SoC02 Ugeni wenye faida na uliosababisha vifo vingi

SoC02 Ugeni wenye faida na uliosababisha vifo vingi

Stories of Change - 2022 Competition

kukujogoo

Member
Joined
Nov 22, 2013
Posts
21
Reaction score
5
Takriban miaka miwili iliyopita Dunia ilipokea ugeni hatari bila hodi . Mgeni huyu alitembelea maeneo mbalimbali kuanzia bara la Asia, Ulaya, Amerika ya Kusini na Kaskazini, Australia pamoja na bara letu la Afrika.

Kwa nchi yetu, mgeni alibisha hodi kupitia mkoa wa Arusha na Kisha kusambaa katika mikoa mingine mbalimbali. Mgeni huyu aliogopeka Kila alipokwenda na hakuna aliyekua tayari kumpokea Kwa sababu ya hofu na madhila aliyoyasababisha.

Serikali na mataifa mablimbali yalitikiswa, Mgeni hakuchagua dini wala kabila, ilifikia hatua ya binadamu kuogopana na kuonana kama maadui, watu walilazimishwa kufungiwa ndani kama wanyama hatari. Wakashindwa kufanya shughuli za uzalishaji Mali na za kuhudumia jamii, Njaa ilitamalaki vifo vikaongezeka miongoni mwa Vijana, wazee, watoto waume Kwa wanawake, Nchi zikapoteza nguvu kazi.

Dalili za kutembelewa na Mgeni huyu zikaanza kudhihirika wazi wazi miongoni mwa nyingi lakini kubwa zilikua ni kupata changamoto ya upumuaji, kikohozi kikavu, viungo kuuma, uchovu uliopitiliza, kupiga chafya na kudhoofu mwili.

Hospitali zilifurika na kuzidiwa na waathiriwa wa mgeni huyu hadi kufika wahudumu was afya kukimbia wagonjwa. Mfumo mzima wa maisha tuliyozoea ulibadilika, taratibu za mazishi na maziko zilibadilika zikawa tofauti kabisa na Mila na desturi zetu. Watu walizikwa kwenye makaburi ya pamoja na ndugu hawakuruhusiwa kuona wapendwa wao. Hakika Hali iliogofya sana.

Uchumi wa Dunia ulitetereshwa na kuporomoka kabisa, watu waliachishwa na kuacha kazi Kwa hofu, baadhi ya serikali duniani zilianguka na nyingine kufilisika kutokana na athari za mgeni huyu.

Wataalamu wa Afya wakiongozwa na shirika la afya duniani, WHO walifanya tafiti wakaja na mbinu mbalimbali na kanuni za kujikinga na mgeni huyu.

Mbinu hizo zilijumuisha, Kwanza kuzingatia umbali wa mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine hii itasaidia kupunguza kusafirisha vimelea kwa umbali mfupi na kuwa si rahisi kumfika mtu mwingine, Pili tulikumbushwa umuhimu wa kunawa mikono mara Kwa mara kwa maji tiririka na sabuni Ili kuua vimelea vya mgeni huyu.

Tatu, kuvaa barakoa kuepuka vimelea vya mgeni huyu, Nne kuepuka misongamano ya watu katika vyombo vya usafiri,shuleni na popote pale kwenye huduma za kijamii, Nne kufunika pua zetu kwa kitambaa safi pale tunapotaka kupiga chafya au kukohoa. Na mwisho kabisa lakini si kwa umuhimu ni kuwahi katika kituo Cha afya kilichokaribu nawe pale unapohisi ni mgonjwa.

Kutokana na taratibu na kanuni hizi za afya, Mgeni akadhibitiwa Kwa kiasi kikubwa na kupunguza vifo kwa kiwango kikubwa sana duniani kote na maisha yakaanza kurejea kama ya awali japo si kwa kiwango kile kwa sababu ya hofu miongoni mwa watu.

