Nimefuatilia kwa siku kadhaa sasa kuhusiana na sinema inayoendelea kati ya Ramadhani Singano 'Messi' na klabu yake Simba. Japo sijajua nani ni mkweli na nani mwongo, lkn ninapotafakari kinachoendelea naamini kuwa kuna kitu nyuma ya hili sakata maana kuna maswali mengi yasiyo na majibu
Moja, Kwa nini Messi anakwenda kwenye vyombo vya habari na hasa Clouds fm (to be specifically, Shaffih Dauda) kulalamikia 'kughushiwa' kwa mkataba wake badala ya kwenda TFF? Msemaji wa TFF amekaririwa akidai hawajapokea malalamiko yoyote hadi sasa. Kwa hiyo swali langu hapa ni kuwa Messi anataka nini hasa,kuichafua Simba au kutatuliwa kwa tatizo hili la mkataba?
Mbili, 'kughushiwa' kwa mkataba wake kuna uhusiano gani na mahali anapoishi yaani kwa kaka yake? What is logical connection kati ya mahali anapoishi Singano na kughushiwa kwa mkataba wake. Hili la sehemu ya kuishi lilikuwa la muhimu kuendana na movie ya 'kughushiwa' kwa mkataba?
Tatu, kama kuna nia njema nguvu hii inayotumika kulalamika kuujulisha umma kuwa mkataba wa Messi na Simba umekwisha, kwa nini haikutumika kudai kutekelezwa kwa makubaliano na vifungu vya mkataba aliokuwa nao na Simba kama walivyofanya akina Okwi kwa Yanga na Kessy kwa Simba? Au kwa nini hadai fidia kwa Simba kwa kutokutekezwa kwa vipengele hivi?
Nne, Shaffih Dauda na mwenzie Luambano, wana tatizo gani na Simba au na uongozi wa sasa wa Simba(sitaki kuamini kuwa ni chuki) maana ktk siku za hivi karibuni wamekuwa na mtazamo mbaya tu kuhusiana na Simba, nakumbuka nguvu waliyotumia kupigia kelele mgogoro wa Kessy na Simba, matatizo ya Simba ktk ziara za mikoani mfano kule Shinyanga na Mbeya na mambo mengine yanatosha kuaminisha kuwa kuna kitu ambacho kinatafutwa au kinafichwa. Siungi mkono ubabaishaji wowote unaodaiwa kufanywa na viongozi wa mpira wakiwemo Simba, lkn nguvu inayotumika inaelekezwa upande mmoja tu? Ndio kusema huko tu ndio kuna matatizo, au wachezaji wasiolipwa au kutimiziwa mahitaji yao?
Je tuamini ktk maneo ya msemaji wa simba Haji Manara kuwa kuna 'maumivu' yanayotokana na siasa za uchaguzi?
Tano, kama hakuna, kwa nini taarifa nyingi zinazohusu malalamiko dhidi ya Simba hasa viongozi wake huwa zinakuwa za upande mmoja? Yaani mlalamikaji anatoa malalamiko yake, lkn wasikilizaji hatupewi upande wa pili wa shilingi kwa nguvu ileile au airtime ileile ili tuamue mbivu na mbichi? Maadili ya uandishi wa habari yanasemaje ktk hili?
Maswali ni mengi lkn ngoja niishie hapa kusikia maoni ya wadau wengine.