hivi ugonjwa wa kifafa unatibika kweli? maana ninamdogo wangu kaugua kifafa akiwa na umri wa miaka 24.
Pole sana mkuu
NIKIMU ... kwa kweli kifafa ni tatizo gumu sana si kwa mgonjwa tu, hata familia (ndugu na marafiki). Kifafa kipo kati ya magonjwa ya akili, kwa kuwa kina athari kwenye akili za muathirika. Labda nianze kwa kusema...kifafa mara nying ni 'dalili' ya ugonjwa, kuliko chenyewe kuwa ugonjwa. Kinapotokea kinaonyesha kuna tatizo ambalo limeathiri ubongo wa mhusika. Hivyo ukifika Hospitali lazima wachunguze kilichopelekea kifafa hicho.
Mara nyingi tatizo huwa kuathirika kwa ubongo kutokana na mambo mbali mbali (ajali, kansa, kiharusi (stroke), maambukizi (infections eg Meningitis etc), kwa watoto degedege kwa Cerebral Malaria, minyoo ya kitimoto (Tape worm Neuro-Cysticercosis hili tatizo linatokea sana siku hizi sababu ya kula kitimoto kisichopimwa), madawa au sumu, etc). Kati ya matatizo hayo, yapo yanayotibika na hivyo 'dalili' ya kifafa ikapotea kabisa...na yapo yasiyotibika. Ila mara nyingi tatizo linalosababisha kifafa linaweza lisijulikane ikaishia kuitwa tu 'kifafa (Epilepsy)'.
Matibabu ya Epilepsy mara nyingi ni dawa ambazo zinazuia au zinapunguza kupata epileptic attack i.e ile hali ya kupoteza fahamu, kuanguka, na kukakamaa, kujing'ata na kutoa haja ndogo au kubwa. Na pia kama mgonjwa ameathirika kiakili..basi kupewa dawa za magonjwa ya akili..lakini sio kwamba kinatibika kikaisha kisitokee tena..unless ni kifafa kinachosababishwa na ugonjwa Fulani na huo ugonjwa unatibika.
USHAURI: Mpeleke Muhimbili idara ya magonjwa ya akili karibu na wadi ya Sewa Haji pale atachunguzwa na kupewa huduma stahiki.