Ugonjwa wa Ngiri (Hernia), Dalili na tiba yake

Ugonjwa wa Ngiri (Hernia), Dalili na tiba yake

Kwanza niseme kuwa kwa kiswahili bado kuna mkanganyiko wa neno Ngiri. Wapo wanoiita ngiri kwa maana ya busha (hydrocele), na wengine huita ngiri (Hernia) ambayo ni sehemu ya viungo kuingia sehemu nyingine kwasababu ya kuwa l'oose'

Kwa maelezo yako nadhani unaongelea abdomen hernia ambayo sehemu ya utumbo hutumbukia katika hasua. Hii ni kwasababu sehemu inayozuia (kiwambo) inakuwa imeachia. Utumbo huingia huko na kukuletea maumivu. Siyo maradhi yanayosababishwa na wadudu, hutokea hata kwa watoto wadogo au watu wazima ambao hufanya kazi za nguvu n.k.

Hakuna dawa inayotibu bali zinazopunguza maumivu. Mara nyingi ukilala na taratibu kusukuma hicho unachokihisi kurudi juu, basi hali inaweza kutulia. Itajirudia tena tena kwasababu umesogeza tu lakini hujazuia.

Matibabu yake ni operesheni ya kufunga sehemu hiyo. Matibabu hayo ni muhimu sana kwasababu inaweza kutokea kuwa utumbo umeingia ukajikunja na kushindwa kupitisha damu (strangulated hernia) hivyo sehemu hiyo itaoza na kuweza kuleta madhara makubwa zaidi tusiyotarajia.
Hutokea nadra lakini inapotokea hujui utakuwa sehemu gani ya huduma muhimu na za haraka hapo unaweza kujikuta katika wakati mgumu sana kimaumivu na pengine kimaisha.

Tafadhali kawaone madaktari katika hospitali kubwa kwa ushauri zaidi.
source:
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/177748-ugonjwa-wa-ngiri.html

Mkuu nashukuru kwanza kwa kukubali kubadilisha hiyo lugha ya kingereza kuwa kiswahili kwa faida ya wengi. Nakumbuka mwezi ulopita niliweka thread kama hii nikiwa nasumbuliwa na huu ugonjwa wa ngiri. Nimeshaonana na doctor na ameniambia nahitaji upasuaji. Hivyo ndo najiandaa kwa operation. Asanteni kwa wale walotoa mchango wao wa kunishauri.
 
Wakuu nina tatizo la kutopata choo(Nikifika chooni mzee anafika mpaka dirishani lakini hatoki ng'o) wakati wa baridi au nikipigwa na baridi kama ya ac, sometime nikinywa maji ya baridi. Ukienda hospitali wanakupa dawa za constipation. Daktari huwa wananiambia niwe nakunywa maji na kula matunda sana. Ukweli ni mlaji sana wa matunda na kunywa maji yasipongua lita 3 kwa siku.

Katika uchunguzi wangu nimegundua kwamba tatizo hili hutokea wakati nikihisi hali ya ubaridi kama nilivyoelza hapo juu, nimegundua kwamba hii itakuwa ngiri tu ingawa sihisi chochote kuvimba kwenye mwili wangu.

Nani anajua dawa ya tatizo hili. Kama ni ngiri je ipi ni tiba yake ya kudumu acha hizi za muda

Nawasilisha
 
Nenda Pale Eneo la Temeke Vetenary kuna kituo cha Mafuta OIL COM, next building ni msikiti, unaitwa Masjid Iman. Ukifika hapo utaona kuna kibanda kidogo geti la kuingia msikitini. Hapo kuna jamaa anauza dawa za miti shamba. Kuna dawa ya mchanganyiko wa miti mbalimbali inaitwa MIDDLE FILDER. Ukiitumia dawa hiyo naamin tatizo lako litaisha. Naomba usidharau kama kweli unatatizo hilo.
 
Nenda Pale Eneo la Temeke Vetenary kuna kituo cha Mafuta OIL COM, next building ni msikiti, unaitwa Masjid Iman. Ukifika hapo utaona kuna kibanda kidogo geti la kuingia msikitini. Hapo kuna jamaa anauza dawa za miti shamba. Kuna dawa ya mchanganyiko wa miti mbalimbali inaitwa MIDDLE FILDER. Ukiitumia dawa hiyo naamin tatizo lako litaisha. Naomba usidharau kama kweli unatatizo hilo.

