Ewaaaaaaa saaafi sana, Nina mwaka maybe wa nane au kumi napambana nayo but Mungu anasaidia. Nimeweza kufanya yafuatato:
1. Nakula mapema sana kati ya saa nane na saa kumi Jioni, kwahio Nina Milo miwili tu breakfast na late lunch, baaasi!
2. Usiku nakunywa juice fresh ya parachichi na embe lililoiva sana, ukipata ambalo halijaiva imekula kwako
3. Nakula papai, hii inaisaidia saaana sanna Kwa upande wangu Mimi huyu ni mkombozi, hata Sasa nimetoka kula papai
4. Nakunywa maji ya kutosha usiku
5. Nikiona nimeharibu ratiba yangu either nikiwa Safarini au pengine nikiwa sherehe au kampani na jamaa mkala late kidogo BASI kwenye Bag langu la PC sikosi Magnesium (hizi natafuna mnooooo, juzi nimenunua magnesium nzuri sana, ikabidi ninunue za buku nne, Hadi muuzaji akashangaa.
Matokeo yake
1. Nalala bila kupata heartburn
2. Sipaliwi Tena usingizini
3. Sikoromi Tena usiku
4. Napata choo bila kutumia nguvu
Changamoto
1. Kuna siku kama Leo nimekula mapema zaidi, saa nane kasoro, muda huu nimekula papai na juice, yaani night itakua ndefu kuanzia saa Tisa hivi......
Hii ndio niliyofanya lakini pia ukipata TANGO ni nzuri kama utalila bila kuweka vitu vingine, yaani ule tango kama TANGO, haya ni Kwa upande wangu