Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

ni vigumu sana kuvumila mtoto akipatwa na shida yoyote
Mungu tu atupe neema yake , maana likitokea kuchanganyikiwa ni kawaida
Ukimuona mtoto akiwa kwenye hali ya ugonjwa huu unajua kwamba huo ndio mwisho wake,
Mungu tu kwake hakuna lisilowezekana, Tumtumainie Yeye kwenye shida hizi
 
DEGEDEGE ni hali ya ghafla ya kutingishika mwili mzima au mikono na miguu kunakosababishwa na kukakamaa kwa misuli ya mwili.

Tatizo la degedege mara nyingi linatokana na magonjwa au hitilafu katika ubongo ambapo husababisha kutokea kwa upungufu wa vichocheo vya sukari kwenye damu (Hypoglycemia) pamoja na upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye damu (Hypoxia).

Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, huku asilimia 80 wakiwa Waafrika.
Hata hivyo, maradhi haya husababishwa na magonjwa mbalimbali na mara nyingi hujitokeza kwa watu ambao wana familia yenye historia ya ugonjwa huu au kifafa.

Watu wa rika zote wanaweza kuathiriwa na degedege, lakini watoto na vijana ndio huathirika zaidi na inapojirudia huitwa kifafa.

Imani za kuwa mtu mwenye degedege hachomwi sindano zimechangia kuongezeka kwa vifo au mtindio wa ubongo ambavyo hutokea iwapo maradhi haya hayakutibiwa kwa haraka na kwa ufasaha.

Wakati mwingine si rahisi kubaini iwapo mtu amepatwa na degedege kutokana na baadhi ya watu hushikwa na bumbuwazi (kuduwaa) kwa muda mfupi hivyo kutojua kama amepatwa na degedege au la.

Dalili
Wataalamu wa afya wanasema dalili za maradhi haya hutegemea sehemu ya ubongo ambayo imeathirika na hujitokeza kwa haraka ambapo husababisha mwili, miguu na mikono kuanza kukakamaa na kurudisha kichwa nyuma.

Kushindwa kupumua na kutokwa na mapovu mdomoni, macho kugeukia nyuma na kuonekana kwa sehemu nyeupe ya jicho.

Kupoteza fahamu au kuzimia ikifuatiwa na kuchanganyikiwa (mgonjwa anapoteza kumbukumbu) pamoja na kushindwa kuzuia mkojo na haja kubwa.
Hata hivyo, shambulio la degedege huisha baada ya muda mfupi mara nyingi chini ya dakika tano.

Baada ya shambulio hupitiwa na usingizi mzito kama takribani dakika 30 hadi saa nzima na azindukapo hushindwa kutambua kitu chochote kwa muda.

Chanzo chake
Degedege si ugonjwa bali ni maradhi yanayosababishwa na magonjwa mbalimbali,pia hutokana na kuvurugika kwa mfumo wa umeme katika ubongo.

Chanzo kikubwa cha degedege hutokana na maambukizi kwenye ubongo na uti wa mgongo.
Kuumia ubongo kunakoweza kujitokeza wakati wa kujifungua, ugonjwa wa malaria, homa kali hasa kwa watoto, kifafa pamoja na kifafa cha mimba.

Matibabu
Matibabu yake hutegemea chanzo cha maradhi hayo, mfano iwapo degedege imesababishwa na malaria au homa ya uti wa mgongo, mgonjwa anapaswa kutumia dawa za kutibu malaria na antibiotiki.

Pia mgonjwa huweza kutumia dawa zinazosaidia kudhibiti degedege

Madhara
Mwenye degedege asipopata tiba sahihi kwa wakati anaweza kupatwa na madhara yafuatayo:
1. Kupata tatizo la kifafa, mtindio wa ubongo kwa watoto inaweza kuchangia uelewa duni katika masomo yake.

Ukuaji duni kwa mtoto hasa kama degedege ikiwa itamtokea mara kwa mara hatimaye mtoto kudumaa.
Inashauriwa na wataalamu wa afya kuwa pindi mtu apatapo degedege kuwahishwa haraka katika zahanati ili kumwepushia kupata magonjwa ambayo yanaweza kumsababishia magonjwa ya kudumu katika maisha yake.

Mtanzania
 
NAOMBENI MSAADA KWA ANAEJUA DAWA YA KIFAFA

Niliuguliwa na mtoto alipatwa homa. Kali sana nilimpeleka hosptali nikaambiwa ana degedege hivyo alitibiwa.Mida ilipita nashanga alipofikisha umri wa miaka 14 .Ghafla alianza kuanguka mpaka sasa.Hivyo nilimpeleka hospital.Aliandikiwa Dawa Aina ya phenorbabitore lakini bado tu anaanguka.Yani napata tabu Sana.

