Ugonjwa gani huu?

Ugonjwa gani huu?

Majoajosh

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2020
Posts
276
Reaction score
186
Wakuu salamu za asubuhi

Naomba mnitoe tongotongo, huu ni ugonjwa gani kwa kuku na dawa yake ni nini?

Kuku anakuwa kama amepaniki, anaangalia juu na mara chini, anazungukazunguka, anarudi kinyumenyume, yaani fujo tupu.

Hata kula anashindwa ni kama amepata kichaa. Mimi siuelewi huu ugonjwa,wadau karibuni kwa maelezo.

Ni kuku wa kienyeji
 
Kuku anakuwa Kama amepaniki, anaangalia juu ya Mara chini, anazungukazunguka, anarudi kinyumenyume, yaani fujo tupu.

Hahahaha, hapo kwenye kupaniki nacheka kama mazuri. Ila mkuu uko vizuri sana kwenye kufuatilia mienendo ya mifugo yako, mpaka kugundua kuku hayuko sawa sio jambo rahisi. Wengi wanajuaga mdondo tu
 
Hahahaha, hapo kwenye kupaniki nacheka kama mazuri. Ila mkuu uko vizuri sana kwenye kufuatilia mienendo ya mifugo yako, mpaka kugundua kuku hayuko sawa sio jambo rahisi. Wengi wanajuaga mdondo tu
Asante mkuu,ndo hivyo Sasa akifa kuku mmoja ni hasara kwenye huu uchumi wa kati
 
Wakuu salamu za asubuhi

Naomba mnitoe tongotongo, huu no ugonjwa gani kwa kukuna dawa yake ni nini?

Kuku anakuwa Kama amepaniki, anaangalia juu ya Mara chini, anazungukazunguka, anarudi kinyumenyume, yaani fujo tupu.

Hata kula anashindwa ni km amepata kichaa. Mimi siuelewi huu ugonjwa,wadau karibuni kwa maelezo.

Ni kuku wa kienyeji
Kideli
 
Sio ugonjwa ila inaonekana kàtoka kufumania mkewe anamegwa na kuku mwingine. Mke anauma we acha tu.
 
Back
Top Bottom