Uganda yapata hasara ya matrilioni ya pesa kibiashara kutokana na mizozo yake na nchi jirani

Uganda yapata hasara ya matrilioni ya pesa kibiashara kutokana na mizozo yake na nchi jirani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Sekta ya biashara nchini Uganda imepata pigo kubwa sana mwaka huu kwa kuandikisha upungufu wa shilingi trilioni 3.4. Hii inatokana na mizozo ya kibiashara na mataifa jirani.

Kwa mujibu wa ripoti ya ufanisi wa kibiashara ya mwaka 2018/2019, shughuli za kibiashara kati ya Uganda na mataifa jirani, zilipungua kutoka dola milioni 932 mwaka wa 2017/2018, hadi dola milioni 11 pekee kufikia tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba mwaka 2018/19, taifa la Uganda liliuza bidhaa nje, kwa mataifa jirani, yenye thamani ya dola bilioni 1.16. Hii ikiwa ni hasara ikilinganishwa na mwaka wa 2017/18, ambapo Uganda iliuza bidhaa yenye thamani ya dola bilioni 1.55 kwa mataifa jirani.

TRT
 
Back
Top Bottom