Ugonjwa usiojulikana waibuka Kongo na kuua watu zaidi ya 50

Ugonjwa usiojulikana waibuka Kongo na kuua watu zaidi ya 50

Kwa mujibu wa ofisi ya WHO barani Afrika, mlipuko wa kwanza katika mji wa Boloko ulitokea baada ya Watoto watatu kula popo na kufariki ndani ya saa 48 baada ya kuonesha dalili za homa na kutokwa na damu.
Hawana wanyama wengine wa kula?
 
madaktari wa ukanda huo wanalipwa kujenga hofu kwa watu wapakimbie au wasiende ili waibe madini vzr , tangu nakuwa nasikia ugonjwa mpya DRC , mpk ss sikuwai juwa yameishia wap hayo magonjwa
Mkulu, sina uhakika wa madai kwamba madaktari wanalipwa, lakini nakubaliana na ww kuwa upo uwezekano mkubwa hizi ni njama za kujenga hofu na hatimae watu wakimbie maeneo yao-haswa.

Ila utasikia watu wakitolea lawama watu wa huko na sio watu kutoka nje ya mucongo.
 
Hawagundua kuwa ni nyama
Mimi nafikiri nchi zetu hizi za Africa na dunia ya tatu zikianza kugonga population ya watu milioni 100 unaanza kuona mambo ya ajabu ya vita, umasikini wa kutupwa, ujinga wa ajabu, ugaidi, kulakula vitu ovyo, magonjwa ya ajabu.

Huku ndiko hata Tanzania inaelekea.
 
Ugonjwa wa ajabu usiojulikana umeua zaidi ya watu 50 ndani ya saa chache baada ya kuanza kwa dalili zao huko Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Tovuti ya Daily Mail imeripoti Jumanne Februari 25,2025, kuwa takriban watu 419 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo, huku kukiwa na vifo 53, tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipoanza nchini DRC mnamo Januari 21.

“Hilo ndilo linalotia wasiwasi zaidi,” amesema Serge Ngalebato, ambaye ni Mkurugenzi wa Matibabu wa Hospitali ya Bikoro ambacho ni Kituo cha Ufuatiliaji cha kikanda.

Screenshot 2025-02-26 000412.png
 
Back
Top Bottom