Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwanamke mmoja wa Uganda aitwaye Fortunate Kyarikunda, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kushindwa kumlipa Mwanaume aliyekataa kuolewa nae, fidia ya zaidi ya shilingi milioni 14 za Uganda (Tsh. milioni 9.6) pesa ambazo Mwanaume huyo amedai kuzitumia kumlipia ada Mchumba huyo aliyepindua meza dakika za jioni.
Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkuu Wilayani Rukungiri mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kubainika kuwa Kyarikunda alikiuka amri ya Mahakama iliyomtaka kumlipa Richard Tumwiine ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi fedha alizotumia kumlipia masomo kwa matarajio ya ndoa.
Chanzo cha kesi hiyo ni uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Kanungu uliotolewa Januari 2023, uliomtaka Kyarikunda kulipa zaidi ya shilingi milioni 9 kama gharama za masomo pamoja na shilingi milioni moja kama fidia ya usumbufu na maumivu ya kisaikolojia aliyopata Tumwiine.
Hata hivyo, Kyarikunda alipoteza kesi hiyo baada ya kushindwa kufika Mahakamani au kuwasilisha utetezi wake ambapo badala ya kutekeleza hukumu alifungua maombi ya kutaka hukumu ifutwe akidai hakuwahi kupokea wito wa Mahakama, ombi ambalo haya hivyo lilikataliwa.
Baadaye alijaribu tena kufungua kesi nyingine katika Mahakama tofauti akitaka hukumu hiyo hiyo ifutwe kwa hoja zilezile lakini juhudi zake ziligonga mwamba ambapo licha ya maamuzi ya Mahakama, Kyarikunda aliendelea kupuuza kulipa fedha hizo jambo lililosababisha kiasi cha deni kuongezeka hadi kuvuka shilingi milioni 14.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Rukungiri, Dinah Nekesa, aliamuru Kyarikunda apelekwe katika gereza la Serikali la Rukungiri kutumikia kifungo kisichozidi miezi sita au hadi pale atakapolipa deni lote.