Wao, umeongea vizuri kuwa unasema ukweli! Lakini nikashangaa hujasema ukwli hapo! Ndo unazidi kushangaza zaidi!
Au basi, kila mtu aseme hapa, maana hoja imeanzia mauaji ya kimbali ya Rwanda kuwa hatukufanya kitu! Hebu sema hapa ukweli, nchi yako ilifanya nini kwenye hayo mauaji? Maana ulivyo tuliyofanya Tanzania huwezi kusema, hiyo itakuwa kazi yangu kukwambia! Sema tu ukweli kama unavyojinasibu hapa!
Suala la kuipita Kenya wala hatusubiri eti muingie kwenye machafuko, wala hatuwaombei hilo! Lakini pia msije kuleta machafuko makusudi ili mkitoka huko mkakuta tumewazidi basi mlaumu machafuko! Tunataka tuwazidi huku mkiona hivi hivi!
Na mimi ngoja nikwambie, kuwazidi kiuchumi hatutegemei eti mizigo ya rwanda na Uganda! La hasha! Tulijua tulipokosea na tutatumia rasilimali zetu hizi hizi kuwazidi!
Hivyo malizeni uchaguzi salama tubaki kupambana kiuchumi huku mkiwa mnaona!
Najua kuhusu kuzidiwa ni kitu hutaki kusikia, lakini nakwambia, majibu yako hayana tofauti na majibu ya mtu aliyeunda meli ya Titanic, alivoulizwa ubora wa meli ile akasema haitaweza kuzama kamwe! Kilichotokea kila mtu anajua!
Sasa na ninyi Kenya mtakuwa kama Titanic, mkiamini hamtaachwa kufumba na kufumbua hamtaamini!