Ugiriki:Tetemeko La Ardhi Limevikumba visiwa Vya Amorgos Na Santorin

Ugiriki:Tetemeko La Ardhi Limevikumba visiwa Vya Amorgos Na Santorin

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Tetemeko kubwa la ardhi limerekodiwa kati ya visiwa vya Ugiriki vya Amorgos na Santorini, baada ya siku za mitetemeko mfululizo katika eneo hilo.

Zaidi ya watu 11,000 tayari wameondoka Santorini huku karibu 7,000 wakiondoka kwa feri na watu 4,000 wakiondoka kwa ndege.

Tetemeko hilo lilifuata mitetemeko midogo miwili dakika zilizopita, na lilirekodiwa saa 21:09 saa za ndani (19:09 GMT) kama tetemeko la kipimo cha 5.2, na kuifanya kuwa kali zaidi katika siku za hivi majuzi. Inakadiriwa kuwa ilitokea kwa kina cha kilomita 5.

Hadi sasa uharibifu mkubwa haujaripotiwa katika kisiwa hicho lakini mamlaka imekuwa ikichukua hatua za tahadhari.
 
Back
Top Bottom