Mtapenda
JF-Expert Member
- Sep 20, 2011
- 1,115
- 2,063
Waziri wa Uganda akinukuliwa
"Ikiwa hutumii akili alizokupa Mwenyezi Mungu, usimlaumu unaposalia kuwa maskini. Jitahidi kuushinda umaskini kwa sababu kuwa tajiri ni utukufu,"
Gazeti la New Vision la Uganda linamnukuu kiongozi mmoja mkuu nchini Uganda akisema kuwa
"maskini hawataenda mbinguni kwa sababu wanamtukana Mungu kwa njia ya maombolezo na shutuma kila siku".
Waziri wa Masuala ya ndani Kahinda Otafiire aliripotiwa kutoa maoni hayo katika hafla ya shule huko Kyenjojo, magharibi mwa Uganda, huku akiwaambia wanafunzi kuwa kufanya kazi kwa bidii ndio dawa ya umaskini.
Ukosefu wa ajira kwa vijana ni mkubwa nchini Uganda, ambayo ina moja ya idadi ya watu changa zaidi duniani ikiwa na 75% ya raia chini ya umri wa miaka 30.
Unazungumziaje hili ?
Je anapingana na biblia inayosema ni vigumu tajiri kwenda mbinguni kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!?
Source: BBC Swahili Instagram