Mkuu nashukuru sana. Tatizo lipo.Nitalifanyi akazi mkuu. Nikirudi nitakubrief
 
Dawa yake ndgo husinywe maji na vingine vya baridi!
 
wakuu naomba kujua huu ugonjwa wa enia hauna tiba mbali na upasuaji?karibuni sana.
 
Na Ngiri ingine ni ya Mshipa wa Kushuka ni hii hapa Mabusha kwa lugha ya kiswahili
IMabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu. Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani.

Inakadiriwa kuwa karibu asilimia moja ya wanaume wote kote duniani huathiriwa na tatizo hili. Kwa hapa nchini, tatizo hili ni maarufu sana maeneo ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kiasi cha kuhusishwa na imani kadhaa.

Mojawapo ya dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wa mwambao ni kuwa mabusha yana uhusiano mkubwa na unywaji wa maji ya madafu. Aidha, tatizo hili limekuwa likichukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni hali ya kudhalilisha

ingawa kwa wengine huonekana ni hali ya kuwa ‘mzee wa heshima’ au ‘umwinyi’.
Ifahamike pia kuwa, tatizo la mabusha halitokei kwa wanaume watu wazima tu. Watoto wa kiume hususani katika

mwaka wa kwanza (infants) pia ni waathirika wakuu wa tatizo hili.
Kwa kawaida mabusha hayana maumivu na wala hayaleti madhara, isipokuwa kama yatapata uambukizi kwa sababu nyingine yeyote ile, hali inayowafanya wengi wa waathirika, hasa wa mwambao, kuwa wagumu kutafuta ufumbuzi wa tiba.

Hata hivyo, ni vyema kama mtu ana uvimbe wowote kwenye pumbu zake, kutafuta msaada wa kitabibu ili kuweza kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa magonjwa mengine ya sehemu za siri kama vile saratani ya korodani (testicular cancer) n.k.

Mabusha husababishwa na nini?
Sababu za kutokea kwa mabusha hutofautiana kati ya watoto wa kiume na wanaume watu wazima.
Kwa watoto wa kiume

Kwa watoto wa kiume, mabusha huweza kuanza kutokea kipindi cha ujauzito.
Wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa kiume huwa kwenye tumbo lake kabla ya kushuka taratibu kuelekea

kwenye mapumbu. Wakati wa ushukaji huo, kifuko kinachozunguka korodani kinachoitwa processus vaginalishushuka sambamba na kurodani hizo na kufanya korodani kuzungukwa na maji.

Kwa kawaida, ndani ya muda wa mwaka mmoja, kifuko hiki hufunga na maji hayo yanayozunguka korodani yote hufyonzwa na kurudishwa kwenye tumbo la mtoto. Iwapo baada ya kifuko kufunga na maji yaliyomo kushindwa

kufyonzwa kurudishwa kwenye tumbo la mtoto, mtoto hupata busha lijulikanalo kitaalamu kama busha lisilo na mawasiliano (non-communicating hydrocele).
Hali kadhalika, wakati mwingine inawezekana kifuko kikashindwa kufunga na hivyo maji yakaendelea kujaa ndani ya

kifuko kuzunguka korodani. Aina hii ya mabusha kwa watoto ujulikana kama busha lenye mawasiliano (communicating hydrocele).
Kwa wanaume watu wazima

Kwa wanaume watu wazima, mabusha husababishwa na mambo makuu mawili; Kwanza, kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida, na njia ya pili ni kupungua kwa ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of scrotal

lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili (blockage of scrotal venous system).
Ongezeko la uzalishaji wa maji linaweza kutokana na

Maambukizi au/na majeraha katika korodani (testicular inflammation auorchitis) au maambukizi katika mshipa ujulikanao kama epididymisyanayoweza kusababishwa na kifua kikuu (tuberculosis) cha makende, au maambukizi yanayosababishwa na vimelea wa filaria (filariasis) wanaosababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.
Kujinyonga kwa korodani (testicular torsion) kunakoweza kuzifanya korodani kutenda kazi zaidi ya kiwango chake (hyperactive testis).
Uvimbe katika korodani (testicular tumors) ambao husababisha uzalishaji wa maji kupita kiasi.

Kupungua kwa ufyonzaji wa maji hutokana na

Kufanyiwa upasuaji kipindi cha siku za nyuma katika eneo la kinena, au operesheni ya upandikizaji figo ambazo zinaweza kuathiri mfumo wa lymph na vena na hivyo kupunguza ufyonzaji wa maji kutoka kwenye mapumbu.
Kuwahi kufanyiwa tiba ya mionzi kipindi cha nyuma nayo uhusishwa na kutokea kwa mabusha.

