UGANDA: Mama ajifungua mapacha wenye Baba tofauti, Naibu Waziri wa Afya (Tanzania) atolea ufafanuzi

UGANDA: Mama ajifungua mapacha wenye Baba tofauti, Naibu Waziri wa Afya (Tanzania) atolea ufafanuzi

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
1.jpg

Katika hali ya kushangaza huko nchini Uganda, wanaume wawili na watu wengine wamejikuta kwenye mshangao baada ya kukuta wote wawili ni baba wazazi wa watoto wawili mapacha.

Inaelezwa kuwa wanaume hao waliingia kwenye mgogoro siku za hivi karibuni kila mtu aking’ang’ania kuwa baba mzazi wa mapacha hao, na ndipo walipoamua kwenda hospitali ili kupima kipimo cha DNA.

Hatahivyo matokea ya daktari yalionesha kuwa wanaume hao wote wawili ni baba halali wa mtoto mmoja wa mapacha hao, yaani kila mmoja ana mtoto mmoja kati ya mapacha hao.

Inaeelezwa kuwa wanaume hao Joseph Baseka Sengendo, 25, na Patrick Ssegane, 30, wamezaa na Rashida Nakabugo, ambapo Sengendo anatajwa kuwa mume wa ndoa wa mwanamke huyo.

Wanaume hao wanasemekana kuwa ni ndugu.

Chanzo: Kijukuu cha Bibi


--------------

Ufafanuzi wa kitaalamu kutoka kwa Dkt. Faustine Ndugulile - Naibu Waziri wa Afya, Tanzania.

Ndglile.jpg

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amefafanua uwezekano wa kisayansi kwa mwanamke mmoja kubeba ujauzito mapacha kutoka kwa wanaume wawili tofauti

Amesema jambo hilo hutokea pale mwanamke anapotoa mayai mawili tofauti katika mzunguko huo mmoja ambayo yanarutubishwa (fertilized) na mbegu za wanaume 2 tofauti. Kisayansi inaitwa Super-fecundation.

Ndugulile ambaye ni daktari kitaaluma, ametoa ufafanuzi huo kutokana na habari kuhusu mwanamke mmoja nchini Uganda kuingia kwenye mgogoro wa kindoa na mumewe baada ya wanaume wawili (mumewe na mdogo wake) kujikuta wote wawili ni baba wazazi halali wa watoto wawili mapacha, kila mmoja akiwa na mtoto mmoja baada ya kupimwa DNA.

"Kisayansi inawezekana. Inatokea pale mwanamke anatoa mayai mawili tofauti katika mzunguko huo mmoja ambayo yanakuwa-fertilized na mbegu za wanaume wawili tofauti. Kisayansi inaitwa superfecundation" ameeleza Dkt. Ndugulile kupitia ukurasa wake wa Twitter.
 
Ngumu kumeza, huo uchunguzi ufanywe upya kwenye kituo cha kuaminika, dah hapa sasa ni ugomvi kwa kwenda mbele.
 
Ngekua jamaa ngeachana na
Huyo mke mazima
 
Heteropaternal superfecundation. Hamna cha ajabu hapa.... Kafanya mapenzi na wanaume wawili katika kipindi cha muda mfupi, na mwezi huo mayai mawili yaliiva kwa wakati mmoja.
 
Nitaria shaka hiyo DNA, hao ni mapacha waliofanana au siyo.
Madaktar mje kutusaidia hiyo mechanism nahis huyo mme wa ndoa watoto siyo wake ili kuepusha mgogoro wakatoa matokeo hayo.

Ila wanawake ni hatari sana kachepuka kutafuta mimba ilipogongwa kurudi home kamlazimisha mmeo kufanya tendo la ndoa ili mimba ionekane yake.
 
Dah huyu mwanamke ni bora angamkana tu huyo wa nje mzigo uwe wa mumewe
 
Back
Top Bottom