Ugonjwa hatari wa mbwa

Ugonjwa hatari wa mbwa

Helicobacter pylori

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
424
Reaction score
283
IMG_5631.JPG

Kama unataka/Unapenda kufuga Mbwa hasa wakigeni (Wakizungu) basi huna budi kuujua ugonjwa huu na namna ya kuepuka.

Kwa wale Wapenzi wa Mbwa kindaki ndaki, Wanaofuga Mbwa kwa Mapenzi au Kibiashara Wanajua Shuguli yake,
Akifika na Hujajiandaa atakuachia Historia tu.,

Canine Parvovirus Infection(CPV) alimaarufu kama Parvo, ni Ugonjwa hatari, unaoshambulia haraka, na ndio moja ya sababu kuu ya vifo vingi vya utotoni kwa watoto mbwa.

Ugonjwa huu ni Ugonjwa wa Virusi.
Mbwa watoto (wiki 4-24 yaani mwezi 1-6) na wale Wasiochanjwa wapo katika hatari zaidi ya kuugua.

MAMBO HATARISHI
1. Mbwa wa Jamii hizi (Doberman Pinschers, Rottweiler, American Pit bull Terriers, English Springer Spaniels na German Shepherds) zipo katika hatari zaidi kuliko jamii zingine.
2. Mbwa wasiochanjwa
3. Watoto Kupata kinga kidogo/uchache toka kwa mama mbwa (Ambaye hajachanjwa)
4. Msongo/Stress (Kuachishwa ziwa, Lishe duni, Msongamono, Minyoo)

Ila Mbwa wenyeji, asilia(Locals) wameonyesha kua wastahimilivu kwa kutokusumbuliwa na ugonjwa huu, Mbwa dume wameonekana kuugua zaidi kuliko Majike.
Ugonjwa huu unaweza kukaa kwenye mazingira kuanzia miezi miwili (2) mpaka mwaka.

Aina ya Ugonjwa.
Ugonjwa huu upo katika Namna mbili.
1. Athari za Moyo (Cardiac form) - hushambulia Zaidi watoto walioko tumboni na walioko chini ya wiki sita. Mara nyingi vifo hutokea pasipo dalili kuonekana.
2. Athari za Kwenye Utumbo(Enteric form)- Aina hii ndio maarufu zaidi, huwapata wa rika zote na kuambatanishwa na dalili kama za kutapika na kuaharisha wakati mwingine Damu.

NAMNA YA KUENEA/KUSAMBAA/KUAMBIKIZWA.

Mbwa hupata maambukizi kwa kula,kulamba kunusa Mavi yenye wadudu, sakafu au vyombo vilivyo na wadudu (Contaminated)

Wadudu hawa (virus) hutolewa na mnyama siku 4-5 baada ya kupata maambukizi (mara nyingi kabla ya Kuonyesha dalili), kipindi chote cha ugonjwa na siku 10 baada kupona.

NB: Mbwa anaweza kueneza wadudu wa ugonjwa hata kabla kuonyesha dalili.

DALILI ZA PARVO

IMG_5630.JPG

Dalili huanza kuonekana siku 5-7 baada ya Maambukizi (Wastani wa siku 2-14)
Dalili za mwanzo kabisa ni
1. Kokosa hamu ya kula (hali)
2. Mnyonge sana
3. Homa
Baadae masaa 24-48
Huanza
1. Kuharisha,Kuaharisha choo kilichochanganyikana na damu au Damu yenyewe na chenye Harufu kali/Mbaya.
2. Kutapika
Katika hatua hii joto la mwili hupungua.

UTAMBUZI WA UGONJWA.

Historia ya kutokuchanjwa Parvo husaidia kung’amua na hii huambatana na Dalili za kuharisha na kutapika.

Utambuzi wa kimaabara kwa kuchukua sampuli za choo, damu, mkojo (ELISA,PCR nk).

KINGA.