Pamoja na madhila na hasara nyingi zilizosababishwa na ugeni huu lakini Kuna faida Dunia na taifa lilipata kutokana na mgeni huyu hatari.Kwa taifa letu la Tanzania, faida hizo zimegawanyika katika makundi makuu matatu kwanza faida katika sekta ya Afya, pili katika sekta ya Elimu na tatu katika sekta ya Maji na Miundombinu mbalimbali.

Kwenye sekta ya Afya, tulipata msaada wa hela kutoka mashirika ya kifedha ya kimataifa Ili kuweze kuimarisha sekta ya Afya iliyokua imeathiriwa zaidi na ugeni huu, nchi yetu ilitumia fedha hizo kujenga na kufanya maboresho kwwnye maabara, ujenzi wa majengo ya dharura, ujenzi wa vyumba vya upasuaji, kuzalia pamoja na vyumba vya kuhudumia na kulaza wagonjwa mahututi na ununuzi wa vifaa tiba. Hii imechangia kuongeza ufanisi na motisha kwa wahudumu wa afya nchini na kupunguza gharama za matibabu. Vile vile imechangia kupunguza vifo na rufaa zisizo na ulazima.

Kwa upande wa Uboreshaji wa huduma za maji, ugeni huu ulisaidia sana upatikanaji wa fedha Ili kuboresha huduma za maji safi na salama hususani vijijini na mijini, kwa kiwango kikubwa changamoto hizo zimepungua kama sio kuisha kabisa.

Kwa upande wa elimu, Ugeni huu umwtupatia faida kubwa, faida hizo ni kama upatikanaji wa fedha zilizotumika kuboresha na kujenga madarasa mapya nchi nzima, kutengeneza madawati, kujenga na kuboresha nyumba za walimu, kuondoa ada kuanzia elimu ya msingi na sasa hadi kidato cha sita, hii imechochea kuongeza ufanisi na kuboresha kiwango Cha udahili na ufaulu kwenye shule zetu katika ngazi mbalimbali.

Uchumi wetu kama nchi umeimarika na vile vile uchumi wa mtu mmoja mmoja umeendelea kuimarika. Kwa sasa wananchi wanatumia muda mchache kupata huduma za kijamii kama afya, elimu,maji na nyinginezo zilizoboreshwa zaidi na serikali kutokana na fedha zilizotengwa katika kupambana na athari zilizoletwa mgeni huyu.

Kutokana na Mgeni huyu sisi kama jamii tumepata funzo nyingi sana, ikiwemo, Moja Umuhimu wa kushirikiana miongoni mwetu Ili kupambana na majanga yanayotukabili, hili limeonekana Katika kipindi Cha ugeni huu, maana ushirikiano baina ya mataifa ulisaidia kupunguza kuenea kwa mgeni huyu.

Pili, umuhimu wa kuweka akiba ya chakula, tumeona katika kipindi hiki zile jamii ambazo hazikua na utaratibu wa kujitunzia chakula nyingi zilitaabika na kupoteza maisha Kwa baa la njaa. Na tatu, umuhimu wa kufuata miongozo, kanuni na taratibu za afya kutoka kwa wataalamu wetu wa afya Ili kupunguza kusambaa Kwa magonjwa mbalimbali na mwisho kabisa ibada na toba no silaha tosha katika kujikinga na majanga mbalimbali katika dunia yetu.

Pamoja na yote haya niliyoandika lakini tuendelee kukumbuka kwamba mgeni huyu bado yupo katika mazingira yetu. Na bado sisi kama jamii tuna wajibu wa kulinda afya zetu kwa kufuata kanuni zote za afya tunazoelekezwa na wataalamu wetu.

Ndugu msomaji,Je umeweza kung'amua mgeni huyu ni nani?

Hakika, tuendelee kuchukua tahadhari mgeni bado yupo. Tushirikiane kuupiga vita Ugonjwa wa Virusi vya Korona 19 ( UVIKO- 19).
 
Upvote 1
Back
Top Bottom