Kavimbe
Member
- May 9, 2023
- 51
- 80
Jinsi ya kugawa Mirathi ya Kiislamu
Katika somo letu hili tutawatizama wale warithi wa msingi jinsi wanavyapata viwango vyao vya kurithi hawa huitwa warithi wasiozuiwa na yeyote.
Warithi wa msingi ni Baba, Mama, Mke/Wake, Mume, watoto wa kike na watoto wa kiume. Somo hili ni marejeo ya Kuraani Surat An Nisaai aya ya 11 na 12.
Baba na Mama hupata sudusi kila mmoja. Sudusi ni sehemu moja katika sehemu sita 1/6, yaani kiasi kinachorithiwa kinagaiwa katika mafungu sita. Baba na Mama kila mmoja atapata fungu moja katika yale sita. Baba atachukua fungu lake na mama fungu lake. Iwapo mmoja amefariki basi atachukua aliye hai fungu moja tu.
Mke au Wake wao hupata thumuni. Thumuni ni sehemu moja katika sehemu nane 1/8. Yaani kiasi kinachorithiwa kinagaiwa mafungo 8. Fungu moja katika hayo 8 ndio atapata mke au wake. Kama ni mke mmoja atachua pekee yake na kama ni wake wawili watagawana fungu hilo hilo moja.
Kama ni watatu au wanne ni hivyo hivyo watagawana fungu hilo hilo moja. Wake au Mke hupata hii thumuni 1/8 iwapo kama kuna mtoto au watoto. Na kama hakuna Mtoto au Watoto basi watapata robo 1/ 4. Robo ni kugawa kinachorithiwa mafungu manne yaani sehemu nne. Hawa ni tafauti na Baba na Mama.
Baba na Mama kila mmoja anapata fungu moja la sudusi. Wake wao hushirikiana (hugawana) wote fungu moja la thumuni au robo. Mume yeye hupata robo 1/ 4. ya kilichoachwa na na Marehemu (Mke) kama kuna Mtoto au Watoto. Na kama hakuna Mtoto au Watoto atapata nusu. Robo ni kugawa mafungu manne na nusu ni kugawa mafungu 2.
Watoto wao hupata au hugawana kile kilichobakia baada ya kutoa mafungu ya sudusi za baba na mama na thumuni ya mke au wake au robo ya mume kama aliyekufa ni mwanamke.
Mtoto wa kiume hupata sehemu sawa na wanawake wawili. Hii ni sawa na kusema mtoto wa kiume anapata mbili na mtoto wa kike anapata moja (yaani 2:1). Hapa ni iwapo warithi ni watoto mchanganyiko wa kike na kiume.
Iwapo warithi ni watoto wa kiume tu hugawana sawa sawa na ikiwa ni mtoto mmoja tu wa kiume basi huchukua kiasi chote kilichopo au kilichobakia.
Iwapo ni mtoto mmoja tu wa kike basi atapata nusu ya kilichopo na kama wapo watoto wa kike wawili na zaidi yaani watatu, wanne, watano na kuendelea wapata thuluthaa. Thuluthaa ni sehemu mbili katika sehemu tatu 2/3.
Yaani kilichopo kinagaiwa mafungu matatu wao watoto wa kike watachukua mafungu mawili na watagawana sehemu sawa sawa.
Ile sehemu ya nusu iliyobaki ya mtoto mmoja wa kike au hii sehemu ya thuluthi moja 1/3 iliyobaki ya watoto wengi wanawake, atapata tena baba wa marehemu kama yupo. Kama hayupo atapata Babu au wajukuu au kaka na dada wa marehemu.
JINSI YA KUGAWA
Mfano;
Marehemu wa kiume ameacha shillingi 150,000. Na ameacha Baba, Mama, Mke mmoja, watoto wa kike watatu na watoto wa kiume wanne.
Kwanza kabisa kabla ya kurithi kilichopo inatakiwa iwe tayari kumeshatolewa sehemu wosia kama upo, madeni, gharama za mke au wake wakati wa kipindi cha eda na zakka iwapo muda wake umefika au kama haijatolewa.
Mke/Wake: Tunachukua fedha zilizopo za kurithi ambazo ni 150,000. Katika kiasi hichi tunatoa thumuni 1/8 ya Mke au Wake. Hapa tunaigawa 150,000 kwa nane au mafungu nane.
150,000 /8 = 18,750. Hapa mke mmoja atapata kiasi hiki cha 18,750 au wake zaidi ya mmoja watagawana au watashirikiana kiasi hicho hicho kwa pamoja.
