Ugonjwa wa akili upo na unawatesa watu

Ugonjwa wa akili upo na unawatesa watu

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Tunakubali na kuruhusu mawazo ya watu wachache wagonjwa kuleta tafarani kwenye hoja za msingi kwa ajili ya wengi.

Hakuna kipindi bora cha maisha kama kipindi hiki lakini hakuna kipindi chenye upuuzi kama kupindi hiki. Tunaishi kwenye dunia ambayo mtu anayezungumza pumba anaonekana mwenye akili kuliko mtu mwenye utimamu.
1744398031546.jpg

Tunaishi kwenye dunia ambayo vyombo vya habari vinahangaika kutafuta taarifa na habari kutoka vyanzo ambavyo ni vyanzo vya kijinga sana. Huku wakiacha kuangazia mambo ya msingi.

Tunaishi kwenye dunia ambayo usipokuwa makini na damu yako basi dunia itakusaidia kumlea na kumfanya mtoto wako kuwa mtu wa ajabu kuwahi kutokea. Tunaishi kwenye dunia ambayo matendo machafu na mabaya ndio yanapewa kipaumbele.

Tupo na watu ambao wanatoa matamko ya kipuuzi kila wakati tena pasipo kuwa na sababu za msingi. Kila siku wajinga wanakuwa wengi kuliko watu wenye utimamu.
1744398031546.jpg


TUKUBALI TUKATAE ILA DUNIANI TUNAISHI NA WATU WAGONJWA WA AKILI KWA KIWANGO KIKUBWA SANA.
 
Issue ya msingi ni kuchukua yale ambayo yanakufaa na kupuuza mengine. Chamsingi ni kuwa karibu na watu wako wa karibu kuwaepusha na unayoyaona hayafai kwao kwa wakati huo
 
Hii haina tofauti na kumpa pesa mwanamke na hakudai.

Hili nalo ni tatizo la akili.
 
Back
Top Bottom