Uganda yafuta sheria iliyokuwa inapinga ndoa za jinsia moja

fungi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014
Posts
2,539
Reaction score
4,672
Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria hiyo ambayo ilisababisha mataifa ya Magharibi kuinyima Uganda msaada

Wanaume wanaounga mkono mapenzi ya jinsia moja Uganda

Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada.

Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana sio tu Uganda bali kote duniani ambapo mataifa ya Magharibi yalilazimika kuingilia kati.

Mahakama ilisema kuwa mswada huo kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kupitisha mswada na kwa hivyo ni kinyume na sheria.

Baadhi ya waandamanaji waliounga mkono serikali kwa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, tayari vilikuwa vimeharamishwa Uganda , lakini sheria hiyo mpya pia iliharamisha hatua zozote za kueneza mapenzi ya jinsia moja na wakati huu hata kuwajumuisha wanawake wasagaji kama sehemu ya wapenzi wa jinsia moja.

Mataifa kadhaa ya Magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa.

SOURCE: BBC
 
Museveni asingeweza kufuta hii sheria kwa shinikizo la wafadhiri moja kwa moja, ingekuwa ni aibu kwake. Sasa nadhani watasema ni mfumo wa sheria umeamua, sio shinikizo la wafadhiri. Kelele nyingi, mwishowe yanaishia hapa. Fedha ya wafadhiri tamu bwana.

Mie binafsi, japo sikubaliani na suala la ushoga, sielwei kwa nini viongozi wa Afrika wanalivalia njuga jambo hili, wakati kuna mambo mwengi tu ya maana zaidi ya ushoga ambayo tunayapaswa kuelekeza nguvu zetu nyingi na kuyatungia sheria kama ambavyo wamepigia kelele ushoga. Watu wamesimamie kidete ushoga utafikiri wameambiwa mashoga wanawataka wao au watalazimishwa kuwahudumia mashoga. Kama mtu anataka kuwa shoga ni juu yake, achana naye na isiwe kisa cha kugombana na wafadhiri bila sababu za maana.
 
Unacheza na power za wadhamini?
Hadi hapa bongo sheria ya watu kunanilihiwa inakuja kaa chonjo na implementation of new world orders
Kitu chakufanya ni kumkataza tu mwanao atapokua anacheza atunze nanihii yake wasije wakamnonino
 
...ina maana mashoga wa Uganda sasa hivi wataendelea kuzibuliwa mifereji ya maji taka yao kama kawaida?
 
Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada.

Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana sio tu Uganda bali kote duniani ambapo mataifa ya Magharibi yalilazimika kuingilia kati.

Mahakama ilisema kuwa mswada huo kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kupitisha mswada na kwa hivyo ni kinyume na sheria.

Baadhi ya waandamanaji waliounga mkono serikali kwa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, tayari vilikuwa vimeharamishwa Uganda , lakini sheria hiyo mpya pia iliharamisha hatua zozote za kueneza mapenzi ya jinsia moja na wakati huu hata kuwajumuisha wanawake wasagaji kama sehemu ya wapenzi wa jinsia moja.

Mataifa kadhaa ya Magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa.

Chanzo.
BBC SWAHILI
 
Haya sasa......misaada kurudishwa ug...
 
Mahakama ya kikatiba nchini Uganda yafuta sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja iliyosainiwa na Rais Yoweri Museven february yadai si halali.
 
Wanaume wanaounga mkono mapenzi ya jinsia moja Uganda.

source: BBC
 
hata mimi nimeshangaa kweli waafrica hatuwezi kujiendesha bila msaada.!
 
Baadhi ya waandamanaji waliounga mkono serikali kwa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja

Source:BBC
 
Utwa na utwana kamwe hautamalizika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…