Mwamba028
JF-Expert Member
- Nov 15, 2013
- 4,595
- 3,670
Mkuu uko vizuriPole sana mkuu, huo ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu aitwaye kwa jina la kienyeji "dondoa".
Mdudu huyo hutoboa matunda yakiwa machanga na ana sumu ambapo akishatoboa hukojolea hiyo sumu na kusababisha tunda lioze kwenye sehemu iliyotobolewa au kuozesha tunda zima.
Kama halikuoza lote, litaoza sehemu iliyotobolewa na hiyo sehemu husinyaa na sehemu zingine huendelea kukua hivyo tunda huwa na mkunjo flani.
Wadudu hawa huishi kwenye miti hususani mikuyu, miembe nk.
Wadudu hawa ni waharibifu sana kwenye matunda hivyo dawa za sumu kali na zenye harufu huwakimbiza shambani mfano Selecrone ni dawa mojawapo unapaka kwenye pamba au vipande vya godoro na kusimika shambani kila mahali.
Pia kuna mitego ya kuwanasa ambayo hutundikwa at least mitego 6 kwa ekari moja na kila mtego ni shs 5000.
Hiyo mitego ipo kama chocolate inawa attract hao wadudu wanapoingia tu hukutana na sumu na kufa hapo hapo.
Wauzaji wa hiyo mitego nawafahamu waliopo Arusha.
Pole sana mkuu
Naomba ufafanuzi kwenye hili
Mimi nimeanza kilimo cha nyanya ila ile sehemu nayotaka kupandikiza miche kuna miti ya mikorosho miwili, Je inaweza kuleta shida yoyote ya magonjwa au wadudu kwa nyanya zangu?
Ahsante.