IMG_5635.JPG

Kuna njia kuu moja ya kukinga mbwa dhidi ya Ugonjwa huu nayo ni CHANJO.
Chanjo hutolewa katika mtiririko hufwatao na hutolewa kama umoja (Parvo) au katika muunganiko (Distamper & Parvo (DP) au Distamper, Hepatitis, Leptospirosis na Parvo virus, Parainfluenza combination (DHLP+))

1. Akiwa na wiki 4/6 tangu kuzaliwa
2. Akiwa na wiki 8/9 tangu kuzaliwa
3. Akiwa na wiki 12 tangu kuzaliwa

Baada ya hapo Utaratibu hufuatwa kwa maelekezo ya Daktari, mara nyingi ni kila baada ya miezi 6, mwaka au miaka 3.

Njia nyingine ni Usafi wa banda lako, Kupunguza Msongamano wa mbwa, na kuwapa lishe bora (Njia hizi ni za kupunguza tu ila Maambukizi yanaweza kutokea).

Ni vyema kuchanja kwa kutumia chanjo muunganiko hasa wa DHLP+ au DP, Maana Distamper na Leptospirosis ni Magonjwa pia hatarishi kwa Uhai wa Mbwa.

TIBA

IMG_5636.JPG

Ugonjwa huu hauna tiba mpaka sasa.
Habari Njema ni kwamba, ukiwahi kupata huduma (Kumuona daktari) mnyama wako anaweza kuepuka kifo.

Mara nyingi kama sio zote hupewa matibabu shirikishi ili kupunguza Athari za ugonjwa kwa mnyama lakini sio kuua virusi vya Parvo.

1. Kuongezewa Maji (Normal saline) maana mnyama hupoteza maji kutokana na kuharisha na kutapika.
2. Dawa za kuzuia kutapika na kuarisha
3. Chakula laini (uji uji, Supu hasa ya kuku imeonyesha ufanisi zaidi)
4. Sindano/Vidonge (Antibiotics) kwa ajili ya kuzuia Magonjwa Nyemelezi kama atakua anaharisha damu ama itakavyoelekezwa na Daktari.

Kumuhudumia mnyama mwenye “Parvo” ni jukumu zito, na lenye kuchukua muda, gharama na bado haimaniishi Atapona, maana yote yanayofanyika ni kumuwezesha Mnyama Kupata Nguvu ya kustahimili na kupambana na wadudu hao wa Parvo.
Kadiri huduma inavyofanywa mapema ndivyo Asilimia za kupona zikua kubwa.

MATUNZO BAADA YA KUPONA
Mnyama anapokua ametoka kwenye ugonjwa huu anakua mdhaifu(kinga inakua chini) na anaweza kupata Maambukizi mapya ambayo yanaweza kua hatari zaidi ya mwanzo kwa hiyo ni vyema...

1. Kumtunza eneo lisilo na msongamano wa Mbwa
2. Apate chakula kilaini mpaka atakapoimarika.
3. Mazingira yasafiashwe kwa Viatilifu (jik, 1:30).
4. Hakikisha mbwa wanaochangamana naye wamechanjwa Parvo.

YA KUZINGATIA
Hakikisha Mbwa wako wanapata chanjo ya Parvovirus na zingine zote zilizo Muhimu ikiwemo ya kichaa cha Mbwa.

Watunze Mbwa katika hali ya Usafi, Lishe Bora na Epuka Msongamano.

Hakikisha Unamchanja Mama mbwa kabla au wakati ana mimba ili kuongeza kiwango cha kinga watakachopata watoto pindi wakizaliwa.

Wachanje Watoto wa Mbwa pindi tu wanapotimiza Umri wa wiki 4/6, 8/9 na 12.

Wasiliana na Daktari wa Wanyama Mara pale tu unapoona Mbwa hayupo kawaida
Binadamu pia Huugua Parvo (Parvovirus B19), ila USIOGOPE Mbwa SIO chanzo cha maambukizi Kwa Binadamu.

kwa Ushauri, Chanjo na Matibabu
Sipy Vet.centre (Kanyama, Kisesa Mwanza)
+255 625 753 791
 
View attachment 1084736

Kama unataka/Unapenda kufuga Mbwa hasa wakigeni (Wakizungu) basi huna budi kuujua ugonjwa huu na namna ya kuepuka.

