Halafu wamesahau kuongelea reli ya Kampala-Port Bell! Wacha Magufuli afanye mambo yake huku upanuzi wa viwanja vya ndege vya Tanga na Mwanza, upanuzi wa Bandari za Tanga na Dar, maboresho ya reli ya kati na ile ya Tanga-Arusha huku meli mbili za kubeba mabehewa zikiboreshwa na nyingine mpya kuanza kuundwa na Wakorea! Mwenye macho haambiwi ona! Jamaa anataka sana biashara ya mizigo ya Uganda na ataipora kutoka Kenya.
Mimi huwa wakati fulani ninakaa na ninaifikiria sana Kenya ndani ya miaka 5 ijayo itakuwa wapi, unajua Magufuli ni mtu hatari sana, kama Kenya hawatachukua tahafhari uchumi wa Kenya unaweza kuwa kwenye hali mbaya sana, lazima Kenya washituka muda huu na waanze kumfanya Magufuli kuwa rafiki yao ili washirikiane badala ya kumuweka mbali, wanampa nafasi ya kuwazunguka kama anavyofanya sasa hivi, ngoja tufanye analysis fupi sana,
1)Uchumi wa Kenya unashikiliwa na sector zifuatazo; Kilimo, utalii, financial services, manufacturing, construction, construction, transportation and logistics.
2)Utalii ndiyo hivyo tena, sina sababu ya kuelezea unakaribia kufa, mwaka huu Kenya ikifikisha $500m itakuwa ni bahati sana
3)Kilimo kinaendelea kuwa duni kila mwaka, ukame na serikali kupuuzia miradi ya kilimo, migogoro ya ardhi, na matumizi, insecurity vinadidimiza uzalishaji.
4)Manufacturing sector, umezidiwa na bidhaa toka china na India, huku Magufuli anakuja juu sana kujenga viwanda, ambavyo vitaongeza ushindani kwa sababu gharama ya uzalishaji Tanzania ipo chini sana ukilinganisha na Kenya.
5)Transportation and logistic, Kenya haitoweza kupambana na Tanzania katika hili, imejenga reli ya ghali sana, na gharama za uendeshaji pia zitakuwa juu kutokana na kwamba ni diesel engine, hivyo kufanya gharama za kusafirisha kuwa juu ukilinganisha na Tanzania