Hili tatizo linajulikana kama ubongo kusinyaa na kuganda.
Mtu mwenye tatizo hili hupatwa na dalili zifuatazo:
1. Anafanya mambo kama mtoto wa umri kati ya miezi ya mwanzo hadi mwaka (yaani haeleweki)
2, Wengine hupatwa na kifafa au degedege
3. Kupoteza fahamu
4. Kupoteza kumbukumbu
5. Fahamu zinakuwepo na kutoweka (ndani ya dakika 20 anaweza kuwa sawa na hapo hapo kumbukumbu hutoweka)
6. Wengine hufikia hatua ya kushindwa kutafuna chakula na kushindwa kumeza
7. Wengine hushindwa kuongea.
SABABISHO:
Wataalamu wa mishipa ya fahamu wanasema kuwa kuna mambo machache yanayoweza sababisha tatizo hili ikiambatana na lishe hafifu (wavivu wa kula):
1. Uvutaji wa sigara.
2. Unene au uzito wa kupitiliza
3. Presha ya juu
4. Tatizo la sukari kwenye damu
ANGALIZO:
Si kwamba mtu mwenye matatizo haya lazima apatwe na tatizo la ubongo kusinyaa.
NINI HUTOKEA KWA MGONJWA WA AINA HII?
Ubongo ukisinyaa hufanya mishipa ya fahamu kutofanya kazi vizuri na ndipo husababisha mtu kupoteza network. Kule kwenye ubongo damu, umeme, oxygen na protein vinakuwa havipiti vizuri, ndipo humfanya mtu kupooza maeneo ya viungo vya mwili, kupatwa na kifafa/degedege, mishipa kutotulia na kumfanya mgonjwa muda wote kuwa akichezesha aidha mikono au miguu kama vile anastuliwa na umeme.
NB: Ukiona ndugu au jamaa yako anabadilika tabia na kuanza kufanya hayo niliyoyaeleza tafadhali usipuuze na ukafikiri anajifanyisha. Wahi kumpeleka hospitali.
INASEMEKANA kuwa, tatizo hili huwapata zaidi wazee, lakini kwa sasa hata vijana huwapata.
TIBA:
Tiba hufanyika kwa kutibu tatizo kuu liopelekea mtu kupata ugonjwa huo (Mfano kama ni kisukari ndio sababu yake kupata tatizo hilo, basi mgonjwa hutibiwa sukari na kisha hupona = akiambatana na mlo sahihi, maji mengi sambamba na kukaa kwenye hewa safi, hewa safi ni chakula cha ubongo na pindi ubongo ukikosa oxygen hata kwa sekunde moja mtu hupoteza fahamu au kusikia kizunguzungu)
Pia kuna kwenda hospital na kutumia taknologia na wataalamu waliosomea maswala hayo.
UMRI WA KUISHI.
Mgonjwa huishi kwa miaka ya kawaida bila kuathiri umri kama atapatiwa matibabu na kubadili mwenendo wa maisha (Mfano kama ni kijana wa miaka 30 ataishi miaka mingi tu mpaka 60's) Yaani akipata matibabu basi haitakua sababu ya yeye kupungukiwa umri wake wa kuishi.
#Mungu amsaidie mzazi wako[emoji122]