Prince Kunta
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 22,797
- 28,904
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
vip mtaalam bado upo na uyo manzi au 🤔🤔Hivi karibuni, kuna rafiki yangu mmoja alipewa invitation sehemu. Akanicheck nimpe kampani. Tukaenda wote.
Ilikuwa ni house party ya familia fulani ya kiarabu. Naweza kusema ni wale waarabu waliopinda na kunyongorota kabisa maana wanatafuna mirungi, gomba na kukata kilaji kama hawana akili nzuri.
Kitu kimoja ambacho kiliniboa ni playlist yao ambayo ilikuwa inasindikizia ile party. Walijaza nyimbo za Ali Kiba za kiarabu na Marekani kiasi.. Tatizo langu lilikuwa hapo kwa Ally.
Kuna binti ambaye alikuwa ndio anacontrol muziki tulikuwa close na tunapiga story sana vile ni mchangamfu. Uvumilivu uliponishinda, nikamwambia naomba hizo nyimbo za Kiba uzipotezee bhana. Akanishangaa!
Akasema wewe unataka zipi maana humu ndani kila mtu hampendi Diamond/WCB, wote ni team Kiba. Ikawa zamu yangu kushangaa!
Ikabidi tu nimwambie ukweli. Ugomvi wangu na Ali Kiba sio ushabiki wa u-team. Ni binafsi sana. Nikamsimulia kilichotokea kati yangu na msanii huyo takribani miaka 10 iliyopita.
Ni mapenzi. Alitembea na msichana wangu ambaye alikuwa shabiki wake namba moja. Kiukweli ule ushabiki wake hata mimi ulikuwa unanitia wivu sana ila sikujua kama zingefanyika jitihada za kutokea yaliyotokea. Nilirahisisha mno nikajisahau kuwa sote tupo ndani ya Jiji moja na chochote kinawezekana.
Ili ombi langu lifanyiwe kazi, nikamtania kidogo kwa kumsifia kuwa msichana mwenyewe alikuwa shombe shombe kama wewe japo umemzidi uzuri na akili kidogo. Tukacheka na nyimbo za Ali Kiba hazikupigwa tena mpaka tulipoondoka.
NB: Ali Kiba ni msanii mzuri na ana kipaji cha kweli. Sidhani kama kuna msanii anamfikia hasa kwa vocals. Sina tatizo nae kimuziki، ila siwezi kumshabikia kwa sababu nitakuwa natakatisha kile alichonifanyia miaka ile.
Kwa ujumla, nashauri wasanii na watu maarufu wawe na nidhamu. Mitaani kuna visasi vingi.
Hapana mzee. Halafu siku hizi amekuwa video queen.vip mtaalam bado upo na uyo manzi au [emoji848][emoji848]
Mimi nikiwa na mahusiano na binti nikaona ana ndoto za kuwa video vixen na anakuwa inspired na akina tunda yani najiandaa kisaikolojia na kutoka ndukiii
NB: Ali Kiba ni msanii mzuri na ana kipaji cha kweli. Sidhani kama kuna msanii anamfikia hasa kwa vocals. Sina tatizo nae kimuziki، ila siwezi kumshabikia kwa sababu nitakuwa natakatisha kile alichonifanyia miaka ile.
Uwe unasoma kwa kuelewa. Neno siku hizi hukuliona?
Bado hujaelewa!Demu ambaye ndoto zake ni kuwa video vixen huyo hafai hata kwa kachumbari, huo ndio ukweli.
Kipaji chake kinamsaidia nini ..manake anabana tu pua na hana ubunifu wowote ....mnavyomsifia ndiyo mnavyozidi kumpotosha..kubalini tu zama zake zimekwisha.....Bana pua na wewe
Ali Kiba ni msanii mzuri na anapata riziki ya kutosha tu kupitia kazi yakeKipaji chake kinamsaidia nini ..manake anabana tu pua na hana ubunifu wowote ....mnavyomsifia ndiyo mnavyozidi kumpotosha..kubalini tu zama zake zimekwisha.....
Sent using Jamii Forums mobile app