Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

Pole Sana ndugu Yangu....
Sio Siri nimejisikia huzuni kubwa Sana baada ya kusoma thread yako nakuombea Kwa MUNGU ili akuponye ndugu Yangu naomba MUNGU afanye njia uweze kupata unafuu juu Hali yakoo!!
 
Kuna siku mtoto wangu wa miaka 2 alizidiwa na homa akiwa hospitali akawa kama anazimia, Daktari akamuwahi na dawa akaweka kwenye bomba la sindano akamuingizia kwenye haja kubwa alafu mtoto akatokwa na choo laini ndipo homa ikashuka.

Naomba kujulishwa kuwa ni dawa gani ilitolewa? Nauliza hivyo kwa sababu naona kama hii ni huduma ya kwanza ilitolewa, sasa ikitokea hivyo nikiwa mbali na hospital nafanyaje?

Naomba msaada kwa anayejua.
 
Kwanza mshushe chini mtandikie kitambaa kizito kama alikua kitandani

Ondoa vitu vyote unahisi vinaeza kumdhuru kumzunguka kama jiko la moto vitu vyenye ncha kali n.k

Mlaze kwa ubavu kuzuia asipaliwe na mate yake mwenyewe maana kwa kipindi anachopata degedege hawez kujisaidia kwa chochote

Legeza au ondoa nguo zote kuzunguka shingo na kichwa kuzuia kujivingirisha kati yake.

Kagua dalili zote za kupungukiwa na hewa mfano kuwa wa blue miguuni na mikononi .

Alafu kagua ni kwa mda gani mara nyingi degedege inayochangiwa na kuongezeka kwa joto(homa)."huisha yenyewe

Kingine dawa unayotaka kujua inatumika kwa dharura sana na sio kwa watoto wachanga inaitwa (diazepam) sio nzuri kwa matumiz ya nyumbani hasa ukiwa hauna huduma ya hewa na dharura maana ina tabia ya kupooza na kupunguza utendaji wa mfumo wa hewa na fahamu ivo ukitumia bila ushauri unaweza sababisha kifo kwa mtoto ivo usitumie bila medical prescription (iandikwe na kutolewa na wataalamu wa afya)
 
Kwanza mshushe chini mtandikie kitambaa kizito kama alikua kitandani

Ondoa vitu vyote unahisi vinaeza kumdhuru kumzunguka kama jiko la moto vitu vyenye ncha kali n.k...
Mkuu nashukuru sana kwa msaada wako, be blessed
 
Kwanza mshushe chini mtandikie kitambaa kizito kama alikua kitandani

Ondoa vitu vyote unahisi vinaeza kumdhuru kumzunguka kama jiko la moto vitu vyenye ncha kali n.k...
Vyema sana,
 
Habari Wadau,

Leo asubuhi nimejikuta katika wakati mgumu pengine kuliko siku yoyote ile,Nilikuwa nimekaa na mtoto wangu akawa ananiambia baba macho yanauma,mara kichwa kinaniuma nikamgusa akawa amechemka sana mwili,nikamwambia tulia nikupeleke hospitali..
Samahan naomba unisaidie alitibiwa kwa dawa gani maana mdogo wangu anateseka sana
 
Mwanangu ilimtokea miezi miwili iliyopita degedege, mkono wa kulia macho,mdomo, na mguu vyoote vilikakamaa.
Nilimsponji na maji jirani alileta majani fulani yanaitwa mifumbesi/ kifumbasi akamkandia baada ya dakika km moja hivi akakojoa.
Tukambeba kumpeleka hospitali.
 
Daah acha kabisa huo ugonjwa [emoji27][emoji27] kuna kifafa na degedege ni hatari sanaa
 
Ndugu yangu amezaliwa na kifafa,anaweza kupona?
ama nn dawa take?
Kwa utaalamu na ujuzi wa Tiba uliopo sasa, hauwezi kutibu moja kwa moja ugonjwa wa Kifafa ila unaweza kuratibu (management) athari za huu ugonjwa kwa muhusika.

Mgonjwa wa kifafa akifuata masharti vizuri ya kimatibabu na Clinic nzuri basi anaweza kuishi vizuri na kufanya shughuli zake kama kawaida.

Dawa za ku "manage" ugonjwa huu zipo aina tofauti tofauti na zinatofautiana ufanyaji kazi.
Inahitajika ushauri wa daktari na vipimo ili kujua ni dawa ipi nzuri kwa muhusika ambayo inampa matokeo mazuri.

NB: Mshauri aende clinic akafanye vipimo vya kutosha maana kuna aina tofauti za Kifafa na jinsi ya kuanza matibabu yake.
 
Habarini madaktari,

kuna best yangu anasumbuliwa na huo ugonjwa tajwa hapo juu kwa muda mrefu sasa. Stori ipo hivi wakati ana umri wa miaka 5 alipataga ajali ya kugongwa na boda maeneo ya kichwani ambayo yalimpelekea maumivu makali sana ya kichwa.

Sasa wakati yupo hospitali kuna sindano alichomwa ambapo kuna hali ilimtokea kama mtu mwenye kifafa lakini badae alikaa sawa na maisha yakaendelea.Wakati ana umri wa miaka 13 au 14 ndo hiyo hali ya kupoteza fahamu ikamuanza lakini ikapoa baada ya miaka miwili ikajirudia tena ikapotea baada ya miaka miwili ikajirudia hiyo hali na ndio inamsumbua hadi leo na amejitahidi sana kupata ufumbuzi ktk hospitali na waganga wa jadi lakini imeshindikana.

Ila kuna dawa wameandikiwa hospitali anameza kila siku ya maisha yake na asipo meza hiyo hali inamtokea.Sasa kuna daktari kamshauri aende muhimbili akafanye CT SCAN,jee akifanya hiko kipimo na tatizo likagundulika anaweza kurudi ktk afya yake kama zamani alivyozaliwa? NB. Hiyo historia ya ajali yake ni kwa mujibu wa maelezo ya wazazi wake na sasa jamaa yupo 30+.
 
Back
Top Bottom