Ugonjwa wa Hanta virus unasambaa na kuendelea kuua watu kwenye meli ya kitalii

Ugonjwa wa Hanta virus unasambaa na kuendelea kuua watu kwenye meli ya kitalii

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Picha zilizopatikana na shirika la habari la Associated Press za meli ya kitalii iliyo katikati ya mlipuko wa virusi adimu zinaonyesha sitaha (decks) zilizo tupu na maeneo ya pamoja yasiyo na watu, timu za matibabu zikiwa na mavazi ya kujikinga, na mandhari tulivu mbele wakati meli hiyo na karibu abiria na wafanyakazi 150 walipoendelea kusubiri kwa siku nyingine baharini karibu na pwani ya Afrika Magharibi.

Abiria watatu wamefariki dunia na angalau watu wanne wameugua katika kile maafisa wa afya wanasema ni mlipuko wa virusi vya hantavirus, ambavyo kwa kawaida huenea kwa kuvuta hewa yenye uchafu unaotokana na kinyesi cha panya. Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema abiria wanajitenga katika vyumba vyao.
GettyImages-2273814127-645x645.jpg

Kampuni inayoendesha meli hiyo — ambayo kwa sasa imesimama kwenye Bahari ya Atlantiki karibu na Cape Verde — imesema inapanga kuihamisha hadi Visiwa vya Canary vya Hispania baada ya watu watatu kuhamishwa kitabibu na kupandishwa kwenye ndege maalum kuelekea Uholanzi. Mapema Jumanne, maafisa wa Hispania walisema wanafuatilia hali hiyo lakini bado hawajafanya uamuzi.
Meli ya MV Hondius, meli ya Uholanzi ya safari ndefu za polar, iliondoka Aprili 1 kutoka Argentina kuelekea Antaktika na visiwa kadhaa vilivyotengwa vya Bahari ya Atlantiki Kusini.



Nchi kadhaa zimekataa kuipokea meli hiyo ili kuepusha ugonjwa huo kusambaa mitaani.
Kwa sasa hantavirus haina matibabu wala chanjo. Ni ugonjwa hatari na sasa watu walio ndani ya meli wanaomba msaada kwa sababu wanaishi kwa hofu huku abiria watatu wameshafariki tayari na ugonjwa unaendelea kusambaa

Meli yenyewe hii hapa
Screenshot_20260506-105810.png
Screenshot_20260506-105755.png
 
 
 
Mavirusi mengine ni biological weapons tu , ili kuindoa utulivu sehemu zilizo na rasilimali adhimu, ukilink vita hapo gongo mlipo wa ebola na Measles kuna mambo yanaendelea sio bure🤔
 
Mavirusi mengine ni biological weapons tu , ili kuindoa utulivu sehemu zilizo na rasilimali adhimu, ukilink vita hapo gongo mlipo wa ebola na Measles kuna mambo yanaendelea sio bure🤔
Sema safari hii huu ugonjwa unawamaliza wazungu wenzao kwenye meli
 
Misheni imefeli kuwafikia panya wa maabara😅
Wananchi wao wanajadiliana mtandaoni kuwa bora waizamishe meli ugonjwa usiende kusambaa mitaani
Wamefanikiwa kumleta mgonjwa mmoja Africa. Anapewa matibabu hapo South Africa
 
Back
Top Bottom