Ugomvi wa Singano v Simba - kuna nini nyuma ya pazia?

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2012
Posts
1,544
Reaction score
943
Nimefuatilia kwa siku kadhaa sasa kuhusiana na sinema inayoendelea kati ya Ramadhani Singano 'Messi' na klabu yake Simba. Japo sijajua nani ni mkweli na nani mwongo, lkn ninapotafakari kinachoendelea naamini kuwa kuna kitu nyuma ya hili sakata maana kuna maswali mengi yasiyo na majibu

Moja, Kwa nini Messi anakwenda kwenye vyombo vya habari na hasa Clouds fm (to be specifically, Shaffih Dauda) kulalamikia 'kughushiwa' kwa mkataba wake badala ya kwenda TFF? Msemaji wa TFF amekaririwa akidai hawajapokea malalamiko yoyote hadi sasa. Kwa hiyo swali langu hapa ni kuwa Messi anataka nini hasa,kuichafua Simba au kutatuliwa kwa tatizo hili la mkataba?

Mbili, 'kughushiwa' kwa mkataba wake kuna uhusiano gani na mahali anapoishi yaani kwa kaka yake? What is logical connection kati ya mahali anapoishi Singano na kughushiwa kwa mkataba wake. Hili la sehemu ya kuishi lilikuwa la muhimu kuendana na movie ya 'kughushiwa' kwa mkataba?

Tatu, kama kuna nia njema nguvu hii inayotumika kulalamika kuujulisha umma kuwa mkataba wa Messi na Simba umekwisha, kwa nini haikutumika kudai kutekelezwa kwa makubaliano na vifungu vya mkataba aliokuwa nao na Simba kama walivyofanya akina Okwi kwa Yanga na Kessy kwa Simba? Au kwa nini hadai fidia kwa Simba kwa kutokutekezwa kwa vipengele hivi?

Nne, Shaffih Dauda na mwenzie Luambano, wana tatizo gani na Simba au na uongozi wa sasa wa Simba(sitaki kuamini kuwa ni chuki) maana ktk siku za hivi karibuni wamekuwa na mtazamo mbaya tu kuhusiana na Simba, nakumbuka nguvu waliyotumia kupigia kelele mgogoro wa Kessy na Simba, matatizo ya Simba ktk ziara za mikoani mfano kule Shinyanga na Mbeya na mambo mengine yanatosha kuaminisha kuwa kuna kitu ambacho kinatafutwa au kinafichwa. Siungi mkono ubabaishaji wowote unaodaiwa kufanywa na viongozi wa mpira wakiwemo Simba, lkn nguvu inayotumika inaelekezwa upande mmoja tu? Ndio kusema huko tu ndio kuna matatizo, au wachezaji wasiolipwa au kutimiziwa mahitaji yao?

Je tuamini ktk maneo ya msemaji wa simba Haji Manara kuwa kuna 'maumivu' yanayotokana na siasa za uchaguzi?

Tano, kama hakuna, kwa nini taarifa nyingi zinazohusu malalamiko dhidi ya Simba hasa viongozi wake huwa zinakuwa za upande mmoja? Yaani mlalamikaji anatoa malalamiko yake, lkn wasikilizaji hatupewi upande wa pili wa shilingi kwa nguvu ileile au airtime ileile ili tuamue mbivu na mbichi? Maadili ya uandishi wa habari yanasemaje ktk hili?

Maswali ni mengi lkn ngoja niishie hapa kusikia maoni ya wadau wengine.
 
Kwanza huyo msemaji wa Simba ni mropokaji sana na anatia hasira sana some times.
But kuhusu Singano tuwaachie wanasheria kwanza,but just remember,wachezaji wetu ni mambumbu sana,bahiri wasiotaka kutumia wanasheria.
So unaweza kukuta Simba wapo sahihi.
But ngoja tusubiri tutaona mengi maana Simba nao kwa kufoji hawajambo.

cc chuji , Yondani
 
Last edited by a moderator:
Hili la Singano na Simba hata mimi linanipa shida sana kwa sababu TFF wanaweza kulitolea tamko ndani ya masaa machache na kukata mzizi wa fitina kuwa nani mkweli kati ya Simba na Singano. Pili kama litakuwa limewashinda kwenye suala la kughushi wanatakiwa kulipeleka kwenye vyombo vya dola na kutoa taarifa kwa umma basi.
 
Kilichonishangaza zaidi jana ni kwamba baada ya mkutano wa Manara na waandishi wa habari na kutoa maneno kuwa kuna baadhi ya waandishi wa habari wana NONGWA na uongozi wa Simba uliopo madarakani, usiku kwenye kipindi cha michezo Shaffih Dauda alitokwa na povu sana wakati akiongelea hii issue, nikajiuliza kwani maneno ya Hajji Manara yalikuwa yanamgusa yeye?
 
Me naamini mara nyingi Shaffih Dauda anakurupukia sana issues ili aonekana kama mkombozi wa soka la Bongo lakini ni MNAFIKI namba moja huyu jamaa. Ila watu wengi wamekuwa wasahaulifu ndo maana hawaligundui hili. Ntatoa mfano halisi.

Wakati wa SAKATA la issue ya mkataba wa Azam TV na Yanga FC kama mtamkumbuka Shaffih na wenzake waliiponda sana Yanga wakasema mashabiki hawawezi kuacha kwenda uwanjani kisa mechi znaonyeshwa LIVE, kwamba Yanga waache fikra hizo. Akaongeza kuwa hata Ulaya mechi znaonyeshwa LIVE na watu wanajaa viwanjani.

