Uganda yalaani Bunge la EU kutaka kusitishwa kwa ujenzi wa Bomba la Mafuta

ichumu lya

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2016
Posts
2,651
Reaction score
2,790
Bunge la Uganda limelaani azimio la bunge la Umoja wa Ulaya linalozitaka Uganda na Tanzania kusitisha maendeleo ya miradi yao ya mafuta na gesi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika kikao cha Alhamisi, Naibu Spika wa Uganda Thomas Tayebwa alisema azimio hilo linatokana na taarifa potofu na upotoshaji wa makusudi wa mambo muhimu kuhusu mazingira na ulinzi wa haki za binadamu.

Alisema inawakilisha kiwango cha juu kabisa cha ukoloni mamboleo na ubeberu dhidi ya Uganda na mamlaka ya Tanzania.

Hayo yanajiri wakati Uganda na Tanzania zinajenga mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (Eacop), lenye urefu wa kilomita 1,443 (maili 896) kutoka Ziwa Albert magharibi mwa Uganda hadi bandari ya Tanga ya Tanzania kwenye Bahari ya Hindi.

Maoni ya Uganda yalikuja wakati azimio la bunge la Umoja wa Ulaya lililopitishwa siku ya Alhamisi likitahadharisha kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na hatari ya kijamii na kimazingira inayotokana na mradi wa Eacop.

Bunge la EU linashauri mataifa wanachama kutotoa msaada wowote wa kidiplomasia au kifedha kwa miradi ya mafuta na gesi ya Uganda.
Baada ya vuta nikuvute sasa Bunge la Ulaya limemshinikiza mkurugenzi wa Total ajitoe kwenye ujenzi wa bomba hili na tayari unamsikia yeye mwenyewe anaongea ukimwangalia usoni unaona anachosema kinapingana na akili zake.
Kama nilivyouliza apo awali kwanini tuwashirikishe Wazungu kwenye mradi huu? Pesa inayotakiwa kuna uwezekano mkubwa sana kuzipata tukatangaza tenda nakujenga bila mashart ya wazungu/washenzi.

#ChanzoBBC
#StarTvUpdates

Pitia iyo link utapata mwanga kabla hujaanza kurusha makombora.[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

 
Mlipo ambiwa mpige kura ili kuiwekea vikwazo urusi zidi ya uvamizi wa Ukraine mkajifanya nyie ni NAM..bora Uganda alionyesha upande wake mapema.

Hii sera ya NAM ni moja kati ya sera ya hovyo sana..hata maandiko yanasema chagua moja kuwa moto au baridi na wala sio uvuguvugu.

NAM ni moja kati ya kichaka cha umasikini na ujinga ambao hii nchi imeamua kuubariki.

Haya sasa mabwana wakubwa wamepiga pini mradi sijui na njaa zetu tuelekea wapi sasa china ama Emirates.

Nashauri serikali badilisheni hii sera ya NAM imekaa kinafiki sana na mabeberu wameshajua hilo hivyo ni mwendo wa kuwapiga pini tu.

All in all bila kupambana kujitegemea kiuchumi tutarajie mengi ya namna hii.

Akubukwe JPM.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nazani tuta amia kwa wachina... ndipo watavimba zaidi... mchina yeye hana mambo mengi...
 
Alisema inawakilisha kiwango cha juu kabisa cha ukoloni mamboleo na ubeberu dhidi ya Uganda na mamlaka ya Tanzania.
Uganda ya M7 inachekesha.wanapochukua pesa z wazungu zinazofadhili jeshi la Uganda na polisi wao kuminya haki za waganda sio ukoloni mamboleo😅
Ila wakiambiwa wasiharibu mazingira wanaitwa ukoloni mamboleo na ubeberu?
 
Kwani hao wazungu wamezitaja hizo athari za kimazingiea na hizo haki za binadamu?

Kama zimetajwa basi wapeni majibu sio mnabali kujikanyaga kanyaga na kulalamika.
 
Hakika, mambo yetu watuachie wenyewe...
 
Si wamwite Putin tu aje kuwekeza?
Walijikomba kwa Putin sasa ni saa yao ya kusulubiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…