I like the fact that baada ya Kenya na Uganda kufungua mipaka Yao (A Kenyan only needs an ID to cross the border) Uganda for the first time sold more goods than Kenya .... Kina watu wengine kutoka kusini mwa nchi yetu wamekua wakidanganywa Kwa propaganda za CCM Kwa zaidi ya miongo miwili kua ukiwaachia wakenya waingie nchi Yao watachukua biashara zao, mashamba Yao Hadi watawashikisha tabia zao ..etc Mimi sijawahi ona nchi ambayo iko green na inamashamba yenye rotuba kuliko Uganda hapa EAC, walifungulia wakenya mipaka na Sisi tukawafungulia roho Safi, na sasa wamefaidi zaidi kutuliko Yani trade yetu na Uganda iko zaidi ya $1B !
Imagine kama ingekua trade Naina ya Tz na UG pia iko $1B, Kenya na Tz =$1.5B... etc.... EAC ingekua haihitajii kutegemea nchi za EU au Asia au Marekani, ingekua Kenya ina export vikombe vya glasi UG na kununua Vikombe vya plastic kutoka huko, Tz ingekua ina export transformer zote zinazotumika Kenya kwa umeme exclusively na Kenya ingekua ina export meter na nyaya zote za umeme..etc Lakini vile tulivyo mazuzu tunawachia China aje achukue malighafi huku Africa akatengeneze bidhaa alafu aje atuuzie wakati Sisi bado tunabishana kuhusu maziwa na mahindi!
Juzi niliskia kulia ndani ya supermarket nilipoona kibao cha kukandia chapati cha plastic chenye kimeandikwa 'made in China!) Yani hata wajasirimali wanaochonga vibao na chopping board kutumia mbao na mikono Yao miwili pia wanauliwa biashara zao na vibao vinavyotengenezwa na mashini huko China!
------
Anyway, Kwa wale wanaosema uchumi wa Kenya umezorota ndo maana Ug ime export zaidi, Kenya wamenza ku export zaidi Kwa nchi zengine Africa kwahivyo tulipata masoko mengine kuuza bidhaa ambazo Uganda imenza kujitengezea wenyewe...good for UG sasa wamenza kujitegemea, kitambo ilikua hata toothpaste hawatengenezi.. ndani ya COMESA kina nchi nyingi Sana ambazo haijafika level ya Uganda ambazo tunazidi kuwauzia macuta ya kupikia, sabuni, siagi.etc