Baba na Mama; Tunachukua kiasi hicho hicho cha 150,000 tunagawa kwa sita au mafungu sita yaani sudusu. 150,000 /6 = 25,000. Hapa baba atapata 25,000 na mama vile vile atapata 25,000. Tunajumlisha thumuni ya Mke 18,750 na sudusu ya mama 25,000 na sudusu ya Baba 25,000 = 68,750.
Tutachukua kiasi chetu cha kurithi ambacho n 150,000 na tutatoa 68,750. 150,000 – 68,750 = 81,250. Hizi 81,250 ndio watarithi watoto.
Watoto wapo 7. Wa kike 3 na kiume 4.
Ili kupata kigawanyo chepesi cha watoto ni lazima tuzidishe kutokana sehemu wanazorithi. Mtoto mmoja wa kiume huwa anapata sehemu mbili wakati wa kike anapata sehemu moja. Kwa hiyo watoto wanne wa kiume itakuwa ni sehemu 8. Yaani 4 x 2 = 8. (Watoto wanne mara sehemu 2 = 8). Mtoto wa kike ana sehemu1. Wapo watoto watatu wa kike. Itawakuwa ni sawa sawa na sehemu tatu. Yaani 3x 1 = 3.
Tunajumlisha sehemu 8 za wanaume na 3 za wanawake. 8 + 3 = 11. Kiasi kilichopo tutakigawa sehemu 11. 81,250 / 11 = 7,386.36. Hapa tutapata sehemu 11 za kiasi cha shilling 7,386.36. Mtoto wa kiume kila mmoja atachukua sehemu mbili yaani 7,386.36 x 2 = 14,772.72. Na kila mtoto wa kike atachukua sehemu moja yaani 7,386.36.
Kwa hiyo kila mtoto wa kiume atapata 14,772.72 na kila mtoto wa kike atapata 7,386.36.
Mfano zaidi wa kutafuta sehemu za kugawa iwapo watoto ni kike na kiume: Wanaume ni 5 na wanawake ni 9. Ili kugawa vizuri kinachorithiwa ni lazima tupate sehemu za wanawaume na wanawake na kuzijumlisha pamoja. Wanaume wapo 5, kwa vile mwanaume anapata sehemu mbili tunazidisha kwa 5. 5 x 2 = 10.
Wanawake wapo 9. Ni sawa sawa na sehemu 9 kwa vile mwanamke ana sehemu 1. 9x 1 = 9. Tunajumlisha sehemu 10 za wanaume na 9 za wanawake. 10 + 9 = 19. Hapa tuna jumla ya sehemu 19.
Kilichopo au kilichobakia baada ya kurithi baba, mama, mke au mume kinagaiwa sehemu 19. Kama tunazo 2,750,000 tunagawa kwa 19. 2,750,000 /19 = 289,473.68. Kwa hiyo mwanaume kila mmoja atapata sehemu mbili yaani 144,736.84 x 2 = 289,473.68. Wanawake kila mmoja atapata sehemu moja yaani 144,736.84 x1 = 144,736.84.
KAMA HAKUNA MTOTO AU WATOTO.
Iwapo marehemu hana mtoto /watoto na ameacha Mke, Baba na mama. Mke atachukua robo. Kilichobaki watarithi wazazi wake. Mama atapata thuluthi moja 1/3 na baba atapata thuluthi mbili 2/3.
Na vile vile iwapo Marehemu hakuacha mtoto wala Mke basi warithi wake ni wazazi wake. Mama atapata thuluthi. Thuluthi ni sehemu moja katika sehemu tatu. Yaani kilichopo kitagaiwa mafungu matatu, mama atachukua fungu moja na baba atachukua mafungu mawili. Hii ni sawa sawa na ile mwanaume anapata 2 wanamke 1 yaani 2:1
Ikiwa yuko Baba tu hakuna mtoto/watoto, Mke/Wake wala Mama basi baba atachukua urathi wote. Iwapo kuna mama tu na wapo ndugu wa marehemu (kaka na dada) basi mama atapata sudusi na kilichobaki wanagawana ndugu wa marehemu.
Hawa ndugu watatumia kigawano kile kile cha 2:1 kama ni wanawake na wanaume. Kama ni wa jinsi moja watagawana kama tulivyoeleza hapo kabla.
Maiti wa kike atarithiwa katika vigawanyo kama vya maiti wa kiume, isipokuwa tu kwa maiti wa kike ataingia mume. Mume anapata robo kama kuna mtoto/watoto kama hakuna atapata nusu.
Warithi wengine watarithi kama tulivyoeleza hapo mwanzo kwa maiti wa kiume.