Kwa wale Wapenzi wa Mbwa kindaki ndaki, Wanaofuga Mbwa kwa Mapenzi au Kibiashara Wanajua Shuguli yake,
Akifika na Hujajiandaa atakuachia Historia tu.,

Canine Parvovirus Infection(CPV) alimaarufu kama Parvo, ni Ugonjwa hatari, unaoshambulia haraka, na ndio moja ya sababu kuu ya vifo vingi vya utotoni kwa watoto mbwa.

Ugonjwa huu ni Ugonjwa wa Virusi.
Mbwa watoto (wiki 4-24 yaani mwezi 1-6) na wale Wasiochanjwa wapo katika hatari zaidi ya kuugua.

MAMBO HATARISHI
1. Mbwa wa Jamii hizi (Doberman Pinschers, Rottweiler, American Pit bull Terriers, English Springer Spaniels na German Shepherds) zipo katika hatari zaidi kuliko jamii zingine.
2. Mbwa wasiochanjwa
3. Watoto Kupata kinga kidogo/uchache toka kwa mama mbwa (Ambaye hajachanjwa)
4. Msongo/Stress (Kuachishwa ziwa, Lishe duni, Msongamono, Minyoo)

Ila Mbwa wenyeji, asilia(Locals) wameonyesha kua wastahimilivu kwa kutokusumbuliwa na ugonjwa huu, Mbwa dume wameonekana kuugua zaidi kuliko Majike.
Ugonjwa huu unaweza kukaa kwenye mazingira kuanzia miezi miwili (2) mpaka mwaka.

Aina ya Ugonjwa.
Ugonjwa huu upo katika Namna mbili.
1. Athari za Moyo (Cardiac form) - hushambulia Zaidi watoto walioko tumboni na walioko chini ya wiki sita. Mara nyingi vifo hutokea pasipo dalili kuonekana.
2. Athari za Kwenye Utumbo(Enteric form)- Aina hii ndio maarufu zaidi, huwapata wa rika zote na kuambatanishwa na dalili kama za kutapika na kuaharisha wakati mwingine Damu.

NAMNA YA KUENEA/KUSAMBAA/KUAMBIKIZWA.

Mbwa hupata maambukizi kwa kula,kulamba kunusa Mavi yenye wadudu, sakafu au vyombo vilivyo na wadudu (Contaminated)

Wadudu hawa (virus) hutolewa na mnyama siku 4-5 baada ya kupata maambukizi (mara nyingi kabla ya Kuonyesha dalili), kipindi chote cha ugonjwa na siku 10 baada kupona.

NB: Mbwa anaweza kueneza wadudu wa ugonjwa hata kabla kuonyesha dalili.

DALILI ZA PARVO

View attachment 1084737

Dalili huanza kuonekana siku 5-7 baada ya Maambukizi (Wastani wa siku 2-14)
Dalili za mwanzo kabisa ni
1. Kokosa hamu ya kula (hali)
2. Mnyonge sana
3. Homa
Baadae masaa 24-48
Huanza
1. Kuharisha,Kuaharisha choo kilichochanganyikana na damu au Damu yenyewe na chenye Harufu kali/Mbaya.
2. Kutapika
Katika hatua hii joto la mwili hupungua.

UTAMBUZI WA UGONJWA.

Historia ya kutokuchanjwa Parvo husaidia kung’amua na hii huambatana na Dalili za kuharisha na kutapika.

Utambuzi wa kimaabara kwa kuchukua sampuli za choo, damu, mkojo (ELISA,PCR nk).

KINGA.

View attachment 1084738

Kuna njia kuu moja ya kukinga mbwa dhidi ya Ugonjwa huu nayo ni CHANJO.
Chanjo hutolewa katika mtiririko hufwatao na hutolewa kama umoja (Parvo) au katika muunganiko (Distamper & Parvo (DP) au Distamper, Hepatitis, Leptospirosis na Parvo virus, Parainfluenza combination (DHLP+))

1. Akiwa na wiki 4/6 tangu kuzaliwa
2. Akiwa na wiki 8/9 tangu kuzaliwa
3. Akiwa na wiki 12 tangu kuzaliwa

Baada ya hapo Utaratibu hufuatwa kwa maelekezo ya Daktari, mara nyingi ni kila baada ya miezi 6, mwaka au miaka 3.

