ...
Au nyanza province in Kenya kuria district kwa kuwa wanaongea kikurya basi tuassume ni watanzania au vice versa. That is madness the only thing that matters ni borders na amin Ali invade borders hio ni act of war hakuna excuse hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali je hakuvamia Tanzania ?

Na kama alivamia mlitakaje nyie wapambe wake tumuache huku askari wake wakibaka mama zetu,Dada zetu pale kagera na kuua watu wasiokuwa na hatia ??

Maana mnaongea tu as if alikuwa MTU mwema sanaa
Amin Ali kuwa mpuuzi mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muwe mnatumia walau muda wenu kidogo kutafuta ukweli wa mambo badala ya kuziachia akili zenu kulishwa ujinga na kuamini ujinga huo ndiyo ukweli. Haya uliyoandika ni upuuzi mtupu na msomi yeyote hawezi kuandika upuuzi huu.
Wewe mpambe tupe historia ya amin unayoifahamu??

Yani watu mnajidai mnaakili nyingi sana kumbe hamna kitu.

Fact ni kwamba mpuuzi amin alituvamia kijeshi,akaaharibu miundo mbinu yetu, askari wake walifanya ubakaji wa mama zetu na Dada zetu wa kagera na Dawa yake ilikuwa moja tu kumtoaa madarakani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni wale kikundi cha kidini wapinga nyerere mnajulikana mbona.MTU kama wewe kuwekwa kizuizini ni haki sababu upo radhi kumsaidia adui wa nchi yako kwa vigezo vya dini au ujinga wenu mwengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hiii ilikuwa kwetu TU kama angekuwa mla nyama za watu na muuwa wapinzani hakika Amin angepelekwa mahakama za haki ya binadamu ! why mpaka leo Amini ana kesi popote pale? nyerere alitulisha matango pori kuwa Amini anawapiga misumari wahasimu wake n.k
 
Duh anakula nyama za watu?? Hizi propaganda za Nyerere naona zilibrainwash sana akili za watanganyika.
Hivi vitu vingine ilikuwa ni kuwapa watu morale ya kivita tu

Hamna kitabu cha historia serious kabisa kimeandika amin Ali kuwa anakula nyama za watu.

Mkuu kama umeenda jeshi hats jkt tu nadhani utaona kuna nyimbobhazina maana ila ni kuboost morale tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…