fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 2,977
- 3,798
Hawa ndugu wakiumu,waliozaliwa na mama mmoja ila baba tofauti,wote ni madereva na asili yao ni wahindi.Maisha yao wanayoishi ni kama waafrika kabisa,kwa kila kitu,kula,kuvaa,mademu ni kama wafanyavyo wabantu.Wameajiriwa na tajiri mmoja,sasa bosi wao akawaambia kuwa wajiandae kwa safari ya kenya na uganda maana ni madereva wake.Hao ndugu hawasemeshani kabisa na safari nzima hawaongei,bosi wao alikuwa anawashangaa sana,akiwauliza nyie mna ugomvi gani hawajibu.Huyo bosi wao ni rafiki yangu sasa na ndiye alikuwa akinipa huu mkasa na alikuwa anashangaa sana.Njia nzima hao ndugu ni kugombana na mpaka leo hii hao ndugu wana umri mkubwa hawaongei kabisa.Sijui ni kipi kikisababisha,wadau mshakutana na hali kama hii,ndugu hawaongei kwa takriban miaka zaidi ya 20