Ugonjwa wa macho

Ugonjwa wa macho

Bizzly

Member
Joined
May 3, 2010
Posts
79
Reaction score
24
Wadau naombeni msaada wenu, mimi nina tatizo la macho macho yangu yalianza kuwasha miezi kama miwili iliyopita, nikaenda hospital Regency nikapewa dawa ya matone(drops) nikaambiwa nitumie siku 7.

Baada ya siku 7 kuisha nikaenda tena nikabadilishiwa dawa nikapewa ya kutumia mwezi mzima.

Nimetumia hiyo dawa macho yakawa hayawashi isipokuwa mpaka sasa nasumbuliwa na kutoka matongotongo hasa asubuhi na inapofika jioni/usiku macho yanakuwa kama na ukungu fulani.

Tafadhalini sana wataalamu naombeni ushauri nifanyeje?
 
J.tatu katika kipindi kimoja cha afya ya jamii ITV walizungumzia kuhusu presha ya macho ambayo huanza bila maumivu lakini ni hatari kwa kusababisha upofu. ni bora uende hospitali kwa wataalamu wa macho upate vipimi vya uhakika.
 
Back
Top Bottom