Ugonjwa wa Acid Reflux uwe janga la kitaifa

Kuna ugonjwa mwingine una itwa GASTRITIS.

Ebwana eeeh ni balaaa upo kama vidonda vya tumbo ila nahisi huu ni balaa zaidi ya hivyo vidonda vya tumbo.

Mwenyezi Mungu atusaidie tuu.
 
Mimi ninapambana nacho zaidi ya 5 years now
Pole sana kiongozi, ulifanikiwa kupata matibabu au bado tatizo linakusumbua?

Mimi nafahamu dawa za mimea, ukipenda naweza kukuandalia.

Kiujumla Kwa yoyote mwenye tatizo la PEPTIC ULCERS, GERD, GASTRITIS dawa zake nazifahamu.

Naweza kumuandalia atakaependa. Utalipia tu 10,000Tshs kwa kuwa nitatumia muda na fedha kuandaa dawa hizo.

Aghalabu hiyo dawa utakayolipia 10,000Tshs huwa inatosheleza kwa matibabu mpaka kupona, mara chache kuhitajika dozi ya pili isipokuwa kwa tatizo lenye athari za muda mrefu.

Nakutakia afya njema.
 
Piga Tikiti Mzee utakuja nishukuru
 

Serikali haiwezi kutatua hili tatizo kwasababu ni utamaduni mbaya ndiyo chanzo. Sasa mtu anakula saa moja kabla ya kwenda kulala ni lazima atakuwa na acid maana acid kazi yake kubwa ni kuyeyusha chakula sasa lazima utapata acid. Kama hauli vyakula vyenye alkaline utapata acid

Haya ni matatizo lakini kwa wengi ni utamaduni wa kula ndiyo chanzo
 
Ni miaka mitatu napambana nayo mkuu , usiombe ikukamate boss , utaona kijijini kwenu kuchungu
Pole sana kiongozi, pamoja na kuzingatia mtindo wa maisha rafiki kama baadhi ya wadau walivyochangia, unaweza pia kutumia vitu hivi ni vizuri sana kwa tatizo la ACID REFLUX/KIUNGULIA:

i) Manjano - Unatumia unga wake kijiko kimoja cha chai mara mbili kwa siku kwenye chai au maji ya vuguvugu.

Ukiweza kupata pilipili manga ni bora zaidi unanyunyizia kidogo sana (0.4g), inasaidia manjano kuweza kufyonzwa na mwili kwa ufanisi zaidi.

N.B : Kama unatumia dawa nyingine yoyote ni vizuri kupata ushauri wa daktari kabla ya kutumia na (i) hapo juu.

ii) Kabichi - Unaisaga na kuitumia kama juisi, glasi moja (~ 100ml) asubuhi kabla ya kula chochote.
Kama ni tatizo ni kubwa sana unaweza kutumia kabla ya chakula cha mchana pia.

Manjano na Kabichi pia hutumika kwa tatizo la vidonda vya tumbo na gastritis.

Nakutakia matibabu mema.
 
Hii imeeleweka sana nahitaji kujaribu pia naona kwenye comment watu wanatoa ushuhuda mzuri juu ya matumizi ya apple cider vinegar pamoja na Bataine hcl hapa ndo nilipoachwa. msaada kwa tanzania nazipataje hizi material
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…