Uganda yapeleka askari mji mkuu wa juba South Sudan kunusuru mkataba wa amani

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
12 March 2025
Kampala

Picha : rais Salva Kiir na makamu wa kwanza wa rais Dr. Rick Machar

Mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Uganda jenerali Kainerugaba Muhoozi athibitisha askari wa vikosi maalum yaani makomando wa UPDF watua katika mji mkuu wa Juba South Sudan kufuatia tishio la kuzuka mapigano baina ya kambi ya rais Salva Kiir na upande wa kambi ya makamu wa kwanza wa rais Dr. Rick Machar yanayotishia mkataba wa mwaka 2018 wa pande hizo wa mbili kuwa na maridhiano ya amani kuvunjika.


View: https://m.youtube.com/watch?v=yKx_SfIE1XI
Bunge la Uganda limehoji hali hiyo ya Uganda kupeleka majeshi nchini South Sudan ..

Wabunge wa Bunge la Uganda linataka upelekaji wa majeshi nchi jirani ufuate utaratibu wa kulifahamisha bunge maana operesheni za UPDF huko Bunia Uturi DR Congo pesa zinatumika.

Na sasa jeshi la Uganda UPDF limepelekwa South Uganda hiyo inamaana fedha zaidi, bila bunge kuhusishwa pesa zaidi za kodi na bajeti mpya inahitajika
 
Mama Afrika nini kimekupata? Wana wa Afrika kwanini tuna shindwa kumlinda Mama bora Afrika ? Viongozi wa Afrika kwanini wanamtesa Mama aliye tulea na Mama mwema Afrika? Kila uchao tuna haribu mazingira kwa kuata miti hovyo, tunachimba madini na kutapanya pesa hovyo bila kujali wananchi husika, vita kila kona kumwaga Damu za wasio kuwa na hatia ktk ardhi bora na yenye rutuba Afrika. Amahakika ni uchungu sana.
 
Acheni wauane! Ndo nature yetu waafrika…Akili hatuna had kuuana tushindwe jamani!?
 
Hapa ndo nimejua kwanini Uganda alitangaza kuwa ana mafuta mengi
 
Huyo salva kiir kashazeeka mimi naomba tu apumzike kwa kweli
 
Hii vita ya kikabila kati ya Wadinka na Wanuer inaliangamiza hili taifa changa, solution sio mtutu bali Dialogue.

Badala ya kutuma Majeshi tuwaite Arusha waje tuwasuluhishe.

Hii Jumuiya ya Afrika ya Mashariki isiwe Jumuiya ya kwenye makaratasi tu bali iwe mstari wa mbele kusuluhisha migogoro ya ndugu zetu Waafrika.
 
13 March 2025

Uchambuzi wa Uganda kutuma Vikosi Maalum Sudan Kusini

View: https://m.youtube.com/watch?v=0LvbXGWOxd0
Mvutano unazidi kuongezeka nchini Sudan ya Kusini, huku Uganda ikituma vikosi maalum mjini Juba kufuatia machafuko ya kisiasa kati ya Rais Salva Kiir na Makamu wa Kwanza wa Rais Dr. Riek Machar.

Kukamatwa kwa washirika wakuu wa Dr. Machar na mapigano makali ya kaskazini kunatishia kusambaratika kwa makubaliano ya amani ya 2018.

Wakati huo huo, mkuu wa jeshi la Uganda, jenerali Muhoozi Kaine-Rugaba, ametoa onyo kali na kusema kuwa tishio lolote kwa Rais Kiir litaonekana kuwa changamoto ya moja kwa moja kwa Uganda.

Hata hivyo, bado haijafahamika iwapo rais Salva Kiir aliomba kutumwa huku majeshi ya Uganda au ni muda gani wanajeshi wa Uganda watakaa Sudan Kusini.

Je, uingiliaji kati huu wa kijeshi unamaanisha nini kwa utulivu wa nchi ya Sudan Kusini na pia usalama wa kikanda?

Wanaoungana nasi ni Mchambuzi wa Masuala ya Afrika Dk. David Matsanga kutoka Amsterdam Uholanzi na Mtaalamu wa Usalama Dennis Amachree kutoka New York Marekani ili kutoa picha kubwa ya kitaalamu juu ya suala hili .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…