Me mwenyeji wa Moro naujua huo ugonjwa rafiki zangu wengi wameugua wakati tunasoma. Ni ugonjwa wa ngozi ambao ni vigumu kupona haraka ila ukiwa na nia utapona tena kwa dawa nyepesi sana.
Nenda duka la dawa nunua dawa ya kupaka inaitwa Whitefield ipo kama mafuta ya mgando hivi. Hii ndo kiboko ya fangasi ya ngozi. Ukiipata hii dawa ni hatua moja ila unatakiwa ufuate maelekezo jinsi ya kuitumia ili upone maana wengi hufeli hapa.
Hakikisha unaoga angalau mara mbili kwa siku na asubuhi na jioni au usiku. Baada ya kuoga usipake mafuta yoyote ila paka hiyo Whitefield mwili mzima kuanzia kichwani hadi unyayoni ila kuwa makini kwenye sehemu laini kama mapumbu maana inawasha baadhi ya sehemu laini kama ikulu huko.
Pia hakikisha ukivaa nguo usiirudie tena mpaka ifuliwe na kupigwa pasi tena ikiwezekana fua kwa jik na sabuni ili kuondoa fungus. Na kitandani shuka ukilalia mara moja itoe uifue kifupi inabidi umaintain usafi kwa hali ya juu sana.
Tumia hiyo dawa kwa wiki mbili mfululizo utaoma matokeo. Pia kama unawashwa sana basi tafuta vidonge vinaitwa cetrizine vinasaidia kuondoa muwasho kwenye ngozi. Ukienda duka la dawa utaelekezwa matumizi ya hivyo vidonge.
So vitu vitatu muhimu
1. Tumia Whitefield kupaka mara mbili kwa siku 2. Maintain usafi, nguo utakayotumia usiirudie hata iwe leso.
3.Tumia cetrizine kuondoa muwasho.
Hiyo ndiyo dawa ya utangatanga nimekushauri nikiwa mkazi wa Moro so naujua huo ugonjwa pia nimekushauri kama mtaalam wa afya by professional. Huo ugonjwa hospital utapata shida kupona.
Sent using
Jamii Forums mobile app