Uganda yakabiliana na Mlipuko wa Ebola, Watu 100+ wamewekwa Quarantine

Uganda yakabiliana na Mlipuko wa Ebola, Watu 100+ wamewekwa Quarantine

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mamlaka nchini Uganda zimesema kuwa zaidi ya watu 100 wamewekwa 'quarantine' wakati maafisa wa afya wakipambana kudhibiti mripuko wa nadra wa ugonjwa wa Ebola, unaohusishwa na kirusi cha aina ya Bundibugyo.

Watu hao wanachunguzwa kwenye eneo ambalo halikutajwa, huku jopo la madaktari likifuatilia kwa karibu kuona kama watapata dalili zozote za maambukizi. Hata hivyo, viongozi wanasisitiza kuwa hali iko salama na inadhibitiwa, wakisema uzoefu wa Uganda katika kukabili milipuko iliyopita umeongeza uwezo wao wa kukabiliana na hali hii.

Alan Kasujja, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Habari cha Uganda na msemaji wa Kamati ya Kudhibiti Ebola, amesema nchi hiyo inawategemea wahudumu wa afya wenye uzoefu mkubwa ili kukabiliana na hali hiyo.

“Kitu kikubwa mnachopaswa kujua kwa sasa ni kwamba zaidi ya watu 100 wameshabainishwa na wamewekwa karantini, na wanahudumiwa na wataalamu wa afya wenye uzoefu mkubwa sana,” alisema Kasujja."

Aliongeza kuwa huko nyuma Uganda imeweza kudhibiti vizuri milipuko ya Ebola, UVIKO-19, na virusi vya Ukimwi (VVU), na akawataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata miongozo ya afya.

Hatua hizi zinakuja huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likionya kuhusu "kasi na ukubwa" wa mripuko wa Ebola unaozidi kuwa mbaya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maafisa nchini Kongo wanasema kuwa hadi sasa takriban watu 131 wamefariki, na zaidi ya visa 500 vinavyoshukiwa vimeripotiwa, hali inayozua hofu kuwa kirusi hicho kinaweza kusambaa zaidi katika ukanda huo.

1779258952253.png

Soma pia TAHADHARI: Ugonjwa wa Ebola Walipuka DRC na Uganda, WHO Yatangaza Hali ya Hatari (PHEIC)


Source: African news
 
Back
Top Bottom