Juzi hapa kajitokeza Hans Poppe na kusema kuwa TFF, Simba, Yanga na Azam Tv wakae tena wauangalie upya mkataba wa Azam TV unazinyonya klabu kubwa Simba na Yanga kwamba mapato yao mlangoni yamepungua sana tofauti na wakati Azam Tv haionyeshi mechi zao. Akamsapoti kwa nguvu zote. Nikajiuliza alichopinga kwa Yanga ni nini na leo ana-support nini?
 
Tatizo ninaliloiona ni ubabaishaji unaoanza kwa wachezaji, vilabu (vyote), TFF lakini zaidi ni wanahabari. Ubabaishaji wa wachezaji una sura nyingi, lakini yenye mnasaba na sakata la Messi na Simba ni wachezaji kukubali eti wameibuliwa na kulelewa na timu za Premeir (zote) ilhali wakijua kwamba sio kweli. Ukimya wao unatokana na uroho/ushamba wa viposho vidogo wanavyolipwa wanaposajiliwa na 'timu ndogo' za Premeir kwa sifa tu kwamba ni wachezaji wa Azam au Yanga au Simba.

Nina ushahidi hai wa wachezaji waliokataa kucheza Ligi Kuu ya Zanzibar kwa visingizio mbalmbali, wakaishia kwenye timu za Uhai Cup za Ligi Kuu kama wachezaji wa timu 'B'. Wakaishia kusota miaka kadhaa kwenye Timu B hizo kabla ya 'kupandishwa'. Wenzao waliokubali moja kwa moja kucheza Ligi Kuu hiyohiyo ya Zanzibar wakajikuta wanawaniwa na timu A za Ligi Kuu ya Vodacom kwa mamilioni ya shilingi. Wapofu wa aina hii ninaowajua mimi ni wa umri mmoja na Messi, 'waliopndishwa' pamoja (sikusudii Messi alitokea Zanzibar).

Upofu wa aina hii ndio unaovipa jeuri vilabu kusakizia mikataba ya kiajabuajabu kwa wachezaji wa aina hii. Uwe umeghushiwa au la, mkataba wa mchezaji anayejijua ana miaka ishirini lakini akakubali aandikwe ana Miata 16 il aweze kuchezea Timu B kwa sababu tu ya tamaa ya kucheza Premeir lazima utalalia upande wa mchezaji huyo.

Self Abdalla Karihe aliyenunuliwa Azam kutoka timu mojawapo ya JKT misimu mitatu iliyopita alitofautiana kiasi gani kiumri na akina Messi wakati huo? Ubabaishaji wa vilabu wenye mnasaba na sakata hili ni huo wa kujidai vina 'Timu B', 'academy' n.k. ilhali wachezaji wenyewe wanawatoa kwenye timu za Daraja la kwanza na la pili Tanzania Bara na vilabu vidogo vya Ligi Kuu Zanzibar.

Wanahabari nao, iwe kwa kukaa kimya kwa makusudi au kushindwa kubaini uongo huo, wanabaki kuwa wababaishaji namba moja; viziwi wanaooneshwa njia na vipofu!

Hubaki wakivisifia vilabu vinavyoshamiri kudanganya kuwa na academy na kuvilaani visivyotangazia 'uporaji' huo wa vipaji. Kwa mtaji huo tutegemee nini kutoka kwa wachezaji hawa wapofu, vilabu hivi vipuuzi, wanahabari hawa mabwege na TFF hii goigoi inayoyaona yote hayo na ikakaa kimya?
 
tatizo la messi liko kwa watanzania wengi hasa wafanyao kazi nina uhakika wa 75% amesaini hizo nyingine inawezekana hakusaini wengi hawasomi kilichoandikwa wanaangalia wanapata shilingi ngapi kama simba waliboresha mshahara wake ni wazi waliongeza mkataba ila kwa kuangalia tu pesa imeongezwa ndio kinamsumbua kwa sasa
 
habari ya singano na simba mmeiandama sana, acheni yatatatuliwa tu hayo
 
Niliona picha za anakoishi huyu kijana ni zaidi ya uchochoroni mbaya zaidi ni kwa kaka yake,
Kweli Bongo ni shiiiiidddeeerrrr, na ndo moja ya ma star hyo wa soka Bongo hadi kapachikwa jina la Messi
 
Nina almost similar case na kinachotokea kwa messi,kama alivyosema mdau mmoja hapo juu,ili tatizo ni la watanzania wengi.kutosoma kilichoandikwa.
Kuna kundi la manesi wa hospitali walijiokusanya wakaenda kuchukua mkopo kwenye hizi microfinance firms,sasa kilichotokea hawa vijana wa hizi microfinances wanawasignisha watu mikataba kabla ya kuandika kiasi kitakachokopwa,badae wanachokifanya wana waandikia hela kubwa tofauti na ile waliotaka kukopa,matharan walisha sign mkataba,ile hela ikitoka wale vijana wanakata kile kias walichokiongeza thn wale wakopaji wanapewa kias walichoomba bas ktk makato itakatwa ile hela yote,tuwe makin na mikatabannayo mifano mingi ya victims wa mikataba na wengi sababu ni kutoisoma mapema.!
 
Simba kuna tatizo. Huyu si mchezaji wa kwanza kulalamikia forgery. Kumbukeni issue ya Chuji
 
Kumbe Singano hakusomeshwa na Simba sekondari, kama Manara alivyojigamba juzi
 
Kumbe Singano hakusomeshwa na Simba sekondari, kama Manara alivyojigamba juzi

Tatizo la watanzania ni listening skills, ukimsiliza vizuri Manara alisema Simba ilimsomesha IT. Ila kwa kuwa huyu bwana aliongea haraka haraka HIYO IT HAISIKIKI VIZURI , MI NILISIKILIZA CLOUDS NDO NKAELEWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…