SoC02 Ugonjwa wa Afya ya Akili upo

SoC02 Ugonjwa wa Afya ya Akili upo

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 3, 2022
Posts
27
Reaction score
18
Habari ndugu mwana Jamii Forums,Umewahi kusikia kuhusu Ugonjwa wa Afya ya Akili?,pengine labda ukahisi ni kitu kidogo au Cha kawaida,hapana kina madhara makubwa hasa kwa utendaji kazi kiufanisi.Kwani ugonjwa Afya ya Akili ni nini?,Ugonjwa Afya ya Akili unatafsiriwa kwa maana tofauti kulingana na mazingira na historia ya muhusika lakini kiufupi ni msongo wa mawazo.

Vitu vinavyopelekea mtu akapata ugonjwa wa Afya ya Akili ni vitu vingi,tuangalie vile ambavyo vinapelekea mara kwa mara.

Ukosefu wa kipato unachotaka kukipata,hii inapelekea mtu kuwa na msongo wa mawazo ukiangalia vijana wenzio wanafanikiwa wewe Bado uko chini,mawazo yanapelekea kuwa na msongo na hata kupata ugonjwa wa Afya ya Akili.

Sababu ya pili ni Mahusiano,hii imekuwa janga kubwa kwa vijana na wazee,Mahusiano ya familia na ya mapenzi kama Kuna migogoro ni lazima mtu atapata shida ya msongo wa mawazo na kupelekea Akili kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.labda nyumbani huelewani na ndugu au familia haikuelewi na pengine kwa mpenzi wako hakuelewi Yale mawazo yanapelekea Akili kutokuwa sawa.

Sababu ya tatu ni Unyanyasaji na ukatili;unanyanyaswa,unafanyiwa ukatili, utakuwa sawa?,Nitolee mfano mwaka 2016 nilikuwa Arusha niliishi na familia ya jirani tulieishi nyumba Moja alikuwa na watoto wawili na ndugu wawili wa mumewe,ndugu mmoja ni wakike mwingine wakiume,hapa nawaongelea wote kwa makundi ,nianze na wakike; saa 10 asubuhi awe macho kuwaandalia watoto chai na maji na kufanya usafi wa nyumba,na mda wa watoto kuamka awaandae waende shule.ana miaka kumi na mbili na aliacha shule kwa kutaka yeye sababu alikuwa anabakwa na kijana mkubwa wa hapo shuleni,nilijuaje anabakwa?mama aliekuwa anaishi nae pindi mtoto alikosea tusi lake kubwa ndomana ulibakwa.

Huyu Binti alikuwa mnyonge sana nikaamua kumuuliza historia yake na alikuwa hayuko sawa kiakili yaani hajatulia,kumuuliza historia alibakwa na wazazi wakalipwa pesa wakakaa kimya na akaamua kuacha masomo sababu walitaka kumuoza kwa aliyembaka,na anajichukia na anataka kufa TU na ni mtoto wa miaka 12 lakini kaishia tishia kujiua mara nyingi.nikamsihi sana na kila siku nilikuwa namsifia kuwa yeye ni Binti mzuri na atakuja kuwa na maisha mazuri na ana thamani. Baadae niliona kabadilika unyonge umeisha na kazoea kufokewa na anajua Iko siku yataisha,lakini kwanini turuhusu Unyanyasaji na ukatili uharibu Afya zetu?.

Sijamaliza nirudi kwa huyu wa kiume yeye hataki kuzungumza na mtu na Haelewi anachofanya na ni mkimya sana na ukichunguza ni ugonjwa wa Akili sababu ya vipigo.nani katuroga?,piga mtoto kwa kiasi na usimpe maneno mabaya.

Athari za ugonjwa wa Afya ya Akili.
Kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.
Kukosa usingizi na kupelekea kuumwa.
Kuwa na hasira kupita kiasi.
Kutamani kujidhuru na kujiua kabisa na hata kudhuru wengine,na vingine vingi.

Tunaepukaje?Pinga ukatili na Unyanyasaji,ongea na vijana na rika zote,kama ni wanandoa na mna watoto jitahidi mgombane pembeni mtoto asiwaone na Kaa na watoto wape elimu ya maisha na kingine vijana wengi tunatamani kufikia ndoto zetu tupambane ndio,lakini kwa kiasi tukiamini Iko siku.fanya mazoezi,kula vizuri na unapopata muda Kaa na watu.

Ugonjwa wa Afya ya Akili unatibika-: unapogundua hauko sawa muone daktari Kuna njia za kutumia unapona kabisa.

13-8-2022
Binti Mzalendo.
 
Upvote 3

Tatizo la ugonjwa wa afya ya akili, HUWA MUHUSIKA HANA PANAPOMUUMA na WALA YEYE HAJIJUI KAMA ANA TATIZO HILO..!!!
NB: Kichaa huwa haendi hospitali yeye mwenyewe, walio wengi hupelekwa na tena wengine wakiwa wamefungwa kama
 
Back
Top Bottom