Habari,
Yapata mwezi sasa nimekuwa nikikumbwa na tatizo la kuwashwa mwili kama nimemwagiwa upupu, hasa mida ya saa tatu usiku ambapo mambo yanakuwa mabaya zaidi na najikuna vibaya mno. Mwanzo, mtoto wangu mmoja alianza na hali hii, kisha ikaenea kwa watoto wote. Walipokuwa wanashindwa kulala sababu ya kujikuna, sikuwa naelewa kama walikuwa wanapitia kipindi kigumu kiasi hiki.
Baada ya kupewa tiba ya siku 14, watoto walipona, lakini mmoja ameanza tena kupata vipele vibaya mikononi na miguuni. Nachanganyikiwa kuelewa ni ugonjwa gani huu. Na si sisi tu, inaonekana kama umeenea kimya kimya. Leo nikiwa kwenye duka la dawa, nilikutana na mtu mwingine aliyekuwa akiomba dawa itakayomsaidia yeye na familia yake, ambao pia wanapitia hali kama yangu. Pia, dada yangu ambaye yupo Shinyanga naye analalamika hivyo hivyo kuwa wamepatwa na ugonjwa huu wa kuwashwa mwili.
Wakuu, kuna yeyote anayepitia changamoto kama hii? Mimi nipo Ruvuma na si msimu wa joto. Cha ajabu ni kuwa hata walio katika hali ya hewa ya joto wanalalamika kama mimi. Hii ni nini? Wataalam wa mambo wanasema ni maambukizi ya fungus kwenye damu, ingawa sijui kama nilisikia vizuri au nilikuwa busy na gitaa.
MSAADA HATA WA MAWAZO UTASAIDIA. Nilipewa Ethromaisini lakini bado nakesha nikijikuna. Mpaka sasa nimejaribu dozi kadhaa bila mafanikio, kuna unafuu kidogo lakini tatizo linarejea palepale.