McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Wakuu,
Ugonjwa wa Mpox wasambaa Magharibi mwa Kenya Kaunti za Busia, Bungoma na Kakamega zimeathiriwa na mlipuko wa ugonjwa wa Mpox, unaosababishwa na virusi.
Busia ni ya pili kwa athari nchini Kenya, ikiwa na maambukizi 56 yaliyothibitishwa, wagonjwa wawili wamelazwa, wanane wanatibiwa nyumbani, na vifo viwili vimeripotiwa. Jumla ya kesi 226 zimeripotiwa katika kaunti 13.
.
Mamlaka za afya Busia, zikiongozwa na Timu ya Usimamizi wa Afya ya Kaunti (CHMT), zimeanzisha mikakati ya kudhibiti maambukizi. Mratibu wa uchunguzi wa Mpox, Evans Shiraku, amesema kuwa ukaribu wa Busia na Uganda ni changamoto kutokana na hatari ya maambukizi kuvuka mpaka.
.
Kati ya wagonjwa, 53 ni Wakenya na 3 ni raia wa Uganda.