Ugonjwa huu wa kuku nawezaje kuudhibiti?

Political stability

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2021
Posts
906
Reaction score
1,401
Huu ugonjwa unaitwaje?

Unasabishwa na nini?

Na jinsi gani naweza kuudhibiti?

IMG_20210813_081910.jpg
IMG_20210813_081658.jpg
 
Hiyo ndui rafiki. Au fowl pox kwa kiingereza. Unaweza kuithibiti kwa chanjo kabla haijaingia tumia chanjo inaitwa "tatu moja" ambayo pia inadhibiti magonjwa mengine kila baada ya miezi minne hii unawaekea tone moja jichoni. Pia kuna chanjo ya ndui ya ndege pekee ambayo unachovya unamtoboa kwenye bawa katikaki ambapi hapana mfupa.
 
Sasa kama wameshapata wapatie lishe kizuri. Hakikisha umewapa majani mabichi au mamboga mboga au weka vitamini kwenye maji au vyote kwa pamoja itasaidia wakue vizuri na wasidumae.
 
Hiyo ndui rafiki. Au fowl pox kwa kiingereza. Unaweza kuithibiti kwa chanjo kabla haijaingia tumia chanjo inaitwa "tatu moja" ambayo pia inadhibiti magonjwa mengine kila baada ya miezi minne hii unawaekea tone moja jichoni. Pia kuna chanjo ya ndui ya ndege pekee ambayo unachovya unamtoboa kwenye bawa katikaki ambapi hapana mfupa.
Hii ya matone, nawapa baada ya mda gani, baada ya kutotolewa
 
Kuanzia wakiwa na siku saba unaweza kuwapatia ikiwa eneo lako wanapata kwa kasi. Lakini wengi wanashauri wakiwa na siku 14.
 
Hiyo ndui rafiki. Au fowl pox kwa kiingereza. Unaweza kuithibiti kwa chanjo kabla haijaingia tumia chanjo inaitwa "tatu moja" ambayo pia inadhibiti magonjwa mengine kila baada ya miezi minne hii unawaekea tone moja jichoni. Pia kuna chanjo ya ndui ya ndege pekee ambayo unachovya unamtoboa kwenye bawa katikaki ambapi hapana mfupa.
Chanjo ya tatu moja inauzwaje madukani kaka?
 
kwa Dar es salaam haizidi 7000-10000 ila kwa sasa kumekuwa na cases ya pox kutokea hata ikichanjwa. kuna ile ya pox pekeyake ambayo unatoboa kwenye bawa nayo bei ni kati ya 12 mpaka 15 ni ya uhakika zaidi.
 
Nashukuru mkuu, na vipi kuhusu mdondo, hii tatu moja ni nzuri au bora ile ile ya mwanzo inayokua peke yake?
 
Kwa uhakika tumia TU chanjo za zamani, maana kama tatu 1 imefeli kwenye ugonjwa wa Ndui, Imani ya kwamba kwenye magonjwa mengine itafanya vizuri tunaitoa wapi

Tatizo wafugaji waliona kama tatu 1 inawapunguzia gharama ila kumbe rahisi aghari, unanunua Chanjo elf 9 alafu unakuja kuhangaika na kutibu Ndui Kwa elf 15
 
Poa mkuu, nashukuru
 
Achana na chanjo ya tatu moja.
Haitasaidia chochote. Tumia chanjo ta zamani sema umechelewa maana ugonjwa umeshaingia.

Huo ugonjwa itakubidi utumie muda wa ziada kukaa karibu na vifaranga kiufupi vifaranga watakuwa wanakufa kimoja au 2 kwa siku mwishowe hata kma ni vifaranga 200 vitakufa vyote.

Jitihada binafisi. Chakula, madawa, maji, uangalizi.

Ponapona yako labda kama kuku ni wakubwa ni rahsi sana kupona

Mafuta ya maziwa uwe unawapaka kwenye vidonda..
 
Back
Top Bottom