Kwa hapa kwetu Tanzania, kung’atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria kunaelezwa kuwa sababu kuu mojawapo inayopelekea kuwepo kwa tatizo la mabusha na matende hususani maeneo ya Pwani na mwambao.
Dalili za Mabusha

Katika hatua za awali, mabusha huwa hayana dalili zozote (asymptomatic).
Hata hivyo, baada ya muda fulani, mapumbu hujaa na uvimbe huweza kuonekana hata kwa nje. Kwa kadiri uvimbe unavyozidi kuongezeka, dalili zifuatazo zaweza kujitokeza pia;

Muhusika kujihisi hali ya uzito na kuvuta sehemu za siri kutokana na kujaa na kuongezeka kwa uzito wa mapumbu.
Mgonjwa huweza kujihisi hali ya usumbufu na kutojisikia vizuri maeneo ya kinena mpaka mgongoni.

Kwa kawaida mabusha hayana maumivu yeyote. Hata hivyo, iwapo mgonjwa ataanza kujihisi maumivu, hiyo ni dalili ya kuwepo kwa uambukizi katika mshipa wa epididymis (acute epididymitis)

Uvimbe huwa na tabia ya kupungua iwapo mgonjwa atakaa kitako na huongezeka pindi anaposimama.
Iwapo mgonjwa atajisikia homa, kichefuchefu na kutapika, hizo ni dalili za kuwepo kwa uambukizi katika mabusha.

Kwa kawaida mabusha hayana muingiliano na uwezo na ufanisi wa utendaji wa ngono. Hata hivyo kuna taarifa tofauti za kitafiti kutoka bara Asia na Afrika Magharibi kuwa mabusha yanaweza kuathiri ufanisi wa ngono na kwa kiasi fulani kusababisha mhemko au msongo wa mawazo kwa muathirika.

Uchunguzi na Vipimo

Uchunguzi mzuri wa kitabibu (physical examination) huwezesha kugundua uwepo wa mabusha kwa kiasi kikubwa bila hata kuhitaji vipimo vya ziada. Vipimo uhitajika tu kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha mabusha, madhara yaliyoletwa na mabusha au kujua hali ya korodani.
Vipimo ni pamoja na

Kupima damu (Full Blood Count) na mkojo (Urine Analysis) kuchunguza uwepo wa maambukizi kama vile vimelea wafilaria na mengineyo.

Ultrasound ya kinena pamoja na mapumbu: Aina hii ya kipimo hufanywa ili kuchunguza uwepo wa matatizo mengine tofauti na mabusha. Matatizo hayo ni kama vile ngiri, uvimbe, kujinyonga kwa korodani (testicular torsion), majeraha katika korodani, damu kuvuja kwenye kwenye korodani (traumatic hemorrhage) au maambukizi.

Matibabu ya Mabusha

Kwa watoto wadogo, kwa kawaida mabusha hupotea yenyewe ndani ya mwaka mmoja. Iwapo hayajapotea, mtoto uhitaji kufanyiwa upasuaji kama tiba.

Kwa wanaume watu wazima, mabusha pia huweza kupona yenyewe bila kuhitaji tiba. Iwapo mabusha hayajapotea na yanamletea mgonjwa usumbufu (discomfort) au hali mbaya ya kiumbo (disfigurement) hayana budi kufanyiwa upasuaji ili kuyaondoa.
Njia za tiba ni
Upasuaji: Upasuaji wa mabusha huweza kufanyika bila ya mgonjwa kuhitaji kulazwa (outpatient). Madhara yanayoweza kutokea wakati wa upasuaji wa mabusha ni pamoja na damu kuganda (blood clots), maambukizi au majeraha kwenye korodani. Hii ndiyo njia maarufu zaidi na ya kuaminika ya matibabu ya mabusha duniani kote.


Kunyonya maji kwa kutumia sindano maalum (Needle aspiration): Njia nyingine inayotumika kutibu mabusha ni kuyanyonya maji kwa kutumia sindano maalum (needle aspiration). Hata hivyo njia hii haitumiki sana sehemu nyingi duniani kwa sasa kwa sababu maji ya mabusha huwa yana tabia ya kujirudia baada ya muda mfupi hata kama yatanyonywa.

