Ugomvi wa Wema na Kajala, wabunge waingilia kati

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mambo bado mabaya ! Ule ugomvi wa mashosti wawili nyota katika tasnia ya sinema Bongo, Wema Isaac Sepetu ' Madam' na Kajala Masanja ' K ' , sasa umechanja mbuga hadi kufika mjengoni , ambako inadaiwa kuwa baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,wameingilia kati ili kuumaliza.

Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya mvutano wao wa muda mrefu , wabunge hao walimwita Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity , Steven Mengere ' Steve Nyerere ' na kumuuliza kama ni kweli wawili hao hawaelewani.Inadaiwa kuwa Steve alikiri kutokuwepo kwa maelewano kati ya wawili hao ambao awali walikuwa ni marafiki pete na kidole.

Ilisemekana kwamba baada ya kuhakikishiwa kuwepo kwa ishu hiyo , baadhi ya wabunge hao, hasa wapenda michezo na sanaa, walimuagiza Steve kulifanyia kazi tatizo hilo haraka , akishindwa basi awapelekee ili wawakalishe chini .

Wema Isaac Sepetu ' Madam'. "Walimwambia Steve kwamba ni kitendo cha aibu kwa mastaa wakubwa kama hao kugombana, hiyo inawapunguzia heshima kwani hiki kilikuwa ni kipindi cha kushikamana kwa umoja ili kuisogeza mbele tasnia yao badala ya kulumbana ," kilisema chanzo hicho kikikataa kutaja majina ya wabunge hao na kutaka aulizwe Steve.

Gazeti hili liliwasiliana na Steve juu ya ukweli wa madai hayo, ambaye alikubali kuwa ni kweli baadhi ya wabunge wamemtaka kumaliza bifu kati ya waigizaji hao maarufu Bongo kwani nyuma yao kuna vijana wengi wanatamani kuwa kama wao . Kajala Masanja .

Risasi Jumatano lilizungumza na mbunge wa Kinondoni Idd Azan ambaye alisema hata yeye atawaunga mkono wabunge watakaojitolea kuwasuluhisha mastaa hao .
 
Uuwiiii..... Hawa wabunge wamekosa cha kujadili...
Binamu nimetingwa nitakuja baadae
 
Kwa kweli naionea huruma 'kodi' yangu nikatwayo kulipa hawa watu!

Hebu fikiria viongozi wa zamani aina ya Warioba muandishi uchwara kama huyu ampigie simu kumueleza utumbo kama huu nini kingetokea :der:
 
Uuwiiii..... Hawa wabunge wamekosa cha kujadili...
Binamu nimetingwa nitakuja baadae

Binamu na wewe unakata utamu sasa, unaenda wapi sasa ?? , kesho ntakushtua uangalie bunge maana naskia madame atakuwepo mjengoni
 
nahitaji kusuluhishwa na wabunge pia nimegombana na rafiki yangu. Kodi yangu imlete halima mdee aje kusuluhisha
 
This is a special product from Tanzania....yes this is only possible in Tanzania!
 
hhahahahahaha daaa hawa wabunge wamekosa kazi za kufanya kabisa.

Kwanza huyo Steve ni tatizo.
 
Kuna Mbunge mmoja alishawahi kutuhumiwa kutaka kusuluhisha ugomvi wa Wema na marehemu Kanumba kama sikosei kumbe ilikuwa gia ya kuingilia mwishowe akamla Wema.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kuna Mbunge mmoja alishawahi kutuhumiwa kutaka kusuluhisha ugomvi wa Wema na marehemu Kanumba kama sikosei kumbe ilikuwa gia ya kuingilia mwishowe akamla Wema.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Kama ndo ivyo sa hv wataliwa wote hao!
 
Kuna Mbunge mmoja alishawahi kutuhumiwa kutaka kusuluhisha ugomvi wa Wema na marehemu Kanumba kama sikosei kumbe ilikuwa gia ya kuingilia mwishowe akamla Wema.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Waende tu wakaliwe sasa gia zote kumi na sita za nn?? Wakat gar lenyew vits, huyo steve awapeleke kwan asiyejua yeye n kuwad nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…