NAOMBENI MSAADA wenu
 
Stroke au kiharusi ni ugonjwa unaotisha sana. Tumeambiwa kila maradhi yana dawa yake, isipokuwa labda iwe ni adhabu. Kuna njia ya kumsaidia mtu aliyepata 'stroke' ili asiathirike kwa kupooza au kuwa ni sababu ya mauti yake. Usisahau msaada huu utafanikiwa tu ikwa Mungu atapenda. Hakikisha ndani ya nyumba kuna hakiba ya sindano ya hospitali mpya ambayo haijatumika. Utakapogundua kuwa mtu amepata 'stroke', fuata utaratibu ufuatao ili umnusuru na matatizo makubwa ya baadae:

1. Msaidieni mgonjwa akae bila ya kumuondosha pale alipoanguka, mkimuondosha mtamsababishia madhara makubwa ya kupasuka mishipa mwembamba ya damu iliyoko kwenye ubongo.

2. Baada ya kumkalisha toboa ncha za vidole vyake 10 vya mkononi kwa kutumia sindano ili matone ya damu yatoke. Unaweza kutumia sindano ya aina nyengine lakini ni lazima ipashwe moto kwanza ili kuua bakteria.

3. Ikiwa hatorudi kwenye hali yake ya kawaida (yaani mdomo wake bado umeelekea upande) chua (vuta) masikio yake kuelekea chini ili ukusanye damu kwenye ndewe. Kisha toboa ndewe utoe matone ya damu. Baada ya muda mfupi mgonjwa atarejea katika hali yake ya kawaida.

4. Mpelekeni sehemu yenye upepo apumzike kidogo baadae mpelekeni hospitali. Ni muhimu kuzingatia kuwa mgonjwa asihangaishwe au kupelekwa hospitali kabla ya huduma hii maana mtikisiko wa safari utasababisha mishipa ya damu kwenye ubongo kupasuka na kuondosha uwezekano wa kurejea katika hali yake ya kawaida. Suleiman Kitwana ambae ametafsiri taarifa hii anakuuliza 'Je? Unazijua dalili za mtu aliyepata 'stroke'? Kama huzijui zitafute ujifunze. Huduma hii ya mwanzo ni muhimu sana na inamfanya mtu aliyehudumiwa kurejea katika hali yake ya kawaida asilimia mia moja (100%). Ikiwa unahisi taarifa hii ni muhimu tafadhali isambaze kwa watu ili tuokoe maisha ya familia zetu.
 
Sodiun valproate, mtoto ni wa kike au wa kiume? Kwa wanawake side effect ya dawa hii ni irregular menstrual cycles
 
Stroke au kiharusi ni ugonjwa unaotisha sana. Tumeambiwa kila maradhi yana dawa yake, isipokuwa labda iwe ni adhabu. Kuna njia ya kumsaidia mtu aliyepata 'stroke' ili asiathirike kwa kupooza au kuwa ni sababu ya mauti yake. Usisahau msaada huu utafanikiwa tu ikwa Mungu atapenda. Hakikisha ndani ya nyumba kuna hakiba ya sindano ya hospitali mpya ambayo haijatumika. Utakapogundua kuwa mtu amepata 'stroke', fuata utaratibu ufuatao ili umnusuru na matatizo makubwa ya baadae:

1. Msaidieni mgonjwa akae bila ya kumuondosha pale alipoanguka, mkimuondosha mtamsababishia madhara makubwa ya kupasuka mishipa mwembamba ya damu iliyoko kwenye ubongo.

2. Baada ya kumkalisha toboa ncha za vidole vyake 10 vya mkononi kwa kutumia sindano ili matone ya damu yatoke. Unaweza kutumia sindano ya aina nyengine lakini ni lazima ipashwe moto kwanza ili kuua bakteria.

3. Ikiwa hatorudi kwenye hali yake ya kawaida (yaani mdomo wake bado umeelekea upande) chua (vuta) masikio yake kuelekea chini ili ukusanye damu kwenye ndewe. Kisha toboa ndewe utoe matone ya damu.
Baada ya muda mfupi mgonjwa atarejea katika hali yake ya kawaida.

4. Mpelekeni sehemu yenye upepo apumzike kidogo baadae mpelekeni hospitali. Ni muhimu kuzingatia kuwa mgonjwa asihangaishwe au kupelekwa hospitali kabla ya huduma hii maana mtikisiko wa safari utasababisha mishipa ya damu kwenye ubongo kupasuka na kuondosha uwezekano wa kurejea katika hali yake ya kawaida. Suleiman Kitwana ambae ametafsiri taarifa hii anakuuliza 'Je? Unazijua dalili za mtu aliyepata 'stroke'? Kama huzijui zitafute ujifunze. Huduma hii ya mwanzo ni muhimu sana na inamfanya mtu aliyehudumiwa kurejea katika hali yake ya kawaida asilimia mia moja (100%). Ikiwa unahisi taarifa hii ni muhimu tafadhali isambaze kwa watu ili tuokoe maisha ya familia zetu.
Hiyo ndewe ndio kitu gani?
 
Back
Top Bottom