Njia nyingine ni Usafi wa banda lako, Kupunguza Msongamano wa mbwa, na kuwapa lishe bora (Njia hizi ni za kupunguza tu ila Maambukizi yanaweza kutokea).

Ni vyema kuchanja kwa kutumia chanjo muunganiko hasa wa DHLP+ au DP, Maana Distamper na Leptospirosis ni Magonjwa pia hatarishi kwa Uhai wa Mbwa.

TIBA

View attachment 1084739

Ugonjwa huu hauna tiba mpaka sasa.
Habari Njema ni kwamba, ukiwahi kupata huduma (Kumuona daktari) mnyama wako anaweza kuepuka kifo.

Mara nyingi kama sio zote hupewa matibabu shirikishi ili kupunguza Athari za ugonjwa kwa mnyama lakini sio kuua virusi vya Parvo.

1. Kuongezewa Maji (Normal saline) maana mnyama hupoteza maji kutokana na kuharisha na kutapika.
2. Dawa za kuzuia kutapika na kuarisha
3. Chakula laini (uji uji, Supu hasa ya kuku imeonyesha ufanisi zaidi)
4. Sindano/Vidonge (Antibiotics) kwa ajili ya kuzuia Magonjwa Nyemelezi kama atakua anaharisha damu ama itakavyoelekezwa na Daktari.

Kumuhudumia mnyama mwenye “Parvo” ni jukumu zito, na lenye kuchukua muda, gharama na bado haimaniishi Atapona, maana yote yanayofanyika ni kumuwezesha Mnyama Kupata Nguvu ya kustahimili na kupambana na wadudu hao wa Parvo.
Kadiri huduma inavyofanywa mapema ndivyo Asilimia za kupona zikua kubwa.

MATUNZO BAADA YA KUPONA
Mnyama anapokua ametoka kwenye ugonjwa huu anakua mdhaifu(kinga inakua chini) na anaweza kupata Maambukizi mapya ambayo yanaweza kua hatari zaidi ya mwanzo kwa hiyo ni vyema...

1. Kumtunza eneo lisilo na msongamano wa Mbwa
2. Apate chakula kilaini mpaka atakapoimarika.
3. Mazingira yasafiashwe kwa Viatilifu (jik, 1:30).
4. Hakikisha mbwa wanaochangamana naye wamechanjwa Parvo.

YA KUZINGATIA
Hakikisha Mbwa wako wanapata chanjo ya Parvovirus na zingine zote zilizo Muhimu ikiwemo ya kichaa cha Mbwa.

Watunze Mbwa katika hali ya Usafi, Lishe Bora na Epuka Msongamano.

Hakikisha Unamchanja Mama mbwa kabla au wakati ana mimba ili kuongeza kiwango cha kinga watakachopata watoto pindi wakizaliwa.

Wachanje Watoto wa Mbwa pindi tu wanapotimiza Umri wa wiki 4/6, 8/9 na 12.

Wasiliana na Daktari wa Wanyama Mara pale tu unapoona Mbwa hayupo kawaida.

Binadamu pia Huugua Parvo (Parvovirus B19), ila USIOGOPE Mbwa SIO chanzo cha maambukizi Kwa Binadamu.

Imeandaliwa
Dr. Godwin. Z. MKAMI, DVM
Veterinary Surgeon.
Sipy Vet.centre (Mbuyuni kinyerezi, DSM)
+255 764 667 503
Huuu ugonjwa ulikuwa GERMAN SHEPHERD wangu. Siku iyo, tumenunua dawa ya 50,000 na ndio Mbwa alikufa ili niuma Sana, mwaka 2007.
Tsh 50,000 ilikuwa pesa mingi
 
Pole sana mkuu, kweli kwa miaka hiyo ilikua Pesa nyingi sana! Ugonjwa huu unaitaji Umakini na ni wakutazamwa kwa jicho la pekee!!
 
Back
Top Bottom