Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,298
- 7,612
Ukistaajabu ya Musa utashanga ya mengi katika hali ya kushangaza polisi kwenye wilaya ya Moroto kaskazini mwa Uganda wametangaza kukamata mtu yoyote atakayekutwa akinunua chapati zaidi ya tano kwa mara moja.
Chanzo cha kamata kamata hiyo ni kutokana wakazi wengi wa wilayani humo kutumika kupeleka chakula kwa baadhi ya wezi wa mifugo kwenye wilaya hiyo na kuwaficha majumbani mwao.
Akizungumza na wanahabari msemaji wa jeshi la polisi wilayani humo Micheal Longole, amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya wizi wilayani humo.
“Kwanzia sasa tutakamata na kumhoji mtu yoyote atakaye nunua chapati zaidi ya tano kwa lengo la kujua ni kwa nini ana nunua kiasi hicho cha chapati, tumepata taarifa kuwa watu wengi wananunua na kupeleka kwa waharifu waliojificha maporini” amesema Longole.