Baadhi ya matabibu hupendelea kudunga dawa maalum za kuzuia maji yasijae tena (sclerosing agents) mara baada ya kunyonya na kuyaondoa maji yote.
Njia hii ya kunyonya maji ya mabusha, hufaa zaidi kwa wagonjwa wasioweza kuhimili upasuaji. Madhara yanayoweza kusababishwa na tiba ya namna hii ni pamoja na maambukizi na maumivu kwenye korodani.
Hata hivyo wakati mwingine, bila kujali ni tiba gani imetumika, mabusha huweza kujirudia baada ya matibabu.
Madhara ya Mabusha
Kwa kawaida mabusha hayana madhara yeyote. Aidha mabusha hayawezi kuathiri uwezo wa mtu kuzaa. Hata hivyo mabusha yanaweza kuleta madhara iwapo tu kama yakiambatana na magonjwa mengine kwenye korodani.
Kwa mfano, kama mabusha yataambatana na maambukizi (testicular infection) au uvimbe kwenye korodani (testicular tumor), yanaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji na utendaji kazi wa mbegu za kiume (sperms) na kupelekea tatizo la ugumba kwa wanaume.
Hali kadhalika, iwapo sehemu ya utumbo mkubwa au mdogo imebanwa katika upenyo fulani kwenye sehemu ya ukuta wa tumbo, huweza kusababisha ngiri (strangulated hernia), hali ambayo ni hatari kama isipotibiwa haraka.
 
Kwa anaye fahamu ugonjwa huu wa ngiri atueleze kinaga ubaga maana kuna hali fulani hivi ndugu yangu wa karibu amenielezea eti anasikia maumivu kwa mbali upande wa kushot wa tumbo kwa chini na wakati mwingine tumbo lina jaaa gesi na pia akifanya mapenzi uw anajisikia tumbo lina jaa gesi ni itakua ngiri au nn
 
Muwahisheni hosptl mapema. Nadhani ana hernia au busha mtoto.
Very sorry mtoto.
 
Kuvimba Pumbu, inaweza kuwa chochote hata infection si lazima iwe busha au hernia. Mpeleke hospitali.
 
Mgonjwa huyo nadhani henia.

You are right...hiyo ni 'Right Inguinal Hernia'. Kunakuwa na weakness ya misuli inayotengeneza abdominal wall kwa chini huo upande wa kushoto, hivyo inapoongezeka presha kwenye tumbo (intra-abdominal pressure)..utumbo unasukumwa kupitia hiyo sehemu dhaifu na kuingia kwenye mfuko wa pumbu!

Inatibika, waone maDaktari wapasuaji wamfanyie upasuaji kureinforce hiyo weak abdominal wall (Herniorraphy) na tatizo linakuwa solved.

NB: Ni muhimu kumfanyia haraka iwezekanavyo kwani kuna kipindi utumbo ukishuka unakwama huko na kusababisha utumbo kuziba (Obstructed Hernia) au hata kuzuia damu kwenda kwenye hiyp sehemu ya utumbo iliyopenya kwanya mfuko wa pumbu na kuiozesha (Strangulated Hernia). Ni vyema akafanyiwa upasuaji kabla haijasababisha matatizo hayo mawili kwani HUUA!
 
Kuvimba Pumbu, inaweza kuwa chochote hata infection si lazima iwe busha au hernia. Mpeleke hospitali.

Hujakosea, ni kweli kuvimba pumbu kunaweza sababishwa na mambo mengi, commonly Hernia, Busha (Hydrocoele), na hata infection. Lakini inabidi uende zaidi ya hapo kujua ni kipi kati ya hivyo. Hiyo ni more likely Inguinal Hernia kwa sababu imevimba tokea kwenye inguinal area, na ni upanda mmoja. Busha na infection hazivimbi inguinal area upande mmoja.
 
Ingekua ya mtoto wa kike ingeonyeshwa ivi?

Ivi kwanini watoto wa kiume nyeti zao huwa hazithaminiwi hivi?

Utakuta asubuhi mtoto wa kiume na govi lake anazurula nalo mchana kutwa, lakini wa kike anavalishwa pindi akiamka na akiwa hajashuka kitandani, kwanini double standard?
 
right inguinal hernia ...! mara nyingi ni common kwa wanaume ..! mpeleke hospital atapona
 
Wakuu wote nashukuru kwa ushauri, Nitamfahamisha mwenye mtoto. Once again, thank you guys for your help and concerns.
 
Back
Top Bottom